Na Mwanahabari Wetu
Sekta ya ‘Mauzo ya Moja kwa Moja’
kufafanuliwa – QNET
·
Dhana
potofu zilizosambaa kuhusu sekta ya mauzo ya moja kwa moja
Tarehe 4 Aprili 2019
Biashara
ya masoko ya mtandao inakuwa kwa kasi nchini na katika kanda hii kwa ujumla
ambayo ni matokeo ya ongezeko la idadi ya watu na vijana wenye umahiri. Hata
hivyo bado kuna dhana zisizo sahihi kwamba hii sio biashara halali.
Dhana
hii potofu inaendelea kuwepo licha ya kwamba biashara ya masoko ya mtandao ya
kitaalamu ni sekta yenye thamani ya dola za kimarekani billioni 190 ikiwa na
zaidi ya wasambazaji milioni 96 duniani kote. Kampuni ya mauzo ya moja kwa moja
ya QNET ni sehemu ya sekta hii ambayo imedhibitiwa na sheria, maadili na taratibu
za utendaji zile zinazosimamia taasisi halali.
Meneja Mkuu wa kanda wa QNET Kanda ya
Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika wakati alipotembelea jijini Dar es salaam
hivi karibuni, Biram Fall alikanusha dhana potofu kwa kusema kwamba kampuni ya
QNET inaendesha biashara halali katika nchini nyingi na duniani kote na wanatoa
bidhaa na huduma halisi.
Bwana Fall alikuwa nchini wakati
kampuni ilipoendesha maonesho ya Expo kuonyesha bidhaa na huduma kwa wateja,
ambapo alibainisha kwamba wamekuwa wakiendesha shughuli biashara hii kwa zaidi
ya miongo miwili na iwapo ingekuwa sio biashara halali haingeweza kudumu kwa
muda mrefu kama hivyo.
“Mifumo ya Piramidi huwa haidumu
kwa muda mrefu kama ilivyodumu kampuni hii ambayo imekuwa inafanya kazi tangu
1998, matapeli kama hao huwa hawawezi kustahimili” alisema bwana Fall.
Aliongeza zaidi kwamba kampuni hii
ina nembo yenye sifa nzuri na inayojulikana duniani ambayo iko tayari kuilinda
na hivyo haiwezi kujihusisha na utapeli wa aina yoyote.
“Watu wabaya watakuwepo siku zote
hapa na pale, hii ni changamoto. Lakini kwa suala la kanuni tunawahakikishia
kuwa biashara katika QNET inaendeshwa kimaadili na kwa sababu hatuko hapa kuwadanganya
watu ninawahakikishia kuwa QNET itaendelea kuwa hapa kwa muda mrefu” alisema
bwana Fall.
Tofauti kabisa na dhana hiyo
kampuni ya QNET imekuja kuwawezesha watu, hasa vijana, alisema akiongeza kwamba
kwa mujibu wa Tathmini ya Idadi ya Vijana Afrika iliyofanywa na Taasisi ya
Maendeleo ya Afrika (African Institute
for Development), kwa sasa Afrika ina zaidi ya asilimia 45% kati ya watu milioni
150 walioko Kenya, Tanzania, Rwanda na Uganda.
Wengi wa vijana hawa wana elimu, wengi
wana ufahamu wa teknolojia, wanauwezo wa kuendana na mifumo mipya kwa haraka,
wanahamasa ya kuweka juhudi na wana fikra za ujasiriamali – sifa ambazo ni za
msingi zinazohitajika kwaajili ya mafanikio endelevu katika biashara ya mauzo
ya moja kwa moja.
Biashara ya Masoko ya Mtandao au
Mauzo ya Moja kwa moja ni dhana ya biashara ya kimataifa na inaelezewa kama
‘uuzaji wa bidhaa au huduma kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, mbali na maduka
halisi ya kawaida.’ Mtindo huu wa mauzo una umri wa zaidi ya miaka 100 na
ulianzishwa mwanzoni huko nchi USA.
Leo, kuna takribani watu milioni
117 wanaohusika katika biashara hii. Kwa mujibu wa taarifa ya mwaka ya Shirikisho la Vyama
vya Mauzo ya Moja kwa Moja Duniani (World Federation of Direct Selling Association)
(WFDSA) ya mwaka 2018, biashara ya mauzo ya moja kwa moja ilizalisha dola
bilioni $190 za marekani na takribani nusu ya mauzo yote yametokea katika
masoko yanayochipukia.
Afrika imechangia chini ya asilimia
1% ya jumla ya mauzo ya WFDSA lakini wataalamu wanatabiri kwamba soko la Afrika
Mashariki linatoa fursa ya kukua kwa wajasiriamali wenye ari na hata kwa wale
wenye kazi za kudumu na wanania ya kujipatia kipato cha ziada kupitia mauzo ya
moja kwa moja.
Katika kanda ambayo matakwa ya
ajira rasmi yanazidi kuwa na ushindani na kazi za kudumu kuendelea kuwa kidogo
sana, biashara ya mauzo ya moja kwa moja inatoa njia mbadala wa ajira za kawaida
kwa wale wanaohitaji kipato cha ziada kuongeza kipato kwaajili kwa mahitaji ya
nyumbani, au kwa wale ambao mazingira hayawaruhusu kujipatia ajira rasmi.
Wakati ambapo mtindo huu wa
biashara inakabiliwa na changamoto, changamoto kubwa zaidi ni kuenea kwa mifumo
isiyo halali ya piramidi ambayo inajiwasilisha kama kampuni halali ya biashara
ya mauzo ya moja kwa moja, ambayo inawaahidi wawekezaji wanaotaka kuwekeza kuwa
watapata faida kubwa iwapo watawaandikisha watu wengine.
Hoja ni kwamba ‘matapeli’ hawa wanajenga
dhana potofu kwenye sekta ya Mauzo ya moja kwa moja, jambo ambapo linaleta
vikwazo kwa kampuni halali kusajili mawakala
wa mauzo na kuendesha biashara zao halisi na halali.
Matokeo yake, kampuni inatatua
tatizo hilo kwa kuwaelimisha umma kuwa makini na ‘matapeli’ kama hao na kuwahamasisha
kuthibitisha uhalali wa kampuni yoyote kulingana na inavyotekeleza na kutii
kanuni, sheria na taratinbu zilizowekwa na bodi zinazosimamia na mamlaka
zinazohusika.
Katika kuimarisha uwepo wake
nchini, kampuni ilifanya maonesho ya bidhaa jijini Dar es salaam ambayo
yalibarikiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Paul Makonda, ambaye
aliwapa changamoto vijana wanaotafuta fursa kupitia katika kampuni hii kuwa na
ujasiri wanapofanyia kazi ndoto zao ili waweze kuwa na mafanikio.
Makonda alisema kwamba historia ya
maisha yake binafsi ni ushahidi wa kutosha kwamba kufanyakazi kwa bidii na ujasiri
hatimae huleta mafanikio na kuwaasa vijana wadogo kutokutosheka na mafanikio
madogo.
Alisema, “Historia ya maisha yangu ni ushahidi
kwamba kwa kufanyakazi kwa bidii na kuwa na ujasiri kila wakati unaweza kupata
mafanikio unayoyatafuta. Usiridhike kwa mafanikio au vitu vidogo vidogo kuliko
ndoto zako”.
Maonyesho ya bidhaa ya Expo
yaliyobeba jina la Kuishi Kikamilifi ‘Absolute Living’ inayoendana na falsafa ya
msingi ya kampuni , maonyesho haya huwa yanafanyika kila mwaka katika nchi
tofauti duniani kote kwa lengo la kuonyesha bidhaa na huduma zake zinazotolewa
sokoni.
Pia inakuwa kama jukwaa kwa wateja
na wadau wengine wanaotaka kuelewa kuhusu kampuni na mtindo wake wa biashara.
Dhana hii ni taswira ya juhudi za kampuni kuhamashisha mwenendo wa kiafya, na
mtindo wa maisha wenye uwiano sahihi, kwa kutilia mkazo katika afya, ustawi na
Elimu.
“Kutoka katika kozi za elimu kwa
njia ya mtandao, (online course) mpaka katika kozi za vifurushi vya sikukuu,
mpaka bidhaa za kuongeza nguvu, vyakula vya nyongeza na saa, tuna aina nyingi
mbalimbali zinazoweza kutuwezesha kutoa huduma kwa mahitaji mbalimbali. Katika
msingi wa yote haya, ni hamu yetu ya kutoa
fursa ya ‘kuishi kikamilifu”, alisema bwana Fall.
Kampuni pia inatoa fursa za
biashara kwa gharama nafuu kwa watu wanaotaka kuifanya, bila kujali kiwango
chao cha elimu.
“Tanzania ni moja kati ya masoko
yetu ya kitaalamu katika QNET na kwa kuwezesha kufanyika kwa onyesho la Expo
jijini Dar es salaam ni njia ya kurudisha kwa viongozi wetu hapa na kuwa karibu
zaidi nao.“ aliongeza.
Kama taasisi kampuni inaamini
kwamba hakuna kinachompa nguvu zaidi mtu kama uhuru wa kifedha ambao unatokana
na kufanyakazi katika sekta ya mauzo ya moja kwa moja na inaweza kuwa kazi ya
kujitosheleza kwa wale watakaoamua kuifanya fursa hii muda wote au katika muda
wa ziada.
Tofauti na biashara zingine za kawaida ambazo
zinahitaji mtaji mkubwa wa kuanzisha, rasilimali na hata uzoefu, Biashara ya
Mauzo ya Moja kwa moja inatoa biashara hii kwa gharama nafuu kwa kila mmoja
anayeta kuanza kuifanya bila kujali kiwango chao cha elimu au uzoefu.
Manufaa makubwa ya biashara ya moja
kwa moja katika masoko yanayochipukia kama Afrika Mashariki ni kwamba mtindo
huu wa biashara una athari kubwa zaidi kuliko katika masoko yaliyoendelea kwa
sababu ya athari za kifedha inayoweza kuleta kwenye maisha ya watu, kutoa fursa
za ujasiriamali kwa wote, bila kujali sifa au uzoefu, hatimae kuchangia kwa
kiasi kikubwa katika kupunguza kiwango cha umaskini katika jamii.
No comments:
Post a Comment