Na
Mwandishi Wetu
Sekta
ya michezo barani Afrika inakua kwa kasi sana. Iwe katika michezo ya riadha
(ambayo Afrika ya Mashariki na pembe ya Afrika huwa wanaongoza katika bara zima
na hata katika mashindano ya kiulimwengu kwa ujumla), au michezo mingine. Bara
la Afrika linabadilika taratibu kuwa mabingwa katika shughuli mbalimbali za
michezo ambayo mpaka hivi karibuni zimetawaliwa na nchi za ulaya na Asia.
Kwa
ujumla katika mchezo wa mpira wa miguu Afrika imeonyesha viwango vikubwa kwa
timu za kiafrika kufanya vizuri katika mashindano ya kidunia. Tunashukuru
umaarufu wa mchezo wa mpira wa miguu miongoni mwa mashabiki ndani ya Afrika na
wadhamini wapya wenye mapenzi mema wanaojitokeza, wapenzi wa michezo na wadau
mwengine.
Miongoni
mwa wale ambao wameingia katika ushirika na vyama vikubwa vitatu vya mpira wa
miguu barani Afrika ni QNET, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja yenye asili ya
Asia ambayo biashara yake iko Afrika na ambayo kwa hakika dunia nzima inaichukulia
kuwa ni miongoni mwa mashirika makubwa katika tasnia hiyo.
Mapema
mwaka huu, QNET ilisaini mkataba wa ushirikiano wa muda wa miaka miwili na
mabingwa wa ligi za vilabu vya Afrika: Ligi ya Mabingwa CAF, Ligi ya Kombe la
Shirikisho na Ligi ya Kombe la Super Cup
katika mpango wa udhamini unaolenga katika wigo mpana wa kidigitali na shughuli
ambazo zinalenga kukuza ushirikiano wa mashabiki na wawakilishi wa QNEt (IRs)
Afrika.
Akizungumzia
kuhusu udhamini huo, CEO wa QNET bwana Trevor Kuna alisema kwamba ushirikiano
huo na CAF ni uwekezaji muhimu sana kwa kampuni, ambayo unaendana na wateja
wake na jamii ya Afrika kwa ujumla. Ikiwa inawianisha bidii za kimichezo na
biashara ya QNET. Bwana Kuna alihamasisha: “Kama
mpira wa miguu, QNET inaunganisha dunia na kuhamaisha ari ya kufanya kazi kwa pamoja
kama timu miongoni mwa wawakilishi wake (IRS) na kila mmoja anayehusika katika
biashara yetu. Kufanya kazi kama timu na utendaji thabini ni mambo ambayo yako
sambamba katika mpira wa miguu na biashara ya masoko ya mtandao”
Udhamini huu pia ni kilemba kingine katika kofia ya QNET na
inaonyesha tena jitihada za kampuni ya mauzo ya moja kwa moja katika kuthamini maadili
ya michezo: Umakini, kufanya kazi kwa bidii na kuongeza bidii mpaka kiwango cha
mwisho. Ushirikiano huu unakuja kama jukumu la QNET kama mshirika rasmi wa
mauzo ya moja kwa moja wa Klabu ya Mpira wa Miguu wa Manchester City, shughuli
ambayo imeiwezesha QNET kuunganisha msisimko wa mpira wa miguu na shauku ya
mashabiki katika msisimko wa mauzo ya moja kwa moja na msukumo wa wawakilishi
(IRs) wa QNET
Aliongeza kwamba ushirikiano wa kampuni hii na CAF umepelekewa
zaidi na shauku ya kampuni hii kutengeneza fursa za ushiriki ikiwa inalenga mashabiki
wa mchezo wa mpira wa miguu katika bara la Afrika pamoja na kuandaa matamasha
ya kuangalia mechi kwaajili ya wasambazaji na IRs katika nchi mbalimbali barani
Afrika.
Ushirikiano huu pia ni ushahidi wa kuuzika kwa
mchezo wa mpira wa miguu wa Afrika kama bidhaa – jambo ambalo limehamasisha
makampuni ya kiwango cha kimataifa kama QNET kuonyesha nembo yao katika mchezo
ambao unatazamwa zaidi duniani.
QNET ina maono bora ya kibiashara katika bara la
Afrika ambayo ina endesha shughuli zake katika maeneo ya Afrika ya Magharibi na
Afrika ya Mashariki ambako kampuni ya mauzo ya moja kwa moja imetoa fursa za
ujasiriamali kwa maelfu ya watu kupitia bidhaa zake zinazoweza kubadilisha
maisha zinazotolewa kupitia mfumo wao wa biashara ya mtandao (e-commerce)
kwenda kwa wateja na IRs.
Bidhaa za kampuni zinajumuisha
pamoja na bidhaa za huduma binafsi, bidhaa za majumbani, saa, vito, safari za
mapumziko, elimu na zingine nyingi – ambazo zinauzwa kupitia ofisi za QNET na
mawakala wao walioko duniani kote, pia kutoka kwa waendeshaji walioko ndani ya
maeneo tofauti katika nchi mbalimbali.
QNET ambayo inasherehekea kutimiza
miaka 20 mwaka huu, na ambayo inajigamba kwa kukua kwake kutoka kuwa kampuni
ndogo yenye bidhaa moja kwenda kuwa kampuni yenye zaidi ya bidhaa 100 za aina
mbalimbali tofauti, inabakia kuwa imejidhatiti kutoa programu za mafunzo ya
mara kwa mara, kuhamasisha mwenendo imara wa maadili ya utendaji, kuwasaidia
wasambazaji wake kwa kuwapatia vifaa vya matangazo na vifaa vya kufanyia
biashara na kuendelea kutafuta au kutengeneza bidhaa sahihi kwaajili ya wateja wao walioko dunia nzima.
No comments:
Post a Comment