QNET KUDHAMINI WACHEZAJI CHIPUKIZI WA KIAFRIKA
KUHUDHURIA SHULE YA MPIRA WA MIGUU YA
CITY FOOTBALL ACADEMY
QNET, kampuni ya
mauzo ya moja kwa moja ambayo ni mshirika rasmi wa Timu ya mpira wa miguu ya
Manchester City, Ikiwa kama sehemu ya ahadi yake ya kuendeleza vipaji na kama
namna ya kampuni kurudisha kwa jamii, imedhamini wachezaji watatu chipukizi wa
kiafrika kuhudhuria mafunzo ya mpira wa miguu ya jijini Manchester (City
Football Language School in Manchester) .
Shule ya Lugha ya Mpira wa Miguu ya Manchester ni kozi ya wiki mbili ya
mpira wa miguu na mafunzo ya lugha ya kiingereza kwa wachezaji chipukizi
(vijana). Kozi hii ilianza tarehe 28
Julai na itakamilika tarehe 12 August mwaka 2019.
Wachezaji hao
chipukizi walichaguliwa kutoka katika mchakato wenye ushindani mkubwa nchini
Ghana, Cameroun na Ivory Coast, na ni kozi ambayo haina gharama yoyote kwa
wachezaji hawa walio chaguliwa.
Shule ya Lugha ya
Mpira wa Miguu ni kozi ya lugha ya kiingereza na mpira wa miguu yenye hamasha
kwa wachezaji chipukizi wenye umri wa kati ya miaka 12-17, ambayo inafanyika
katika viwanja vya mafunzo vilivyoko huko katika jiji la Manchester. Wachezaji chipukizi waliochaguliwa wanapata
fursa ya kupata falsafa ya mafunzo na mbinu za mpira wa miguu za manchester city
kupitia katika vipindi vya mafunzo ambavyo vinaongozwa na makocha wa mpira wa
miguu wa jiji la manchester. Vile vile
wanapata fursa ya kuendeleza uwezo na ujuzi wao wa kutumia lugha ya kiingereza
kupitia majadiliano katika vipindi vya ulimwengu wa mpira (the world of football) kutoka kwa walimu wa vituo vya mafunzo ya
lugha vya British Study Centres
Wachezaji hao
chipukizi wanajifunza na kupata mafunzo nyumbani au katika makao makuu ya
machester city katika kitovu cha campus ya Etihad, sehemu ambayo watakuwa na
nafasi ya kutumia miundombinu bora. Mafunzo ya Mpira wa miguu yenye ubunifu wa
kiwango cha juu na Mtaala wa Lugha ya Kiingereza vimeandaliwa kwa lengo la
kuhakikisha wanaongeza uwezo wa kujifunza nje na ndani ya uwanja, ikiwa inagusa
maeneo ya msingi ya maisha ya mtaalamu wa mpira wa miguu. Zaidi ya
kutambuliwa na Shule ya Lugha ya kiingereza ya British Council, kozi hii vile
vile inatambuliwa na Eaquals ambao lengo lao ni kuthibitisha kwamba viwango vya
juu katika kufundisha lugha na mafunzo vinafikiwa duniani kote.
Akiongelea
kuhusu fursa hiyo, Bwana Biram Fall; Meneja Mkuu wa QNET wa kanda ya Kusini mwa
Jangwa la Sahara alisema: "QNET inaendelea kuwekeza katika kuendeleza na
kukuza vipaji katika ngazi zote. Udhamini wa Klabu ya mpira wa miguu ya
Manchester City kama mshirika wa mauzo ya moja kwa moja ni moja kati ya
majukumu yetu katika mpira wa miguu na ari ambayo mpira huo unaambatana nao
duniani kote. Mchezo wa mpira wa miguu unaunganisha watu kutoka katika asili na
maeneo mbalimbali. Mpira wa miguu vile
vile unahamasisha kufanya kazi kwa pamoja kama timu, kuwa na ari ya timu, kufanya
kazi kwa nguvu na hamasa. Hizi ni baadhi ya tunu za msingi za QNET kama
biashara."
Katika Afrika, QNET ni mshirika wa mauzo ya
moja kwa moja Ligi ya mabingwa CAF, Kombe la Shirikisho la Total CAF na Kombe
la Total CAF Supa Cup (Total CAF
Champions League, Total CAF Confederation Cup and the Total CAF Super Cup)
QNET inaendelea kupanua uwepo wake katika sehemu mbalimbali
katika bara la Afrika, huku ikiwa inatoa fursa za ujasiriamali kwa watu na
kuwasaidia kubadilisha maisha yao kuwa bora zaidi. Mbali na ushirika katika michezo, QNET vile vile
ni kampuni ambayo imewekeza katika kuwajibika kwa jamii, kurudisha na kutoa
kwaajili ya manufaa ya jamii na jambo hili linafanyika katika maeneo yote
ambako QNET inaendesha shughuli zake.
Katika mwezi Novemba mwaka 2018, Kampuni ya QNET ilitunukiwa tuzo ya
e-Commerce CSR Company kuwa ni kampuni bora ya biashara ya mtandao kwa mwaka
huo, ambayo ilitolewa na Kituo cha Uwajibikaji wa Mashirka kwa Jamii cha Afrika
Magharibi (Centre for Corporate Social Responsibility West Africa.)
No comments:
Post a Comment