Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Amos Makalla. |
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Amos Makalla amezindua Maadhimisho ya Siku mbili ya kuzuia na kudhibiti dawa za kulevya Mnazi mmoja ambapo ametoa wito kwa Wananchi kushirikiana na Vyombo vya Udhibiti ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa wanapowabaini wauzaji na watumiaji.
RC Makalla amesema Matumizi ya dawa za kulevya yamekuwa yakileta usumbufu mkubwa kwa Taifa na familia ambapo kwa familia vijana wamekuwa wakifanya ukokozi wa fedha na kuiba Vifaa vya nyumbani ili kwenda kuuza wapate pesa ya kununulia Dawa.
Aidha RC Makalla amesema maadhimisho hayo yatafungwa siku ya kesho Juni 02 na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambapo ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi.
Pamoja na hayo RC Makalla amepongeza Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya kwa kazi kubwa na nzuri inayofanya ambapo amewahimiza kuongeza juhudi.
Hata hivyo RC Makalla ametoa wito kwa Mamlaka nyingine ikiwemo Ofisi ya mkemia Mkuu wa Serikali kutoa ushirikiano kwa Mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa ushahidi ili mashauri yaliyopo Mahakamani yapungue.
No comments:
Post a Comment