Tuesday, September 20, 2022

Viongozi wa Siasa Wakumbushwa Kuacha Kuwagawa Wananchi Kwa Maslahi yao Binafsi.

Na Vicent Macha

Wito umetolewa kwa Wanasiasa nchini kuacha tabia ya kuwagawa wananchi nabadala yake waendeleze misingi ya Aamani,Umoja na Maendeleo iliyoachwa na Muasisi wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Wito huo umetolewa leo Dar es salaam na Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba kwenye kikao cha kubadilishana Uzoefu na Ujuzi kilichoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere nakuwakutanisha wadau mbalimbali ikiwemo viongozi wa vyama vya siasa,lengo likiwa  ni kujadili misingi iliyoachwa na viongozi wa Taifa tangu kupata uhuru mwaka 1961.

Amesema kuwa viongozi wa kitaifa walifanya imani kuwa wananchi wote ni sawa ,nakwamba baada ya kupata uhuru viongozi hao  hawakuona umuhimu wa nchi kuwa huru huku wananchi wakiwa hawako huru,hivyo walihakikisha wanasimamia misingi ya Amani,Umoja na Maendeleo ili kulifanya Taifa la Tanzaia kuwa na Umoja.

"Tusiwagawe wananchi,tuhakikishe tunalinda misingi ya amani,umoja na maendeleo iliyoachwa na Viongozi wetu wa kitaifa waliopambana hadi tukapata uhuru,hivyo tunapaswa kuwa na nchi huru yenye watanzania huru."amesema Jaji Warioba.

Awali Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Joseph Butiku amesema kwamba Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi ya uhai wake amekuwa akisimamia misingi ya Amani,Umoja na Maendeleo hivyo viongozi wa vyama vya siasa hawana budi kushirikiana kwa pamoja kuondoa changamoto zinazowakwaza watanzania katika kuwaletea maendeleo.

Kwa upande wake kadhalika Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Bara Christina Mndeme amewambia waandishi wa habari kuwa mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere umewasaidia kupata mawazo ya namna yakuendeleza  misingi ya amani,Umoja na Maendeleo iliyoachwa na Hayat baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
\
                                                                   Habari Picha.
Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba akiongea na Baadhi ya Wajumbe kutoka vyama mbalimbali katika Kongamano liliandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere mapema leo Mkoani Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku akiongea katika Kongamano lililoandaliwa na Taasisi hiyo.
Baadhi ya Viongozi wa dini wakifuatilia matukio katika Kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere mapema leo mkoani Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Bara Christina Mndeme akiongea katika kongamano la kubadilishana uwezo kati ya Viongozi wa vyama mbalimbali vya Siasa na Asasi za Kijamii.
Kongamano likiendelea.




\



No comments: