Na Moshi Saidi Dsm.
Kamati ya Mdundo wa Kitaifa iliyoundwa hivi karibuni na Waziri Tamaduni Sanaa na Michezo Mohamedi Mchengrwa imepokea maoni Kutoka kwa Wadau mbalimbali wa muziki ikiwemo watayarishaji wa muziki,watunzi,watangazaji wa vyombo vya habari pamoja wasanii wa ngoma za asili lengo ni kupata vionjo vitakavyotumika kutengeneza Mdundo wa kitaifa.
Wajumbe wa Kamati ya kutafuta Mdundo wa Kitaifa wakiendelea kukusanya maoni. |
Wakitoa maoni katika Mdahalo uliofanyika Jijini Dar es salaam Mkurugenzi kikundi cha muziki (Kay wa Mapacha) Levison Kasuhuwa alisema tangu nchi imepata uhuru haijawahi kuwa na mdundo wa kulitambulisha Taifa hivyo wasanii wa muziki wameiga Midundo ya za nje kutengeneza muziki yao hivyo sasa kwakuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassani kupitia kamati iliyochaguliwa lazima ije na mdundo utakaokwenda kubadilisha taswira za watu kuondokana na kutumia Midundo isiyo ya asili yao
"Tunakubali kuwa ukoloni umetuathiri kwa kipindi kirefu kwa kuacha Tamaduni zetu kuna usemi asiyependa kwao ni mtumwa hivyo tumechoka kuwa watumwa kutumia Midundo ya kigeni Sasa ni wakati wa kuwa na mdundo wetu wa asili ambao utatutambulisha "alisema Levision
Sixmondi Mneka kutoka chama cha muziki wa Reggae dansi nchini amewasihi na kuwaomba Watanzania kuacha ushabiki wa makabila na badala yake kushirikiana Kwa pamoja kuunganisha vionjo vya makabila mbalimbali ili kutengeneza mdundo wa Taifa utakaotambulisha asili ya mtanzsnia katika mataifa mbalimbali Duniani
"Watanzania wanatabia ya kuibua jambo lakini hatufiki mwisho hivyo tufanye vitu Kwa Makubaliano ambapo naisihi kamati yenu(kamati ya Mdundo wa Taifa) kuendelea kuifanya kazi hiyo iwe endelevu kulingana na mahitaji ya muziki wetu kwasasa ili kuendelea kuulinda Utamaduni wa kitanzania kupitia Sanaa hiyo ya Burudani."amesema Mneka.
Meneja wa Sisi Tambala Bendi Bw. Kibiriti akitoa maoni yake mbele ya wajumbe wa Kamati ya kutafuta Mdundo wa Kitaifa. |
Nae Meneja wa Sisi Tambala Bendi Bw. Kibiriti Nanjuja ameshauri kuwa ngoma za asili za makabila mbalimbali zenye vionjo vya kuvutia ndizo zitumike katika kutengeneza mdundo wa Kitaifa ,nakwama Jamii isipuuzie ngoma za asili kwani ndio utambulisho halisi wa Utamaduni wa Mtanzania kupitia Sanaa hiyo .
Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya mdahalo huo Makamu Mwenyekiti kamati ya Mdundo wa asili Tanzania Masoud Masoudi ambaye ni Manju Muziki amesema kwamba zoezi la kutengeneza mdundo wa Kitaifa unatokana na nia ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amenuia kulinda Mila na Tamaduni za Mtanzania kwani zimekuwa zikisahaulika tangu Tanzania ipate uhuru..
" Tumekubali kwa maoni ya wadau ambao wanaonekana wanakubaliana na dhana nzima ya Mdundo wa Taifa,wamekubali kwamba mdundo wa Taifa ni Muhimu,hivyo kuelewa mdundo wa Taifa ni hatua Moja kubwa sana" Amesema Masoud ambaye pia ni Mtangazaji wa TBC
No comments:
Post a Comment