Ameandika @exaud_msaka_habari1
Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kuna tangazo lilitoka Bodi ya Ithibati @ithibatitz kwenda kwa wanahabari hasa wale waliokuwa wanataka kugombea nafasi mbalimbali
Tangazo lile lilkelekeza kuwa kama unataka kuwania nafasi za kisiasa basi pumzika kwanza uandishi wa habari ili usiwachanganye watu na uwe huru kufanya siasa vizuri. Jambo jema sana
Kwa fikra zangu nadhani tangazo lililenga kuepuka kuwa na waandishi wa habari ambao wana mapenzi na siasa za vyama, yani ni mfia chama cha siasa
Sasa leo nimepata mtanzuko kidogo, inakuaje mwandishi wa habari ambaye ameshashinda nafasi ya kisiasa na anaitumikia anarudi studio akiwa na cheo chake na Chama chake alafu anaendelea kuhudumu kama mtangazaji ?
Itawezekana kweli apokee mshahara wake wa udiwani alafu aje aitendee haki nafasi yake ya utangazaji ?
Studio akija mtu ambaye ni hasimu wa chama chake atamhoji kama mtangazaji au atamhoji kama diwani kutoka chama chake ?
Na Je Akija mgeni kama huyo atakuwa huru kweli kuhojiwa na mtu ambaye anajua kabisa hawezi kumsikilza maana kuna maslahi anayalinda na ndio wanamlipa ?
Au mimi kuna mahali sjaelewa nisaidiwe ila kiuhalisia kwangu ina ukakasi kidogo.

No comments:
Post a Comment