Thursday, February 9, 2017

Mahakama yatupilia mbali pingamizi la Lema

Arusha. Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, imetupa pingamizi la mawakili wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema la kuitaka isisikilize kesi ya kuhamasisha maandamano ya Ukuta, bali kwanza ifikishwe Mahakama ya Katiba.


Lema, ambaye ni mbunge kupitia Chadema, anakabiliwa na kesi hiyo akidaiwa kuhamasisha maandamano hayo ya chama chake yaliyokuwa yamepangwa kufanyika Septemba Mosi, mwaka jana.

Askofu Gwajima Alipuka Dar muda Huu,amaliza na kuelekea Polisi mchana huu

Gwajima:- 
Namuomba Rais ambadilishie Kazi Makonda, hii ya Ukuu wa Mkoa kutawala na kuongoza hata watu usiowapenda imemshinda. Sisemi amfukuze hapana nasema ambadilishie Kazi.

Gwajima : Makonda ana chuki na wivu na mimi

Gwajima : alikasirika hata niliposhuka na helkopta yangu siku ya mechi ya viongozi wa dini na wabunge dodoma.

Jinsi Manji alivyowasili Polisi Central Leo

Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji amefika kituo cha Polisi cha Kati leo saa 4:54 asubuhi kwa ajili ya mahojiano baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaka afike polisi.

Manji amefika leo badala ya kesho ambapo yeye na wengine 64 walitakiwa kufika kituoni hapo.

Manji ambaye pia ni Mwenyekitu wa Klabu ya Yanga jana alizungumza na waandishi wa habari na kusema hatoweza kufika kituoni hapo siku ya Ijumaa.


Amewasili leo na gari aina ya Range Rover rangi nyeusi .

Manji amefika kituoni hapo akiwa na wanasheria wake 8 ambapo wanasheria 6 ni raia wa Tanzania na wanasheria wawili ni raia wa Uingereza.

Aidha, mashabiki wa Yanga wamejitokeza kwa wingi kituoni hapo kumuunga mkono kiongozi wao.

Mbali na Manji, wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni Pamoja na Fremaan Mbowe, Askofu Josephat Gwajima, Iddi Azan. 

Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Azungumza na Waandishi wa Habari Kukamilika kwa Maandalizi ya Tamasha Linaloaza Leo Kwa Uzinduzi wa Maandamano Hadi Ngome Kongwe Zanzibar.

Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza na waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali vya Tanzania na Nje wakati wa kutowa kwa taarifa kwa kukamilika kwa matayarisho ya Tamasha hilo linaloaza leo katika viwanja vya ngome kongwe mji mkongwe wa Zanzibar kwa kutowa burudani ya muziki wa kiasili wa Afrika na kuwashirikisha Wasanii zaidi ya 400 kutoka sehemu mbalimbali ya Afrika na kutowa shukrani kwa Wadhamini waliojitokeza kutowa udhamini wao kwa hali na Mali wakiwemo Kampuni ya Simu ya Zantel, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip Malindi Zanzibar.   
Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar DJ Yussuf Mahmoud, akizungumza wakati wa mkutano huo wa waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip Malindi Zanzibar na kuwataja washiriki watakaopamba Tamasha Wasanii kutoka sehemu mbalimbali wamethibitisha kushiriki na tayari wako Zanzibar kwa ajili ya Tamasha hilo litakaloazia kwa maandamano maalumu yatakayowashirikisha washanii hao yataazia katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani na kupita katika mitaa mbalimbali ya mji wa Unguja hadi kumalizikia katika viwanja vya Mambo Club Ngome Kongwe Zanzibar.   

Wednesday, February 8, 2017

SOMA MAGAZETI YOTE YA LEO HAPA ALHAMIS FEB 9,2017

Magazetini leo Alhamis February 9 2017 

MANJI KUMBURUZA MAKONDA MAHAKAMANI.





Baadhi ya Nukuu kutoka katika mkutano wake na wanahabari baada tu ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda Kumtaja katika Orodha ya wanaohitajika Kufika Kituo cha pilisi kwa Tuhuma za Madawa ya kulevya.

Kauli ya kwanza ya Mh Freman Mbowe leo

Image may contain: text

MFUMUKO WA BEI WA MWEZI JANUARI 2017 UMEONGEZEKA KWA ASILIMIA 0.8

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa kuhusu mfumuko wa bei wa mwezi Januari 2017 jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Idara ya Takwimu za Ajira na Bei, Ruth Minja.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakiwa kazini.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

RC MAKONDA AITWA BUNGENI,HATARINI KUVULIWA WATHIFA WAKE

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma limeandika barua kwenda kwa Kamati ya Maadili na Uongozi wa Umma kuitaka kamati hiyo kumtaka mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda kwenda Bungeni na kuomba radhi juu ya Majibu aliyoyatoa kuhusu tuhuma za mwenendo wa anavyoshughulikia swala la dawa za kulevya.

Wanawake wajasiriamali wa Kisiwa cha Zanzibar wapatiwa mafunzo ya ujasiliamali na Benki ya KCB Tanzania.

Ofisa Mawasiliano ya Umma wa Benki ya KCB Tanzania Aziza Mkwizu, (aliyekaa kulia), Ofisa biashara wa benki ya KCB Tawi la Stone Town Zanzibar Lutfy Said (aliyekaa wapili kulia), Ofisa biashara wa Tawi la Stone Town Zanzibar wa Benki ya KCB, Rashid Mshana (aliyekaa wapili kushoto) na Ofisa mawasiliano ya Umma wa Benki hiyo Margaret Makere (aliyekaa watatu kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanawake wajasiriamali wa Zanzibar.

Ofisa Biashara wa Tawi la Stone Town Zanzibar wa Benki ya KCB Tanzania, Rashid Mshana akimkabidhi mmoja wa wanawake wajasiriamali Bi. Rayyan Khelef cheti cha kushiriki semina ya mafunzo hayo. 

Meneja wa Tawi la Stone Town Zanzibar wa Benki ya KCB Tanzania Iddy Mwacha, akizungumza na wanawake wajasiriamali waliohudhuria semina ya mafunzo ya siku tatu kwa ajiri ya wanawake wajasiriamali inayoitwa 2JIAJIRI iliyoandaliwa na benki hiyo Kisiwani Zanzibar.

Mwalimu wa ujasiriamali wa Kituo cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC) Seif Abdullah akizungumza na wanawake wajasiriamali wa Zanzibar.

Mkurugenzi msaidizi wa Kituo cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC) Daniel Mghwira akitoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wajasiriamali Kisiwani Zanzibar.

Mtikisiko---Mbowe,Gwajima,Manji,Iddi azan watajwa na makonda madawa ya kulevya,wapo pia vigogo 60 wapya

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Palu makonda ametaka majina mapya 60 ambayo kwa namna moja ama nyingine yanahusishwa na Madawa ya kulevya Tanzania yakiwemo majina makubwa nchini.

Amesema kuwa majina hayo ni watu ambao wengine wanatumia,wengine wanauza na wengine wana Taarifa nyingi kuhusu uuzwaji wa madawa ya kulevya nchini

Mh Makonda pamoja na mambo mengine amewataka watanzania kutulia kwani Picha ndio linanoga na kama kuna mtanzania anabeza jitihada zake atashangaa atakaposkia Dar es salaam hakuna madawa ya kulevya Tena.
Wafuatao waonane na Makonda pale central polisi ijumaa hii
Orodha ni ndefu ila hawa wamenivutia kuwaandika hapa 
1. Sleep way Mmiliki
2. Yatch club
3. Saleh MMI
4. Mwinyi machapta
5. Rose 
6. Kiboko
7. Halfin
8. Iddi azan
9. Mch gwajima
10. Mbowe
11. Chizenga
12. Masanga
13. Ben mfundo
14. Yusuf manji
Image may contain: one or more people

Tuesday, February 7, 2017