Sunday, October 8, 2017

LEMA AUNGANA NA JUKWAA LA KATIBA KUDAI KATIBA MPYA NA KUSEMA MABADILIKO YA BARAZA LA MAWAZIRI SIYO DAWA

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kuwa baraza jipya la mawaziri lililotangazwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli halina jipya kwani sura zilizobaki ni zile zile.
         Image result for MBUNGE LEMA
Ameyasema kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Twitter, ambapo amesema kuwa ameona mabadiliko ya baraza la Rais Magufuli lakini bado fikra ni zile zile na watu ni wale wale na kudai katiba mpya ndio suluhisho la vyote.

“Nimeona Mabadiliko ya baraza la JPM. Watu ni wale wale, fikra zile zile. Katiba Mpya yenye fikra mpya ndio tumaini kwa mabadiliko sahihi ya nchi na watanzania kwa ujumla,”ameandika Lema

Saturday, October 7, 2017

Kijana Huyu ameahidi kumuua Lissu akirejea matibabuni-soma Hii

Kijana alyeahidi kummaliza Lissu akirudi kutoka kwenye matibabu

Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Uratibu wa Kanda, Benson Kigaila amefunguka na kulilalamikia jeshi la polisi kushindwa kumkamata ki...
 Yatakayo jadiliwa kikao cha CCM kesho Zanzibar
 Kamanda wa Polisi Geita amekuja na taarifa hii kukamatwa kwa mbunge Msukuma
 Taarifa ya Kamanda Mambosasa waliokamatwa mkutano wa kumuombea Lissu
Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Uratibu wa Kanda, Benson Kigaila amefunguka na kulilalamikia jeshi la polisi kushindwa kumkamata kijana ambaye anaendelea kuandika vitisho kwenye mtandao wa jamii juu ya Tundu Lissu. 
 
Kigaila amesema kuwa kabla ya Mbunge wa Singida Mashariki kupigwa risasi Septemba 7, 2017 mjini Dodoma huyo kijana kupitia mitandao ya kijamii aliomba apewe ruhusa ya kumuuwa Lissu kwa mikono yake mwenyewe. Kigaila amedai kuwa kijana huyo hivi sasa ameendelea kuandika ujumbe mbaya zaidi kupitia mitandao hiyo hiyo ya jamii bila ya polisi kumchukulia hatua zozote zile. 

"Sasa huyo kijana anaandika vibaya zaidi anasema 'Anasikitika sana kwa mtu aliyefanya hilo tukio la kumpiga Lissu anasema alitegemea asikie Lissu amekufa siyo kwamba Lissu amejeruhiwa na anasema wanamsubiri Lissu atakaporudi Tanzania mara hii hawatafanya kosa, wanasema walifanya kosa Dodoma sasa huyu mtu awe ni yeye kweli au si yeye aliyefanya tukio hilo, awe ni mwendawazimu au si mwendawazimu tulitegemea polisi wawe wameshamkamata wapo naye wanamuuliza haya anayosema ni kwa sababu gani lakini polisi halimuoni huyo kijana" alisema Kigaila 

Aidha Kigaila amesema kuwa kitendo cha polisi kutomchukulia hatua kijana huyo kinazidi kuwapa mashaka kuwa huenda wanamtambua huyo kijana lakini hawataki kumkamata kwa sababu zao binafsi.

Zitto Kabwe Atoa Neno Baraza Jipya La Mawaziri

Zitto Kabwe Atoa Neno Baraza Jipya La Mawaziri

Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT -Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, ametoa maoni yake juu ya Baraza jipya la Mawaziri lililofanyiwa mabadiliko hii leo, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Kwenye ukurasa wake wa Facebook Zitto Kabwe ameandika ujumbe akiwapongeza Mawaziri hao walioteuliwa ambao wengi wao ni vijana, huku akiwataka kuchapa kazi kwa bidii.

"Uteuzi wa vijana kushika nafasi za juu ni hatua nzuri, naona vijana wengi wamepewa majukumu makubwa, ninawaombea watekeleze majukumu kwa weledi mkubwa", ameandika Zitto Kabwe.

Leo Rais Magufuli amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na kuongeza wizara mpya mbili, baada ya kuzivunja baadhi ya wizara ambazo zilikuwa na vitengo vingi.





Tigo yatoa zawadi kwa washindi wa promosheni ya 'nunua simu na ushinde

Meneja Mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Woinde Shisael (kulia) akimkabidhi zawadi ya seti ya televisheni  Amina Nachunga, mojawapo ya washindi wa promosheni ya nunua simu na ushinde  jijini Dar es Salaam leo. Jumla ya washindi sita wamejinyakulia zawadi za luninga na pikipiki katika promosheni hiyo inayoendelea, ambapo Tigo inawazawadia wateja wake wanaonunua simu aina ya Tecno S1 na Tecno R6 kutoka kwa maduka ya Tigo nchini kote.

Meneja Mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Woinde Shisael (kulia) akimkabidhi zawadi ya pikipiki Amina Khalfan, mojawapo ya washindi wa promosheni ya nunua simu na ushinde  jijini Dar es Salaam leo. Jumla ya washindi sita wamejinyakulia zawadi za luninga na pikipiki katika promosheni hiyo inayoendelea, ambapo Tigo inawazawadia wateja wake wanaonunua simu aina ya Tecno S1 na Tecno R6 kutoka kwa maduka ya Tigo nchini kote

Wateja wa Tigo mkoani Njombe wafurahia huduma zitolewazo na Tigo msimu huu wa Fiesta

Mtoa huduma wa duka la Tigo mkoani Njombe, Vaileth Burton akitoa huduma kwa wateja waliofika dukani leo hapo kupata huduma mbalimbali msimu huu wa Tigo fiesta 2017 ambapo bidhaa za Tigo zinapatikana kwa bei nafuu.

Mtoa huduma wa duka la Tigo mkoani Njombe, Israel Joseph akitoa huduma kwa wateja waliofika dukani leo hapo kupata huduma mbalimbali msimu huu wa Tigo fiesta 2017 ambapo bidhaa za Tigo zinapatikana kwa bei nafuu.


Baadhi ya wateja wakipata huduma mbalimbali ikiwemo kujipatia tiketi za Tigo Fiesta mkoani Njombe

MAWAZILI WALIOTOSWA NA JPM KATIKA MABADILIKO YA BARAZA LAKE JIPYA

Rais John Magufuli amefanya mabadiliko ya baraza la mawaziri kwa kuwatema mawaziri wanne waliokuwepo kwenye baraza la awali.
Image result for MAGUFULI
Mawaziri walioachwa ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na nafasi yake kuchukuliwa na Hamis Kigwangwala aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Afya.

Mwingine aliyeachwa ni aliyekuwa Waziri Maji na Umwagiliaji,  Mhandisi Gerson Lwenge ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Katavi,  Mhandisi Issack Kamwele aliyekuwa naibu waziri wa wizara hiyo.

Panga hilo limempitia pia aliyekuwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Juliana Shonza.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani naye ametupwa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga.

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kufanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri tangu aingie madarakani.

ALICHOKISEMA MBOWE BAADA YA JPM KUFANYA MABADILIKO KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI

Babati. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amepongeza kitendo cha Rais John Magufuli kuitenganisha Wizara ya Nishati na Madini kwa kuwa kwa zaidi ya miaka saba kambi hiyo ilikuwa inaishauri Serikali kufanya hivyo.



Mbowe amesema hayo leo Jumamosi kwenye mazishi ya marehemu Philip Gekul, baba mzazi wa Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul yaliyofanyika kata ya Dareda.

Amesema kwa mujibu wa kumbukumbu za Bunge zinaonyesha kuwa kambi rasmi ya upinzani ilikuwa inashauri wizara hiyo itenganishwe lakini ushauri wao haukufanyiwa kazi.

"Wizara ya Nishati na Madini ni wizara nyeti mno na mara nyingi tumekuwa tukiishauri Serikali iitenganishe wizara hiyo kwani ni kubwa na nyeti ila sasa wameona ushauri wetu unafaa na kuzitenganisha," amesema Mbowe.

Amesema suala siyo nani anafaa kuwa waziri na nani hafai kuwa waziri au ukubwa wa wizara ila suala ni kuona namna gani ya kuendesha Serikali ya Awamu ya Tano.


"Magufuli ajitafakari namna anavyoendesha Serikali kwani matakwa ya viongozi ndiyo yanakuwa maelekezo ya kuendesha nchi na hata mawaziri wanafanya kazi kwa matakwa ya mtu," amesema Mbowe

MAANDAMANO MAKUBWA "YA AMANI" YAJA TANZANIA,NI KUDAI KATIBA MPYA,

Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Katiba nchini, (JUKATA) Hebron Mwakagenda  akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu  maandamano ya kudai katiba mpya.

Wakati Sintofahamu kuhusu katiba Mpya nchini Tanzania ikiendelea kuzidi huku Utawala wa awamu ya Tano ukiwa Kimya kuhusu swala hilo,Harakati zilizoanzishwa majuma kadhaa yaliyopita hatimaye yameanza kuzua mambo baada ya Jukwaa la Katiba Tanzania JUKATA kutangaza maandamano makubwa kudai kurejeshwa mchakato wa Katiba mpya.

Mchakato wa Katiba nchini ulisimama kupisha uchaguzi mkuu mwaka 2015 na Tangu kuingia kwa serikali ya awamu ya Tano kumekuwa kimya huku wanaharakati wakinongona chinichini kuhusu hatma ya mchakato huo ambao unatajwa kuligharimu taifa pesa nyingi kipindi cha ukusanywaji wa maoni yake.

Wakati hayo yakitokea Leo Jukwaa la Katiba Tanzania limetangaza Rasmi azma yake ya kufanya maandamano ya nchi nzima kuishinikiza serikali Kurejesha mchakato wa Katiba mpya.

Akitangaza Maandamano hayo Leo jijini Dar es salaam wakati Wa mkutano na waandishi Wa Habari,Mkurugenzi Mtendaji Wa (JUKATA),Hebron Mwakagenda amesema baada ya mkutano Mkuu Jukwaa hilo uliofanyika mkoani Dodoma mwisho Wa wiki iliyopita wamezimia kifanya maandamano nchi mzima yenye lengo la kudai katiba mpya.

 "Tumeazimia kufanya maandamano katika ngazi ya  kitaifa yatafanyika Jijini Dar es Salaam,yakianzia ofisi za JUKUTA  hapa Mwenge Tarehe 31 mwezi huu wa kumi Saa nne asubuhi na yatahitimishwa katika viwanja vya mnazi mmoja" amesema Mwakagenda.

Mwakagenda amesema Jukwaa la hilo ni teyari limeshaliandikia barua Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam kutoa taarifa juu ya kusudia kufanya maandamano hayo 

"Maandamano haya  ni ya amani ili kurudisha hamasa ya wananchi kuendelea kushiriki kwenye michakato ya kidemokrasia  hapa nchini"

"Kwa upekee na heshima kubwa sana JUKATA pia tumemwandikia barua Rais Magufuli kumwomba ayapokee maandamano yetu ya amani katika viwanja vya Mnazi Mmoja" Amongeza Kusema Mwakagenda.

Hata hivyo,Mwakagenda amesema kuwa maandamano hayo kwa upande Wa Mikoa  mingine nje ya Dar Maandamano ambapo yatafanyika kila wilaya.

Pamoja na hayo JUKATA wamesema wanaamini watapata ushiriano Wa kutosha Wa Jeshi la Polisi ili maandamano hayo yafanyike kwa amani.

Friday, October 6, 2017

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI OKTOBA 7,2017

Magazetini leo Jumamosi October 7,2017

TGNP MTANDAO YAWAPA TUZO ZA HESHIMA MADEREVA WA TRENI WANAWAKE

Wanawake kote nchini wametakiwa kuwa na ujasiri wa kupingana na mfumo dume kwa kufanya kazi ambazo zinafanywa na wanaume kwani hakuna ugumu katika kazi yoyote endapo utaipenda na utakuwa na nia ya kuifanya kazi hiyo.
Afisa habari wa TGNP Mtandao Bi. Monica John kulia akimkabidhi zawadi ya tuzo ya heshima Bi. Theresia Bernard kwa kuwa mwanamke pekee wa pili kuendesha treni nchini Tanzania
Hayo yamesemwa mapema leo na Theresia Bernad Mahagatira ambae ni dereva wa pili katika historia ya nchi yetu kuendesha treni, walipokuwa wakikabidhiwa tuzo za heshima yeye pamoja na Ritha Chibombo kwa kuwa wanawake pekee kufanya kazi hiyo kwa muda mrefu.

Wanawake hao wamepokea tuzo hizo mapema leo jijini Dar es salaam walizokabidhiwa na Afisa habari wa TGNP Mtandao Bi. Monica John makao makuu ya shirika la reli la Tazara ikiwa ni katika mpango wa kuendelea kuenzi michango ya wanawake waliofanya mambo makubwa katika nchi yetu.
Bi. Theresia Bernard akionyesha Tuzo yake ya heshima juu baada ya kukabidhiwa na afisa habari wa TGNP Mtandao 
Tuzo hizo zimetolewa kwa Bi. Theresia Bernad kwa kuwa kinara kwa kuendesha treni kwa zaidi ya miaka 14 toka mwaka 1982 mapaka 1996 akiwa ni dereva, na Bi. Ritha Chibombo Mduma yeye akiwa ameendesha treni kwa zaidi ya miaka 9 toka 2006 mpaka sasa akiwa bado dereva wa treni hilo.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa kwa tuzo hizo Bi. Theresia alisema kuwa wao walipanza walikuwa wanne kulikuwa na wakwanza ambaye yeye alishindwa na wapili ni yeye na yupo mpaka sasa hivyo anahesabiwa kuwa ni wakwanza baada ya wa kwanza kushindwa na wengine wawili waliobaki kufariki dunia.
Afisa habari wa Mtandao wa Jinsia Tanzania Monica John kulia akimkabidhi tuzo ya heshima Bi. Ritha Chibombo Mduma kwa kuwa ni miongoni mwa madereva wachache wanawake wa treni 
Aidha Bi. Theresia aliendelea kwa kusema kuwa kwa sasa yeye ni regional controller na siyo dereva hivyo uendesha mara moja moja sana majukumu yake ni kuhakikisha kuwa treni zinakwenda ama kufika kwa wakati, kuwa na mawasiliano mazuri na vituo vingine ili kuhakikisha usalama wa chombo na abiria.

Alipenda kusisitiza kwa kusema kuwa changamoto kila sehemu zipo ila sio za kuwafanya wasichana kuiongoapa fani hiyo ya kuendesha treni na miongoni mwa changamoto hizo ni kukosa usingizi kwani muda mwingi unautumia kufanya kazi lakini pia kupata ajari pamoja na kuwa mbali na familia yako kwa kipindi kirefu hivyo watoto kukosa malezi ya mama.
Tuzo zilizotolewa mapema leo ofisi za Tazara jijini Dar es salaam
Na mwisho alipenda kuwashauri wanawake kujishughulisha na shughuli zote na kuachana na dhana ya kwamba hizi ni kazi za wanaume kwani kama yeye sasa amekuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa kuwa watu wengi wanamshangaa kwa kumuona akiendesha chombo hicho na wengine utamani kuwa kama yeye na kuwasihi wanawake kuwa na uthubutu.


MOBETO KUMBURUZA DIAMOND MAHAKAMANI

Mwanamuziki Diamond Platnumz amepelekewa wito wa kuitwa Mahakama ya Watoto na mzazi mwenzake, Hamisa Mobeto kwa madai ya kushindwa kumuomba radhi na kutoa matunzo ya mtoto.Image result for DIAMOND & AMISA
Wito huo wa Diamond umewasilishwa na mawakili wa Mobeto, Abdullah Zulu na Walter Godluck kutoka Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys.

Katika wito huo Diamond Platnumz anadaiwa kumdhalilisha na kutompa matumizi ya mtoto kwa takribani miezi miwili.

Wakili Zulu amesems leo Alhamisi amesema mteja wao Hamisa Mobeto alimtumia Diamond notisi ya kumuomba radhi na kumtaka apeleke matunzo ya mtoto ndani ya siku saba.

“Baada ya kuona kimya tulipeleka kesi katika Mahakama ya Kisutu upande wa watoto  (The Juvenile Court Of Dar es Salaam) na leo(Alhamisi) tumepewa barua ya wito na tayari mwanasheria wa mwanamuziki huyo ameipokea,” amesema.

Zulu amesema kesi hiyo itaanza kusikilizwa Oktoba 30, mwaka huu.

MSIGWA AMJIBU IGP SIRRO SAKATA LA DEREVA WA LISSU

Baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kumtaka kwa mara nyingine dereva wa Mbunge Tundu Lissu, Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa amemjibu Mkuu huyo wa Jeshi kwamba kutangaza hadharani kumtaka dereva huyo ni kinyume na
Image result for MSIGWA
Msigwa amefunguka hayo ikiwa ni siku moja baada ya IGP Sirro kutangaza akiwa Mtwara kwamba dereva huyo ndiye ambaye anakwamisha upelelezi wa shambulio la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Mh. Msigwa amesema kwamba anaamini dereva wa Lissu anastahili kuhojiwa lakini pia kutokana na hali ya usalama wa maisha yake ilikuwa lazima apelekwe nje ya mipaka kutokana na aina ya tukio na siyo kuitwa polisi siku ya pili kwa kutumia vyombo vya habari kwani ni kumuweka pia hatarini dereva huyo.

"Naendelea kuamini dereva wa Tundu Lissu ambae ni 'first physical witness' lazima atahojiwa.., na lazima atatoa ushirikiano wake kama ambavyo alijitahidi kumsaidia Lissu kabla na baada ya kupigwa risasi.. hivyo lazima atatoa ushirikiano wake, kwa uhitaji huu wa polisi, mnaonesha umma kwamba dereva wa Lissu ni mtuhumiwa mkuu kwenye issue hii" - Msigwa.

Ameongeza kwamba "Dereva wa Tundu Antiphas Mughwai Lissu anaitwa Simon Mohammed Bakari yuko Nairobi kwa sasa, porojo za awali kwamba ametoweka na hataki kuonekana ni ujinga wa kupuuzwa, yuko Nairobi akiendelea na huduma za kisaikolojia, yupo kwenye mikono salama. Alishuhudia tukio na kuokoka kimiujiza.., kutokana na hali ya usalama wa maisha yake ilikuwa lazima apelekwe nje ya mipaka...jamaa walitaka kuondoa uhai wa wote wawili..., Mungu ni mwema sana.., siku zote na hata milele.., they survived to tell the tale" alisema Msigwa 

Mbali na hayo Mbunge Msigwa ameendelea kufunguka kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba "Tundu Lissu akipata nafuu na kurejea kwenye hali  yake nae atahojiwa.., ndivyo ilivyo.., na ulimwenguni kote kuwa uchunguzi wa matukio ya kihalifu  hatua zinafanana. Lissu yupo hai na atasema yote.. atamtaja kama dereva ni mhusika. Acheni kufinyanga hili suala..

Aidha Msigwa amesema kwamba dereva wa Lissu alistahili kupatiwa ulinzi kutokana na tukio la shambulio la bosi wake aliloshuhudia" Msigwa amefafanua.

"Huyu dereva alipaswa kupewa ulinzi na usalama wa maisha yake.., pia kwa sababu ameshuhudia tukio la mtu wake wa karibu.., hakuna sababu za kwanini aitwe siku ya pili baada ya tukio kubwa la uhalifu wa maisha ya binadamu kwa kupitia vyombo vya habari. Sikutaka kuamini kama angelitoa ushirikiano wa kutosha kwa nyakati zile.., labda sasa anaweza. Tusitumie vyombo vya habari kuitana kwenye upelelezi wa polisi na kutaja yupi anatakiwa na yupi ameachiwa., bado tension ni kubwa sana kwenye jamii" Msigwa.

GODBLESS LEMA AMJIBU IGP SIRRO

Mbunge  Godbless Lema amefunguka na kusema maneno aliyosema IGP Sirro jana kuhusu dereva wa Lissu ni dhihaka kubwa kwa ndugu wa Lissu, wanachama wa CHADEMA na hata viongozi wa chama hicho na kusema hakustahili kusema maneno yale kama IGP. 
Image result for godbless lema
Lema amesema hayo baada ya IGP Sirro kusikika katika baadhi ya vyombo vya habari akiwa Mtwara akisema kuwa dereva wa Tundu Lissu ndiyo anachelesha uchunguzi wa sakati hilo hivyo aliomba arudi ili kulisaidia jeshi la polisi kutoa taarifa ili kufanikisha upelelezi wa sakata la kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu. 

"Kamanda Sirro amesikika akiwa Mtwara akisema jeshi la polisi linamuhitaji dereva wa Tundu Lissu kwa ajili ya kukamilisha mahojiano ya upelelezi na kwamba tunasema au CHADEMA inasema anaumwa wakati dereva akionekana akipiga picha anang'ara kabisa, hii ni lugha ya mzaa na lugha ya kadhia hasa kwa familia na sisi wanachama wenzake na Tundu Lissu na hasa kwa dereva mwenyewe ambaye alishuhudia na kusikia milio ya risasi zaidi ya 30 na leo si tu kwamba anatatizo la kisaikolojia kwake binafsi lakini amuona boss wake, kaka yake na mzee wake wa siku nyingi akiwa kitandani akisubiri kudra za Mwenyezi Mungu kuweza kuishi hivyo hii ni kauli ya mdhaa ni kauli ambayo haikupaswa kutolewa na IGP" alisema Lema 

Mbali na hilo Lema amelitaka jeshi la polisi kukamilisha kwanza upelelezi wa matukio ya kupotea kwa Msaidizi wa Mbowe, Ben Sanane kifo Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo ambao wao hawakuwa hata na madereva lakini mpaka sasa jeshi la polisi limeshindwa kutoa ripoti juu ya matukio hayo. 

"Leo wanaposema dereva wa Lissu anachelewesha upelelezi kukamilika siyo kweli kwa sababu Ben Sanane hakuwa na dereva na mpaka leo hatujawahi kuona mchakato wa suala lake kukamilika, Mawazo pia hakuwa na dereva lakini mpaka leo tunaushuhuda kwamba waliopo jela walishawahi kugoma barabarani na kusema wao hawakuwa wahusika wa tukio lile, wapo watu wengi wa CHADEMA wameuwawa lakini hawakuwa na madereva kama wameshindwa kukamilisha kwanza upelelezi huo ni mtake kwanza Sirro akamilishe kwa haraka suala la Ben Sanane ambalo kimsingi wamekataa kufanya utafiti wake, tunajua serikali haiwezi kufanya uchunguzi wa tukio la Lissu kwa sababu wanajua nini kimefanyika" alisema Lema