Wednesday, January 3, 2018
CCM WILAYA YA GEITA WALAANI JESHI LA ZIMA MOTO KUWATOZA FEDHA KUBWA WACHIMBAJI BILA YA KUWAPATIA RISITI
| Baadhi ya wachimbaji wa kijiji na kata ya Rwamgasa wakiendelea na kazi ya uchanjuaji wa madini ya dhahabu. |
| Moja kati ya wamiliki wa mialo ya uchenjuaji wa madini ya dhahabu akionesha risti ambayo sio ya EFD ambayo wamekuwa wakipatiwa baada ya kununua kifaa cha kuzimia moto. |
| Eneo la kuchenjulia dhahabu likiwa limefungwa na jeshi la zima moto na uokoaji. |
| Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Wilayani Geita,Barnabas Mapande akikagua moja kati ya mtungi wa kuzimia moto wakati alipofika kuzungumza na kusikiliza changamoto za wachimbaji. |
| Kifaa cha kuzimia moto kikiwa kwenye eneo la kuchenjulia dhahabu. |
Na,Joel Maduka,Geita.
Chama cha
mapinduzi Wilayani Geita kimelaani kitendo cha jeshi la zima moto na uokoaji
kuwatoza gharama kubwa bila ya kuwapa
stakabadhi za serikali baadhi ya
wachimbaji wadogo wa dhahabu kwenye kijiji cha Lwamgasa huku wakifungiwa shughuli za uchenjuaji madini hayo kutokana na baadhi
yao kugoma kununua kifaa cha kuzimia moto.
Akizungumza
baada ya kufika kwenye machimbo hayo na kujionea namna ambavyo wachimbaji hao
wamefungiwa shughuli zao Katibu Mwenezi wa CCM Wilayani Humo Bw Jonatham
Masele,amesema CCM imesikitishwa na jeshi la zima moto kuwatoza Sh Lakini moja na elfu ishirini.
“Kiukweli
sisi kama chama tumesikitishwa sanaa na kitendo cha jeshi la zima moto kuuza
kwa bei kubwa bila ya kutoa risti mitungi hii ya gesi ya kuzimia moto na jambo
jingine kuwafungia watu shughuli zao bila ya kuwapa elimu jambo hili sio nzuri
tunaomba wajitahidi kuwaelimisha kwanza awa watu nasio kujichukulia hatua ya
kuwafungia”Alisema Masele.
Bw Lehamu
Lugiko , Mzee Mathew Kajoro na
Mwananyanzara Hamis wameelezea sababu kubwa ambayo imeendelea kuwapa mashaka
wachimbaji kuwa ni kuuziwa mitungi ya kuzimia moto bila ya kupewa Elimu ambayo
itawasaidia kupambana na majanga ya moto huku wakisikitishwa na kitendo cha
kufungiwa kwa shughuli zao.
Mkuu wa
Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoani
Geita Bw Elisa Mgisha amesema wao sio wasambazaji kwani kuna watu ambao ni
mawakala na kwamba suala la risti za EFD inatokana na wafanyabiashara wenyewe
na kuhusu kuuziwa kwa bei kubwa ni kwamba wao wanapotoa kibari cha mawakala
yeye ndiye mwenye jukumu la kupanga bei ya kuuza mtungi vile ambavyo anaonelea.
Mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Geita Bw Barnabas Mapande amemtaka mkuu wa jeshi la zima moto
kushughulikia tatizo hilo na kuacha kuendelea kuwakandamiza wananchi na wafanyabiashara
pindi wanapokuwa kwenye shughuli zao za kujitafutia kipato.
Monday, January 1, 2018
IJUE MIKAKATI MIPYA ILIYOUNDWA NA CHADEMA KWA MWAKA 2018
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza mikakati ya chama chake kwa mwaka 2018, akisema kitapigania upatikanaji wa Katiba Mpya ikiwemo uwepo wa tume huru ya uchaguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam jana, Mbowe alisema licha ya kutambua kuwa mwaka 2017 ulikuwa mgumu kwa vyama vya upinzani, mwaka huu watahakikisha wanapambana ili kurudisha mchakato wa Katiba mpya.
“Jambo kubwa tunalopigania hapa ni kuwa na tume huru ya uchaguzi,” alisema.
Moja ya mambo yanayolalamikiwa kuwa chombo hicho hakina uhuru ni uteuzi wa viongozi wake kufanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, na muundo wake.
Kwa sasa, NEC ina wafanyakazi wa ofisi ya makao makuu tu, wakati katika ngazi za wilaya ambako uchaguzi huratibiwa, inategemea wakurugenzi wa halmashauri ambao pia ni wateule wa Rais na si waajiriwa wa chombo hicho.|
Katika mkutano wa jana, Mbowe alisema suala la ukosefu wa fedha ili kuendelea na mchakato huo halina mashiko kwa kuwa kinachohitajika ni dhamira ya dhati.
“Tumeshatumia fedha nyingi hadi kufikia mchakato wa Katiba mpya ulipoishia, kinachohitajika ni dhamira ya dhati ya kupata Katiba Mpya. Rais anatakiwa kutambua kuwa Katiba ni matakwa ya wananchi si mapenzi ya Rais,” alisema.
Aliwataka wadau kutoviachia vyama vya siasa pekee kudai Katiba mpya kwa kuwa ina manufaa kwa Watanzania wote.
Mbowe alisema watahakikisha wanatumia kila aina ya mbinu ili kufanikisha kuendelea na mchakato huo.
“Leo tunamaliza mwaka 2017 lakini kwetu ulikuwa mgumu kushinda yote tangu nchi iingie katika demokrasia ya vyama vingi miaka 25 iliyopita,” alisema.
Alisema licha ya kuijenga demokrasia kwa kipindi chote hicho, utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano umerudisha nyuma.
“Pamoja na kuwa mimi ni mwenyekiti wa Chadema siwezi kuitisha mkutano wa wanachama hapa Dar es Salaam,” alisema.
Mchakato wa Katiba Mpya ulizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete mwishoni mwa mwaka 2011 alipounda Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.
Hata hivyo, mchakato huo uliishia kwenye Bunge Maalumu la Katiba ambalo licha ya kupitisha Katiba Inayopendekezwa ambayo haijapigiwa kura ya maoni hadi leo, baadhi ya vyama vya upinzani vilijitoa na kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kikiwemo Chadema na kupinga mchakato huo kwa maelezo kuwa ulivurugwa na chama tawala.
Vyama vya upinzani vimejikuta katika wakati mgumu tangu kuingia madarakani Serikali ya Awamu ya Tano kutokana na kushindwa kufanya mikutano ya hadhara, viongozi wake kukamatwa kwa tuhuma za uchochezi, kufanya fujo na uharibifu.
Mbowe alisema wakati vyama vya upinzani vinakatazwa kufanya mikutano, chama tawala kinafanya.
“Hakuna usawa katika kufanya siasa, ni sawa na kumfunga mikono bondia halafu unataka apigane na mwenzake ambaye hajafungwa mikono,” alisema.
Mbowe alisema kama Serikali inaona hakuna umuhimu wa kuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa ni bora vikafutwa kuliko kuvizuia visifanye siasa
MKE WA NAIBU WAZIRI LUGOLA, MARRY LUGOLA AFARIKI DUNIA
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Lugola amefiwa na mkewe Mary.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais imesema Mary amefariki dunia leo Jumatatu Januari Mosi, 2018 jijini Dar es Salaam.
Imeelezwa utaratibu wa mazishi unaendelea kufanyika na taarifa zitatolewa baadaye.
Wakati huohuo, Ofisi ya Bunge katika taarifa kwa umma imesema Spika Job Ndugai amemtumia rambirambi Lugola kutokana na kifo cha mkewe.
Imeelezwa msiba upo Railway Club Gerezani jijini Dar es Salaam.
Ndugai ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa kumpoteza mpendwa wao.
MCHEZO KATI YA MBEYA CITY NA KAGERA SUGAR WAAHIRISHWA KUTOKANA NA UWANJA KUJAA MAJI
NAIBU WAZIRI MWANJELWA AWATAKA WANANCHI MBEYA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI KWA VITENDO
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary
Mwanjelwa akiwasihi waumini kumuunga mkono na kumuombea Rais Magufuli wakati
akitoa salamu kwenye ibada ya Siku ya Wazee iliyofanyika katika kanisa La
Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus Healing Centre T. Ministry) lililopo
Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga Jijini Mbeya, Leo 1 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary
Mwanjelwa akimlisha chakula mmoja ya wazee waliohudhuria ibada ya Siku ya Wazee
iliyofanyika katika kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus Healing
Centre T. Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga Jijini
Mbeya, Leo 1 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary
Mwanjelwa pamoja na Viongozi wengine wakiongoza maombi wakati wa ibada ya Siku
ya Wazee iliyofanyika katika kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus
Healing Centre T. Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga
Jijini Mbeya, Leo 1 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary
Mwanjelwa akishiriki chakula cha mchana na wazee waliohudhuria ibada ya Siku ya
Wazee iliyofanyika katika kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus
Healing Centre T. Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga
Jijini Mbeya, Leo 1 Januari 2018.
Na Mathias Canal,
Mbeya
Wananchi Mkoani Mbeya wametakiwa kuunga mkono kwa vitendo juhudi
za uwajibikaji wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.
Mwito huo umetolewa Leo 1 Januari 2018 na Naibu Waziri wa Wizara
ya Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa wakati akitoa salamu kwenye ibada ya Siku ya
Wazee iliyofanyika katika kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus
Healing Centre T. Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga
Jijini Mbeya.
Alisema kuwa Rais Magufuli na serikali anayoingoza anawathamini
kwa kiasi kikubwa wazee kote nchini kwani kwa umri wao ni sehemu ya turufu
muhimu kimawazo na busara katika utendaji ndio maana Mke wake Mhe Mama Janeth
Magufuli hushirikiana na wazee waliopo katika makundi mbalimbali katika huduma
za kijamii.
Alisema kuwa serikali hii ya awamu ya Tano inayochagizwa na
kauli mbiu isemayo "HAPA KAZI TU" inawakumbusha na kuwahamasisha
wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kuinua haraka uchumi wa mtu mmoja mmoja na
Taifa kwa ujumla.
Katika ibada Hiyo Mhe Mwanjelwa ameshiriki chakula cha mchana na
wazee waliohudhuria ibada Hiyo ya siku ya wazee kutoka Kata ya Manga na Sinde
ikiwa ni ishara ya mapokezi mema ya Mwaka Mpya 2018.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo aliongoza
waumini wa kanisa la Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus Healing Centre
T. Ministry) kumuombea Rais Magufuli sambamba na serikali kwa ujumla ili
wananchi waendelea kujivunia matunda ya Rais Magufuli ambaye Duniani kote
anasifika kwa umakini na ushupavu.
Alisema kuwa zoezi hilo linapaswa kuwa endelevu kwa kanisa hilo
kushirikiana kwa Karibu na wazee huku akisema kuwa litakuwa jambo zuri na
muhimu zaidi endapo litafanyika kwa ajili ya wazee wa Mkoa mzima wa Mbeya.
"Wazee ni Tunu, kuwa Mzee ni Baraka kwani hata vijana ni
wazee wajao, Lakini niwasihi kuendelea kuwatumia wazee kwa ushauri wa kijamii
pia kidini lakini zaidi Mwaka Mpya 2018 uwe Mwaka wa Mafanikio kwetu
sote:" Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Mhe Mwanjelwa Alisifu uongozi wa kanisa hilo kwa kumualika
kushiriki nao katika ibada hiyo huku akiwapongeza kwa kufanya ibada ya kiroho
lakini pia ibada ya kimwili kwa ushirikishaji wa jamii.
Naye Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Huduma ya Maombezi na
Uponyaji (Jesus Healing Centre T. Ministry) Mchungaji Capson Masimbani
alimpongeza Mhe Mwanjelwa na kusema kuwa ni kiongozi mwenye kujali wananchi
pasina kubagua itikadi za dini zao.
Alisema kuwa ni Viongozi wachache nchini ambao wana unyenyekevu
kama yeye huku akimsihi kuendelea na busara na hekima Hiyo.
Sambamba na hayo Mhe Naibu Waziri wa Kilimo aliunga mkono juhudi za kanisa hilo kwa kuandaa sherehe hiyo ya siku ya wazee kwa kuwapatia mifuko 66 ya sukari wazee hao.
MWISHO.
WAJUA KUWA MAZIWA MTINDI UNG`ARISHA NGOZI NA KUIFANYA KUWA NYORORO
Ulisha wahi kukaa ukajiuliza mbona kuna baadhi ya watu wana ngozi nzuri laini na soft? lakini kwako ni tofauti? ukawaza labda wanatumia vitu vya bei ghali ambavyo wewe huwezi ku – afford, au umesha hangaika na ma – cosmetics lakini bado ngozi yako haikubali kukaa vizuri?

Jaribu hii Home made Yogurt Cleansing ,Tumia mtindi ambao hauna mafuta mengi au hauna kabisa (low fat),
Paka mtindi wako usoni fanya kama una sugua kwa muda mchache halafu uache kwa dakika 15, fanya hivi mara mbili kila siku na utapata matokeo kwa muda mchache.
Hii husaidia kuondoa cell za ngozi zilizo kufa (dead skin cells) na protein tighten the pore.

Jaribu hii Home made Yogurt Cleansing ,Tumia mtindi ambao hauna mafuta mengi au hauna kabisa (low fat),
Paka mtindi wako usoni fanya kama una sugua kwa muda mchache halafu uache kwa dakika 15, fanya hivi mara mbili kila siku na utapata matokeo kwa muda mchache.
Hii husaidia kuondoa cell za ngozi zilizo kufa (dead skin cells) na protein tighten the pore.
LISSU ASEMA WALIOMPIGA RISASI ALIWAONA SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
HALI ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu inaendelea kuimarika huku akiendelea na mazoezi ya viungo katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya ambako anapatiwa matibabu ya majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa kwa risasi nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma mnamo Septemba 7, 2017.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Kituo cha Runinga cha Azam TV, Lissu ameeleza namna alivyoshambuliwa huku akisema kuwa watu waliotekeleza tukio hilo la kinyama dhidi yake aliwaona japo hawajui.
“Watu walionishambulia kwa risasi niliwaona lakini siwafahamu, nilikuwa ninajitambua mpaka muda nafikishwa Hospitali ya Dodoma, na mtu wa kwanza kumpigia simu alikuwa ni Mwenyekiti wangu wa Chadema, Freeman Mbowe. Dereva wangu ndiye alinisaidia kuwasiliana naye pamoja na watu wengine kuwapa taarifa hizo,” alisema Lissu.
Aidha Lissu amewashukuru madaktari wa Dodoma na Hospitali ya Nairobi kwa kufanya jitihada zao kuokosa maisha yake.
“Nisingefika Nairobi bila msaada wa kwanza wa madaktari wa Dodoma. Nilipofika Nairobi Hospital madaktari walifanya kazi kubwa sana kunitibu na kuokoa maisha yangu hadi kufikia hapa nilipo leo. Madaktari wametoa risasi kumi na sita mwilini mwangu tangu nimefika hapa Hospitali ya Nairobi, risasi moja bado ipo mwilini na risasi zingine kumi na sita zilinikosa siku hiyo ya tukio,” alifafanua Lissu.
Akizungumzia pesa za matibabu kutoka Bungeni, Lissu amesema: “Mpaka sasa tunapoongea, Bunge halijatoa hata senti moja kwa ajili ya matibabu yangu, hili jambo si la mimi au familia yangu kuliomba Bunge kunilipia matibabu. Hii ni kwa mujibu wa sheria. Isitoshe, hakuna Ofisa wa Bunge yeyote aliyekuja kuniona hospitali tangu Septemba 7, 2017 niliposhambuliwa, si Spika, Naibu Spika wala Katibu wa Bunge.”
Kuhusu uimara wa Chadema kufuatia hamahama ya wanachama wake alisema Chadema haiwezi kufa akiwataja watu wengi walioondoka wakiwemo Kafulila na Masha. Alisisitiza chama hicho kiko imara na kitaendelea kuwa imara. Aliwahakikishia Watanzania kwamba hawatatarudi nyuma, akisema pindi akipona ataendelea na harakati zake za ubunge, kazi ambayo anaipenda kutoka moyoni
Subscribe to:
Posts (Atom)

































