| Bi HELLEN KIJO BISIMBA ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa LHRC akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi wa kitabu hicho leo jijini Dar es salaam |
Wednesday, May 28, 2014
LHRC WAZINDUA KITABU CHA URANI NA MAZINGIRA 2014,MADHARA YA MADINI HAYO YAANISHWA
Tuesday, May 27, 2014
UCHAGUZI SIMBA SC MAMBO MOTO--WAMBURA OUT
KAMA ilivyotarajiwa, Michael Richard Wambura ameenguliwa katika kinyang’anyiro
cha Uchaguzi mkuu wa Simba SC unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao, kwa sababu
kubwa mbili.
Akizungumza katika Mkutano maalum na
Waandishi wa Habari mchana huu makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), makutano ya mitaa ya Ohio na Libya, Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kamati
ya Uchaguzi ya Simba SC, Wakili Dk Damas Daniel Ndumbaro amesema Wambura
ameondolewa kwa sababu kwa sasa si mwanachama halali wa klabu hiyo.
SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI--KITAIFA NI MWANZA,WAZIRI MAHENGE ATOA NENO
Watanzania wametakiwa kuungana kwa pamoja katika
kuadhimisha siku ya mazingira duniani ambayo itaadhimishwa tarehe 5 mwezi juni
mwaka huu ambapo kidunia siku hiyo itaadhimishwa katika kisiwa cha BARBADOS
moja ya visiwa vya karibian na tanzania siku hiyo itaadhimishwa mkoani mwanza.
Akitangaza maadhimisho hayo leo mbele ya wanahabari
jijini dar es salaam waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira mh
BINILIUS MAHENGE amesema kuwa siku ya
mazingira duniani iliamuliwa na azimio la baraza la umoja wa mataifa la mwaka
1972 kama kielelezo cha ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa umoja wa mataifa
kuhusu mazingira uliofanyika huko stockholm nchini sweden.
Monday, May 26, 2014
PIGO TENA BONGO MOVIES--HUYU NDIYE MSANII MAARUFU WA KIKE ALIYEFARIKI DUNIA MUDA HUU WAKATI AKIJIFUNGUA
HABARI AMBAZO MTANDAO HUU UMEZIPATA MUDA HUU NI KUWA MSANII MAARUFU WA SINEMA ZA TANZANIA RECHO HAULE AMEFARIKI DUNIA ASUBUHI HII.MAREHEMU AMEPOTEZA MAISHA BAADA YA KUJIFUNGUA ASUBUHI HII,MUNGU AILAZE PEPONI ROHO YAKE AMEN.
HABARI KUTOKA KWA RAIS WA BONGO MOVIES STEV NYERERE AMEDHIBITISHA KUTOKEA KWA KIFO HICHO ASUBUHI HII YA JUMANNE NA TAYARI YUPO NJIANI KUELEKEA HOSPITALI YA MUHIMBILI KWA AJILI YA TARATIBU NYINGINE.
WASANII WOTE WA BONGO MOVIES MNAOMBWA MKUTANE VIWANJA WA LEADERS CLUB LEO MCHANA KWA AJILI YA KUPANGA JINSI YA KUMPUMZISHA MWENZENU.
HABARI24 BLOG INATOA POLE SANA KWA FAMILIA YOTE YA HAULE NA WANATASNIA WOTE WA TASNIA YA FILAMU TANZANIA.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA,JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
AMENNNNN
HABARI KUTOKA KWA RAIS WA BONGO MOVIES STEV NYERERE AMEDHIBITISHA KUTOKEA KWA KIFO HICHO ASUBUHI HII YA JUMANNE NA TAYARI YUPO NJIANI KUELEKEA HOSPITALI YA MUHIMBILI KWA AJILI YA TARATIBU NYINGINE.
WASANII WOTE WA BONGO MOVIES MNAOMBWA MKUTANE VIWANJA WA LEADERS CLUB LEO MCHANA KWA AJILI YA KUPANGA JINSI YA KUMPUMZISHA MWENZENU.
HABARI24 BLOG INATOA POLE SANA KWA FAMILIA YOTE YA HAULE NA WANATASNIA WOTE WA TASNIA YA FILAMU TANZANIA.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA,JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
AMENNNNN
PICHA ZA MGOMO WA MADEREVA NA MAKONDAKTA WA DALADALA LEO ASUBUHI KUGOMA KUPELEKA ABIRIA MWENGE KUTOKA MAKUMBUSHO
Kamanda wa Polisi Kinondoni akiongea na waandishi wa habari kuelezea ni jinsi gani watashughulikia shida ya barabara hiyo ya kutoka kituoni makumbusho kuelekea mwenge
Kondakta wa Daladala akiwa ameumia mkono wake wa kulia baada ya kukatwa na side mirror ya basi la UDA alipokuwa akilizuia lisipakie abiria na kuondoka kwenda mwenge
Hapo ni Madereva na makondakta wakilikimbiza basi la UDA ambalo lilimkata mkono dereva mwenzao wakati wanalizuia lisiweze kutoka ndani ya kituo kuendelea na safari.
BIBI ALIYENASWA NA MADAWA YA KULEVYA AANGUA KILIO MAHAKAMANI
BIBI wa Kinigeria, Olabisi
Ibidun Cole (65), leo ameangua kilio katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
jijini Dar ers Salaam wakati akipelekwa kizimbani kwa ajili ya kusomewa kesi
yake ya kunaswa na madawa ya kulevya yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni
37.
Hakimu aliyepelekewa kesi hiyo,
Frank Mushi, aliiahirisha kesi hiyo mpaka kesho ili bibi huyo ambaye hajui
Kiswahili wala Kiingereza atafute mkalimani.
Cole alisema lugha anayoweza
kuitumia kiufasaha ni Kiyoruba ambacho hutumiwa nchini Nigeria. Katika hali
iliyoonesha kukata tamaa, bibi huyo alianza kuangua kilio akiomba Mungu
amsaidie.
![]() |
| Bibi wa Kinigeria, Olabisi Ibidun Cole akipelekwa mahakamani. |
KAMISHNA KOVA AMLILIA MWANDISHI MZEE MAX,ATOA RAMBI RAMBI YAKE,WENGINE TUIGE KWAKE
Na Karoli VInsent
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam,lamlilia Aliyekuwa Mwandishi na mpiga Picha wa Kituo cha Runinga cha
Mlimani Mzee Maxmiliani,ambaye aliyefariki Gafla kwa Presha.
Kilio hicho, kimetolewa leo Jijini Dar
es Salaam na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman
Kova,wakati wa Mkutano na Waandishi Habari, Ambapo alisema wao kama Jeshi la
Polisi wamesikitishwa na Kifo cha Mwandishi wa huyo Mkongwe wa Habari na Mpiga
picha Nchini.
“Sisi Jeshi la polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam,Tumesikitishwa sana na Kifo cha Mzee wetu huyo Bwana
Maxmiliani,kwani amekuwa akitoa Mchango mkubwa,kwetu Jeshi la
Polisi hususani Kanda hii ya Dar es Salaam kwa kuhakikisha Taarifa
zinafika kwa Wananchi kutoka kwetu kwa wakati Muhafaka,”
SALAAM ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA MWANDISHI MAXIMILIAN JOHN NGUBE KUTOKA CHADEMA
Kurugenzi ya
Mawasiliano na Uhusiano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
imepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa taarifa za kifo cha mmoja wa waandishi
wa habari za picha (mpiga picha) mwandamizi nchini, Maximillian John Ngube
aliyefariki siku ya Ijumaa baada ya kuugua muda mfupi.
Kwa masikitiko makubwa
kurugenzi, kwa niaba ya chama, inatuma salaam za pole kwa familia ya marehemu
Maximilian kwa kuondokewa na baba na mpendwa wao, katika wakati ambao tunaamini
walikuwa bado wakimhitaji sana kama moja ya nguzo za familia.
HABARI INAYOTIKISA JIJI KWA SASA---VIJANA WA PANYA ROAD 149 WATIWA MIKONONI MWA POLISI KWA MASAA 24,KAMISHNA KOVA ASEMA HATOKI MTU,HADI WAKAMATWE WOTE,PICHA ZAO NA MAJINA YAKO HAPA
| Hawa ndio viongozi wa panya road na mbwa mwitu ambao tayari wameshakamatwa |
Maeneo
yaliyoathirika ni Kigogo, Magomeni, Tabata, maeneo yote yanayozunguka mto
Msimbazi, maeneo ya Mbagala nk. Msako
huu unaendelea kufanywa na askari wa vikosi maalum ambao wamepewa kazi ya
kuhakikisha kuwa vikundi hivyo haviibuki tena na vinatokomezwaa kabisa kwa kuwakamata wale wote wanaojihusisha na vitendo
vya kuvamia kwa mkundi wananchi ambao hawana hatia
| Kamishna kova ambaye amezungumza na wanahabari muda mfupi uliopita |
Imegundulika pia kwamba vijana hawa wanatumia dawa za kulevya aina ya bangi na wengine hujichoma sindano na kuwafanya iwe rahisi kujihusisha na matukio ya uhalifu. Vijana hao hupenda kushiriki katika ngoma kama Mnanda, Mchiriku, Kigodoro, Kanga moja nk. ambazo kwa kawaida huchezwa hadi usiku wa manane.
Wakitoka katika ngoma hizo hujikusanya pamoja na kufanya matukio ya uporaji kwa mtu wanayekutana naye, kufanya uvunjaji katika majumba na wakati mwingine wana mtindo wa kugema mafuta ya diesel au petrol katika matanki ya malori yanayosafirisha mafuta.
Operesheni kali inafanyika katika maficho ya wahalifu hao ikiwa ni pamoja na daraja la River side, Kigogo darajani, Manzese, maeneo ya Tandale pamoja na maeneo mengine ya maficho mkoa wa Kipolisi Temeke.
Tunawasiliana
na Maafisa utamaduni wa Wilaya zote za Mkoa wa D’Salaam kusimamisha utoaji wa
vibali wa ngoma za usiku ambazo hazina tija.
Pia Jeshi la Polisi linafuatilia na kuwavizia vijana wanaopora watu wanaotoka katika sherehe za usiku kama
vile Harusi na wanaotoka katika mikesha ya Ibada na sehemu zozote zenye mikusanyiko.
Aidha Jeshi la Polisi wanapambana na vijana
wanaowavizia watu katika vituo vya mabasi pindi wanapotoka alfajiri kwenda
katika shughuli zao za kila siku.
| Wanahabari |
Oparesheni
hii ni endelevu na ya kudumu hadi kero hii ya vibaka itakavyokwisha kabisa.
Baadhi ya majina waliokamatwa ni kama ifuatavyo:-
1. DANIEL
PETER @ MALUNDE, miaka 25, mkazi wa Yombo Kigunga
2. MWISHEHE
ADAM, miaka 35, mkazi wa Mtoni mashine ya maji
3. MOHAMED
SAID, miaka 32, mkazi wa Mtoni
4. JAKAMA
ALPHONCE, miaka 23, mkazi wa Mtoni Kilakala
5. HAMADI
MDUDU, miaka 25, mkazi wa Mbagala
6. SALUM
MUSA, miaka 25, mkazi wa Kiwalani
7. ANTHONY
DANIEL, miaka 20, mkazi wa Mashine ya maji
8. FIDELIN
ANTHONY, miaka 18, mkazi wa Kigogo
9. HAMZA
MAZUMA, miaka 19, mkazi wa Kigogo
10.
MGANGA ABEID, miaka 20, mkazi wa Kigogo
11.
SAID ABEID, miaka 19, mkazi wa Kigogo
12.
SALUM NYENJE, miaka 36, mkazi wa Chamazi
13.
DOMINICK PETER miaka 22, Mkazi wa Kigogo
14.
KULWA ABEID, miaka 20, mkazi wa Mabibo
15.
MUSA IBTRAHIM, Miaka 20, mkazi wa
Magomeni
16.
HUSSEIN SHABAN, miaka 22, Mkazi wa
Magomeni
S.
H. KOVA
KAMISHNA
WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
Sunday, May 25, 2014
KIINGILIO TAIFA STARS, MALAWI HIKI HAPA
Kiingilio cha chini cha mechi ya kirafiki kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (Flames) itakayofanyika Jumanne (Mei 27 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000.
Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni kwa wale watakaokaa kwenye viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa upande wa VIP B na C kiingilio kitakuwa sh. 10,000 wakati kwa VIP A itakuwa ni sh. 20,000.
MWENGE WA UHURU 2014 WAMALIZA MBIO ZAKE MKOANI RUKWA LEO, WAMMULIKA MLEMAVU WA NGOZI (ALBINO) ALIYEKATWA MKONO MWAKA JANA
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (katikati) akishiriki mbio za Mwenge wa
Uhuru (2014) na viongozi wa mbio hizo kitaifa, viongozi na wafanyakazi wa
Serikali, vyama vya siasa Mkoani Rukwa na wananchi muda mfupi kabla ya
kukabidhi Mwenge huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abass Kandoro baada ya
Mwenge huo kukamilisha mbio zake Mkoani Rukwa leo tarehe
25-05-2014. Mwenge huo wa Uhuru mkoani Rukwa ulitembelea miradi ya
maendeleo 28 na vikundi 27 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh. bilioni nne
Uhuru (2014) na viongozi wa mbio hizo kitaifa, viongozi na wafanyakazi wa
Serikali, vyama vya siasa Mkoani Rukwa na wananchi muda mfupi kabla ya
kukabidhi Mwenge huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abass Kandoro baada ya
Mwenge huo kukamilisha mbio zake Mkoani Rukwa leo tarehe
25-05-2014. Mwenge huo wa Uhuru mkoani Rukwa ulitembelea miradi ya
maendeleo 28 na vikundi 27 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh. bilioni nne
Subscribe to:
Posts (Atom)



.jpg)





