Waziri wa Ladha na Vibe wa Tigo Fiesta 2018,Kennedy The Lemedy akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Moshi, Ambapo kesho tamasha la Tigo Fiesta litaendelea Mjini Moshi mkoa Kilimanjaro .
|
Msanii Rapa wa Kike Tanzania, Rosa Ree akizungumza na wanahabari kwenye hoteli ya Panama leo mjini Moshi |
Onesho hilo latua Moshi na ofa kabambe ya Data Kama Lote inayowapa wateja hadi mara mbili ya thamani ya intaneti watakayonunua kutoka Tigo
Moshi,
Oktoba 18, 2018 –Tigo Fiesta 2018- Vibe Kama Lote imewasili mjini Moshi na ahadi ya
kuwapagawisha mashabiki wa muziki kwa vibe asilimia 100% za nyumbani pamoja na promosheni
tatu kabambe zitakazoendana na fursa kubwa za kibiashara kwa wakaazi wote wa
mji huo.
Mdhamini
mkuu wa msimu huu wa Tigo Fiesta 2018, kampuni ya Tigo imewakumbusha mashabiki
wote wa muziki mjini Moshi kufurahia promosheni zake tatu murwa katika msimu huu
wa vibes. ‘Data Kama Lote inawapa
wateja hadi mara mbili ya vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu
iliyoboreshwa ya *147*0#. Hii
itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa
kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+,’ Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Kaskazini, Nancy
Bagaka alisema.
Tigo
pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa
kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kwa tamasha la Moshi litakalofanyika katika
viwanja vya Majengo, tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa Masterpass
QR zitagharimu TSH 8,000 pekee badala ya TSH 10,000 kwa watakaonunua kwa pesa
taslim, Wateja wanapaswa kupiga *150*01#
na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha
kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.
Wateja
wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila
siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za
mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni
10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya
http://tigofiesta.co.tz
na kuchagua Trivia.
Huu
ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta
2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu linashirikisha 100%
wasanii wa nyumbani wanaozuru mikoa 15 ya nchi ikiwemo; Morogoro, Sumbawanga, Iringa,
Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na
Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment