Fastjet
kumilikiwa na Watanzania.
Tarehe,
12 Novemba 2018, Dar es salaam…..Kati ya mashirika ya ndege
zinazokua kwa kasi zaidi, Fastjet Airlines Ltd, Tanzania, leo imethibitisha
mikakati ya kumiliki shirika hilo yanaenda vizuri.
Tarehe 6 Novemba Fastjet
ilimteua Ndugu Lawrence Masha kuwa Mwenyekiti Mtendaji wa kwanza wa shirika
hilo. Uteuzi huu umedhibitisha nia ya kuendelea kuhudumia soko la ndani na nje
ya nchi kama kampuni inayomilikiwa na Watanzania pamoja na masoko ya talii za
nje.
Akizungumza leo jijini Dar es
salaam Ndugu Masha alisema, “ tumejikita zaidi kwa watanzania ambao wamefaidika
kutokana na huduma zetu kwa miaka sita sasa. Tunatarajia kuongeza kuongeza
safari za ndani na pia kuongeza idadi ya ndege ambazo zinakidhi mahitaji ya
soko”. Tunaona fursa kufanya kazi na kushirikiana na mashirika ya ndege za
ndani na nje ya nchi pamoja na Air Tanzania kutimiza mikakati ya serikati ya
utalii.
Ndugu Masha ataendeleza vizuri
na mikakati ya kubadilisha shirika hilo pamoja na uongozi kuhakikisha wanatoa
huduma kwa watanzania.
Fastjet imetoa huduma kwa miaka
sita ambapo imesafirisha zaidi ya abiria milioni 2.5 ndani ya Tanzania pekee.
Shirika hili lenye bei nafuu
lina hudumia usafiri wa ndege katika miji ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya,
Kilimanjaro, Lusaka na Zimbabwe. Na linarekodi
ya kusafirisha wastani wa abiria 30,000 kwa mwezi.
No comments:
Post a Comment