Msanii wa Bongo Fleva, Nikki Wa Pili akizungumza na
wanahabari jinsi alivyojipanga kutoa burudani kwenye tamasha la Tigo Fiesta
kesho Jumamosi.
|
Mkuu wa Mkoa Wa
Mwanza, Mhe. John Mongella akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tigo
na wasanii wataopanda kwenye jukwaa la Tigo Fiesta uwanja wa CCM Kirumba kesho.
|
Msanii wa Bongo Fleva, Wakazi akizungumza na wanahabari
jinsi alivyojipanga kutoa burudani kwenye tamasha la Tigo Fiesta kesho Jumamosi
uwanja wa CCM Kirumba.
|
Wakaazi wa Mwanza kufurahia ofa murua ya
Data Kama Lote inayowapa wateja hadi mara mbili ya thamani ya intaneti
watakayonunua kutoka Tigo
Jumamosi
hii, jiji la Mwanza linatarajiwa kufurika na vibe kama lote kutoka kwa wasanii
100% wanaokonga nyoyo za mashabiki wa msimu huu wa Tigo Fiesta 2018- Vibe Kama Lote.
Baada ya wiki saba ambazo zimeshuhudia
msimu huu mkubwa zaidi wa kitamaduni katika ukanda wa Afrika ya Masahariki na
Kati ukizuru miji ya Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Njombe, Mtwara, Songea na
Moshi, Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote sasa imetua katika fukwe za Ziwa
Victoria na ipo tayari kutifua vumbi katika viwanja vya CCM Kirumba leo Jumamosi
tarehe 27 Oktoba.
Waandaaji wa tamasha hilo, kampuni ya
Clouds Media group wamesema vibes katika jiji la Mwanza zitaongozwa na msanii
Fid-Q ambaye ni mzaliwa wa jiji hilo, akisindikizwa na kundi la Weusi, Rostam,
Wakazi na Rich Mavoko. Wasanii wengine watakaopagawisha siku hiyo ni Jux,
Barnaba, Whozu, Nandy, Aslay, Country Boy, Nedy Music, Nkunda Star pamoja na
Jay Melody. Mwanza pia itashuhudia vibes kutoka kwa Mchama the Best, Jolie,
Benson watakaotanguliwa na washindi wa shindano la kusaka vipaji la Tigo Fiesta
Supa Nyota.
Akiashiria kuanza kwa msimu huu wa
vibes jijini Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alizungumzia uwepo
wa fursa za biashara zinazoambatana na msimu huo. “Wamiliki wa kumbi za
starehe, hoteli na nyumba za kulala wageni, mam ntilie, wauza maji na wamiliki
wa vyombo vya usafiri ikiwemo bodaboda wote wana fursa kubwa ya kujiongezea
kipato kwa sababu tunaratajia maelfu ya wageni kufurika jijini Mwanza katika
kipindi hiki,’ alisema.
Hali
kadhalika, kampuni ya Tigo imewakumbusha wakaazi wa Mwanza wazikose kufurahia
promosheni murwa ya Data Kama Lote itakayowapa
bonasi ya hadi mara mbili kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia
menu iliyoboreshwa ya *147*0#. ‘Hii
itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa
kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+,’ Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Ziwa, Uthman
Madati alisema.
Tigo
pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa
kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kwa tamasha la Mwanza litakalofanyika, tiketi
zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu TSH 8,000 pekee
badala ya TSH 10,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslim, Wateja wanapaswa kupiga *150*01# na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua
namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.
Wateja
wa Tigo pia wanaweza kujaribu umahiri wao wa kujibu maswali yanayohusiana na
msimu wote wa vibes kupitia shindano la Tigo
Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia. Washindi
wanajinyakulia zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za wiki za TSH 1 milioni,
simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge
nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma
neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz na kuchagua
Trivia.
Huu
ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta
2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu linashirikisha 100%
wasanii wa nyumbani wanaozuru mikoa 15 ya nchi. Baada ya Mwanza, tamasha hilo
linahamia Musoma kabla ya kutua Muleba, Kahama, Arusha Singida na Dodoma, huku
kilele kikifanyika jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment