Wakati ikiwa bilionea maarufu Ernest Babu ‘Sambeke’amezikwa huko arusha wiki hii tata umegubika kuhusu idadi ya wake wa marehemu baada ya taarifa kudai kuwa alizaa na wanawake watatu tofauti enzi ya uhai wake.
Hata hivyo, Msemaji wa familia, Dk Richard Masika alisema juzi kuwa marehemu ameacha mke mmoja, Marcelina Sambeke na watoto watatu.
Dk Masika alitaja majina ya watoto wa marehemu kuwa, ni Siah, Getrude na Jamal ambaye amefuata taaluma ya baba yake ya urubani, hivi sasa yuko Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akichukua fani hiyo.
Taarifa hizo zinadai enzi za uhai wake, marehemu hakupenda kuishi na wanawake hao balialipenda kuishi na watoto wake muda wote hadi anakutwa na mauti.
Mmoja wa ndugu wa karibu na marehemu, alidai kuwa Sembeke hakupenda kuishi na wanawake hao kwa sababu kipaumbele chake kilikuwa kimeegemea kwa watoto wake. Mmoja wa wanawake wanaodaiwa kuzaa na Sembeke, Leila Ally mkazi wa Kilimanjaro, alikiri kuzaa naye mtoto aitwaye Jamal ambaye hivi sasa anachukua fani ya urubani.
“Mimi ni mzazi mwenzake, nimezaa naye mtoto mmoja anaitwa Jamal,” alidai Leila kwa huzuni. Akisimulia historia yake, Leila alisema waliwahi kuishi na marehemu wilayani Moshi na kuna wakati aliwahi kwenda nchini Kenya kuchukua masomo ya urubani.
Suala la idadi ya wanawake waliozaa na marehemu limeonekana kuzua utata katika msiba huo, taarifa za ndani zinadai kuwa baadhi ya wanafamilia wameanza kuhisi huenda likazua tafrani katika mirathi.
Pia, Jamal alipotafutwa alikiri kuwa miongoni mwa watoto wa marehemu, huku akisema ameamua kufuata fani ya baba yake.
Hata hivyo, Dk Masika alipoulizwa iwapo watoto hao ni wa mama mmoja, hakutoa majibu ya uhakika.
No comments:
Post a Comment