Amana Mbijili 30 mkazi wa Vinhawe Wilayani Mpwapwa akiwa haamini Baada ya kuambiwa Mtoto aliyejifungua Kafariki, kama alivyokutwa na Mpiga picha wetu Katika wodi Namba 17
Wananchi waliofika kushuhudia tukio la kubadilishwa kwa watoto mara baada ya wazazi wao kujifungua wachungulia madirishani Kwenye whodi namba 17 jana
AMANA Mbijili Mkazi wa kijiji cha Vinhawe Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma ameilalamikia Hospital ya Rufaa ya General kwa kitendo cha manesi kumbadirishia motto baada ya kujifungua.
Tukio hilo lililotokea jana Hospitalini Hapo majira ya saa 11 jioni baada ya Mwanamama Huyo kujifungua kwa njia ya upasuaji na moja kwa moja kupelekwa chumba cha mapumziko kilizua Tafrani .
Akielezea tukio hilo Mbijili alisema alishangazwa na kitendo cha yeye kulazwa chumba tofauti na mtoto wake ndipo alipo muuliza mmoja wa manesi alipo mtoto wake akajibiwa kuwa mtoto huyo alishafariki kitendo ambacho yeye hakuridhika nacho.
Alisema hakuridhika kutokana na kuona mtoto mwingine akipitishwa na kuingizwa chumba kingine akiwa amefungwa moja ya nguo alizofika nazo hosipitalini hapo akiwa hai ndipo akaanza kulalama na baada ya kuona hivyo nesi yule akaenda kumletea mtoto akiwa hai na kumkabidhi.
Amana alisema‘’nilipoanza kulalamika kwa sauti ndipo wakaamua kuniletea mtoto wangu akiwa hai kitendo kilichonifanya nilie kwa furaha baada ya kumpata mwanangu, japo sijui kama walichanganya watoto au walitaka kuniibia makusudi maana hata hivyo sikuona mama wa huyo marehemu mungu ndiye anajua mimi namshukuru,’’ alisema Amana
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu Zainab Chaula alisema ni kweli tukio hilo lilitokea lakini limenukuliwa tofauti maana yeye anachojua Mama wa Mtoto huyo alifanyiwa upasuji baada ya kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida.
Chaula alisema kawaida mtotoakizaliwa lazima alie lakini mtoto huyo hakulia ndiyo sababu ya kumpeleka Chumba cha Leba kuliko na kitanda chenye mashine maarumu na hata hivyo Mtoto huyo alifariki.
‘’ hiyo ya kupewa Mtoto akiwa hai ni uvumi usio na maana, kwani baada ya kuona kelele zimezidi ikabidi tumwambie Baba wa mtoto kuwa amefariki na alidhibitisha kutokana na mtoto kufanana nae na yule,’’ alisema
HABARI KWA HISANI YA MAASINDA BLOG
No comments:
Post a Comment