HABARI KWA HISANI YA MAASINDA BLOG
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bw ,Benard Membe akiwa na wanafunzi wa vyuo vikuu mkoa wa Iringa wanaotoka mkoa wa Mtwara na Lindi jana |
Waziri Membe |
Na Francis Godwin,Iringa
HUKU hali ya mambo ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) kuwa si shwari kutokana na makada wake kuendelea kupigana vikumbo ikiwa ni sehemu ya harakati mbio za urais mwaka 2015 , waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Benard Membe ameibuka na kutoa ya moyoni kuwa atakuwa tayari kuwania urais mwaka 2015 iwapo wananchi wataona anafaa na watamtaka agombee nafasi hiyo.
Pia waziri Membe alisema kuwa hali ya nchi inavyokwenda kwa sasa si shwari kutokana na baadhi ya wabunge wa CCM na vyama vya upinzani kuendelea kuzungumza ovyo ovyo juu ya chama na serikali jambo ambalo ni hatari zaidi kwa Taifa.
Waziri Membe aliyasema hayo jana wakati akijibu maswali ya mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuhusu mbio hizo za Urais .
mtandao huu ulifanya mahojiano hayo mjini Iringa baada ya kumalizika kwa kongamano la wana vyuo vya elimu ya juu mkoani Iringa kongamano lililofanyika katika ukumbi wa St. Dominic ambako alikuwa mgeni rasmi waziri Membe alisema kuwa pamoja na kauli yake ya kwanza kwa Taifa kuwa muda bado kufika wa kufanya hivyo .
Waziri huyo alisema kuwa mbali ya kuwa muda wa kutangaza kuwania nafasi hiyo bado haujafika na chama chake kina utaratibu wa kutangaza mara baada ya muda kufika ila kwa mtazamo wake kama alivyopata kuueleza umma awali alipozungumza na vyombo vya habari juu ya mbio hizo za urais ,alisema kuwa anaheshimu sana taratibu za chama .
" Naomba kurudia tena mimi nilishapata kuueleza umma kuwa muda bado haujafika wa kutangaza kugombea Urais ....ila nasema hivi natagemea sana ushauri wa watanzania iwapo wataniona nafaa na kunitaka nigombee nitapima mawazo yao na iwapo ni wananchi wengi watakaoniunga mkono kutaka nigombee basi nitachukua fom na kuijaza ili nigombee nafasi hiyo kwani sauti ya wengi ni sauti ya Mungu " alisema waziri Membe
kuwa kama wananchi watasema jaza fom na nikaona ni sauti ya wengi nitajaza fomu ya kuwania kiti cha urais
Pia alisema kuwa hadi sasa hali ya nchi inazidi kwenda vibaya kutokana na kila mtu kuzungumza mambo bila kuthathimini na kuwa mbaya zaidi hata baadhi ya wabunge wa CCM nao wamekuwa si msaada kwa chama kutokana na mambo wanayozungumza dhidi ya serikali na chama.
Kuhusu mwenendo wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa sasa waziri Membe alisema kuwa kwa upande wake amepata kukaa bungeni zaidi ya miaka 15 toka bunge la spika Pius Msekwa hadi sasa chini ya spika Anne Makinda ila anachokiona ni baadhi ya wabunge kukosa maadili na kuzungumza mambo bila kuzingatia kanuni za bunge jambo ambalo ni hatari zaidi.
Alisema kuwa bunge linalotazamwa na watanzania ni lazima liwe bunge lenye mfano wa kuigwa na lenye kuzingatia maadili katika kuzungumza ila kwa sasa ndio maana bunge linaendelea kupoteza mwelekeo wake .
"Bunge linapoteza mwelekeo kutokana na mawazo ya baadhi ya wabunge wakifikiri wakisema ovyo na kutumia lugha kali katika kuzungumza basi wao ndio wanaonekana ni wabunge bora kitu ambacho hakipo ....kwani kuwa mbunge ni pamoja na kujiheshimu na kutumia lugha nzuri katika kuwakilisha wapiga kura wako bungeni"
Waziri Membe alisema kuwa kitendo cha baadhi ya wabunge kutotumia busara katika kujadili mambo bungeni si ubunge mzuri na watambue wazi kuwa wananchi wao wanawatazama na hukumu yao itatolewa mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu kama hivyo wanachokifanya ni kuwawakilisha wananchi ama kujiwakilisha wao.
"Nawaomba wabunge kuwa wazalendo na kuwawakilisha wananchi waliowatuma badala ya kuligeuza bunge kama sehemu ya kuonyesha ujuzi wa kuzungumza ovyo ....nasema tuwaogope wananchi mwaka 2015 watatoa adhabu kwa kila mbunge kwa sasa wananchi wanakusikiliza na kunakutazama ila muda ukifika watakuacha"
Alisema kuwa wabunge wengi ni vijana na wanafikiri kusema vibaya juu ya CCM ndio ubunge bora ila watu watafanya uchunguzi wa kutembelea jimbo la mbunge husika na kuangalia kuwa amefanya nini katika jimbo lake na watakupima kwa kazi uliofanya na sio ukali wako bungeni.
Aidha waziri Membe alisema kuwa baadhi ya wabunge wa CCM wamekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi katika majimbo yao na pia wamekuwa msaada kwa chama na serikali chini ya Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa msaada mkubwa wa kusukuma mbele maendeleo ya Taifa ila baadhi yao wapo kwa ajili ya kuonyesha uwezo wao wa kusema ovyo.
No comments:
Post a Comment