Sasa ni wazi kwamba aliyekuwa kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza ameuawa na genge ndani ya Polisi akiwemo Kamanda Polisi anayejulikana kwa jina la Muna, gazeti la Jamhuri limeripoti katika ukurasa wa Mbele kabisa (Nimesoma kwenye website yao Deo Balile akilalamika gazeti kununuliwa kwa jumla na watu wasiojulikana)
Kuvuja kwa siri hiyo kumetokana na mmoja wa jambazi sugu ajulikanaye kwa jina la Edward Malele kujisalimisha ktk vyombo vya ulinzi na kutoa siri zote.
Jambazi huyu aliombwa wa genge ndani ya polisi kushiriki katika mpango wa kumwua kamanda Barlow. Akakataa kwa kuwa aliwahi kumfahamu kwa karibu kamanda Barlow.
Baada ya kukataa kutekeleza agizo hilo baada ya siku chache alishtakiwa kwa kosa la ujambazi na kuswekwa Rumande.
Akiwa huko ndani ya wiki moja alisikia habari za kifo cha kamanda Barlow. Akajua akina na Muna aliowakatalia wamefanya kazi aliyoikataa yeye. Na alijua yuko mahabusu kwa sababu ya kukataa mradi huo.
Baada ya kukaa huko muda mrefu bila shitaka kueleweka wala mshataki wake huko Lupango walimua kumwaichia. Akagoma kutoka kwa sababu anajua kuwa, kwa kuwa amepelekwa huko ili kuficha siri hivyo, akitoka lazima atauawa. Baada ya muda akaamua kukubali kutoka lupango na kukimbilia kituo cha JWTZ huko Mwanza.
Huko JWTZ Alijieleza vya kutosha na wanajeshi walimwonea huruma wakampa Nauli na Tsh 10,000/= ya kula njiani ilie aende Bungeni huku wakiwa wamemkabidhi namba za simu za wabunge 2 wa upinzani ili wamsaidie.
Kutokana na kutokuelewa kwake alipokuwa anashangaa shangaa katika eneo la Bunge, alikamatwa na polisi wanalinda eneo hilo. Polisi hao wakapiga simu Dodoma central na Mwanza. Haraka haraka mwanza wakataka arudishwe mwanza kwa kuwa ni jambazi sugu.
Hata hivyo, kwa katika kurupushani hiyo taarifa zimeshameshamfikia Pinda na Nchimbi ambapo gazeti linaripoti kuwa Pinda ameagiza kijana huyo apewe ulinzi na asirudishwe Mwanza.
Hata hivyo amepelekwa kusiko julikana.
Kwa mapana zaidi soma gazeti la Jamhuri KAMA zinanunuliwa kwa kasi na watu wasiofahamika.
No comments:
Post a Comment