Kuanzia tarehe 26 Juni hadi 3 Julai, Rais Obama na Mkewe
wanatarajia kutembelea nchi za Senegal, Afrika ya Kusini na Tanzania. Katika
ziara yake hiyo, Rais atawekea mkazo umuhimu ambao Marekani inauweka katika
ushirikiano wetu wa kina na unaoendelea kuimarika na nchi za Afrika Kusini mwa
Jangwa la Sahara kupitia mipango mbalimbali ikiwemo ile ya kuimarisha ukuaji wa
uchumi, uwekezaji na biashara, uimarishaji wa taasisi za kidemokrasia na
uwekezaji katika kizazi kipya cha viongozi wa Kiafrika.
Rais atakutana na viongozi mbalimbali wa kiserikali, sekta
binafsi na jumuiya huru ya kiraia ikiwemo vijana ili kujadili ubia wetu wa
kimkakati katika ushirikano wetu rasmi na masuala mengine ya kimataifa. Ziara
hii itadhihirisha dhamira ya dhati ya Rais ya kupanua na kuimarisha ushirikiano
kati ya Marekani na watu wa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara katika
kuimarisha amani na ustawi katika kanda hii na duniani kote kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment