Sunday, July 7, 2013
EXCLUSIVE.HII NDIO LIST YA VIONGOZI WA BONGO WANAOSEMEKANA WAMEJIUNGA FREMASOON,USHAHIDI WA PICHA HUU HAPA
Siri ya List za Viongozi wa Tanzania Yatajwa (Secret Society), Freemason, imedaiwa kuwa na siri nzito na viongozi wakuu wa nchi yetu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sir Andy Chande akiwa nchini India katika Mji wa Chennai kuzindua hekalu lao la East Star, alieleza kwamba marais wawili wa kwanza wa Tanzania hawakuwa Freemasons lakini walifahamu taasisi hiyo ni nini na inafanya nini katika nchi hii.Aidha, aliwahi kuweka wazi kuwa hata Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere alikuwa akiijua taasisi hiyo na aliwahi kuikingia kifua ilipotaka kunyang’anywa jengo lao ambalo lipo Sokoine Drive, katikati ya Jiji la Dar es Salaam linalofahamika kama Freemasons Hall.
KITABU CHAKERais mstaafu, Mkapa katika kitabu cha Sir Andy Chande kiitwacho ‘Shujaa wa Afrika, Safari kutoka Bukene’ ameandika utangulizi akisema Chande alikuwa akijulikana kama JK na alifahamiana naye baada ya kumuingiza katika bodi ya Shule ya Shaaban Robert.Mkapa amesema Sir Chande ametambuliwa na kupewa heshima na vyombo vya taifa na vya kimataifa, heshima ambayo anaistahili kabisa. “Mimi nafurahi kuhusishwa na kutambuliwa kwa sifa na heshima anayopewa,” alisema Mkapa katika maandishi yake.
Mnajimu maarufu nchini, Maalim Hassan Yahya Hussein ambaye amekuwa akiandika makala za Freemasons katika gazeti hili, alipohojiwa na mwandishi wetu kama viongozi hao wanafahamu taasisi hiyo inajishughulisha na nini, alisema japokuwa hakuna anayejua wanachokifanya wanachama wa Freemasons huku uraiani lakini anaamini kuwa viongozi wakuu wa nchi wanajua kila kitu.“Kwa kawaida huwezi kualikwa katika chama au taasisi fulani bila kujua shughuli zao hasa kwa viongozi wakuu kama hawa, sasa kama waheshimiwa Mkapa, Mwinyi, Sumaye, Karume na Kikwete waliwahi kualikwa au kumualika Sir Andy Chande ni wazi kuwa wanafahamu shughuli zake na taasisi yake,” alisema Maalim Hassan.
Hivi karibuni, nchini Kenya, aliyekuwa Waziri wa Usalama, Profesa George Saitoti aliyefariki kwa ajali ya helikopta, kifo chake kimehusishwa na Freemasons kwa kudaiwa kuwa alipokuwa Makamu wa Rais wa Kenya wakati wa utawala wa Daniel Arap Moi, aliwahi kupiga marufuku makanisa au dini zinazojihusisha na imani za kishetani. Imeelezwa kuwa wengi wanadhani kuwa angeweza kuwa Rais wa Kenya iwapo angegombea hivyo kurejesha amri yake ya kupiga marufuku imani ambayo yeye haiamini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment