BAADA YA MBUNGE WA JIMBO LA UBUNGO JOHN MNYIKA KUSEMA KUWA KATIKA MKUTANO WA JUZI ALIKOSWA NA BOMU NA KUPONA JESHI LA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM LIMEKANUSHA TAARIFA HIZO NA KUDAI NI ZA UWONGO NA HAZINA UKWELI WOWOTE NA KUWATAKA WATANZANIA KUTISIKILIZA MANENO HAYO.
AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM NAIBU KAMISHNA WA JESHI LA POLISI KANDA MAALUM DSM BW ALLY MLEGE AMESEMA KUWA CHAMA CHA CHADEMA KILIKUWA KIFANYE MKUTANOUWANJA WA SAHARA ULIOPO MABIBO KINYUME NA UTARATIBU
BAADA YA KUKASANYIKA KATIKA UWANJA HUO WA SAHARA MABIBI AMBAPO MGENI RASMI ALIKUWA MH JOHN MNYIKA POLISI WALIJARIBU KUMWELEZA KUWA KUFANYA MKUTANO HAPO NI KINYUME NA SHERIA NA MNYIKA AKAELEWA NA KUWATANGAZIA WAFUASI WAKE KUWA WAHAME MAENEO HAYO NA KWENDA MAENEO HAYO
WAKATI HAYO YAKIENDELEA ASKARI NO E.5340 D /CPL JULIUS ALIYEKUWA NDANI YA GARI ALIKUWA AKISOGEZA MABOX YALIYOKUWA NA MABOMU YA MACHOZI KAMA TAHADHARI KATIKA MKUTANO HUO NA YALE YA KURUSHA KWA MKONO AMBAPO KWA BAHATI MBAYA BOMU HILO LILILIPUKA NDANI YA GARI HILO NA HALIKULETA MADHARA YOYOTE KWA ASKARI WALA KWA WANANCHI
BAADA YA HAPO MH MNYIKA ALIKUBALIANA NA POLISI KUWA WAHAME PALE MABIBO NA WALEELEKEE UBUNGO AMBAPO NDIPO MKUTANO HUO ULIPANGWA KUFANYIKA SIKU HIYO NA HAO WALIONDOKA KWA AMANI BILA FUJO YOYOTE ILE
HIVYO AKASEMA KUWA HABARI AMBAYO IMEENEA KUWA NH MNYIKA ALIKOSWA KOSWA NA BOMU NI UWONGO NA SIO KWELI HATA KIDOGO NA KUWAOMBA WATU KUTOZIAMINI
No comments:
Post a Comment