Wizara
ya elimu na mafunzo ya ufundi nchini imetangaza rasmi taarifa ya uchaguzi wa
kuingia kidato cha tano,katika shule za secondary za serikali na vyuo vya
ufundi huku taarifa hiyo ikionyesha kutoa kipaumbele kwa wanafunzi wa masomo ya
sayansi.
Akitoa
taarifa hiyo mbele ya wanahabari naibu waziri wa wizara hiyo mh PHILIPO
MULUGO
amesema kuwa wanafunzi waliochaguliwa kusoma masomo ya sayansi ni wengi kuliko
wale wa masomo mengine,jambo ambalo amesema ni mkakati wa serikali kuendelea
kutilia mkazo masomo hayo ambayo awali yalionekana magumu kwa wanafunzi
Mh MULUGO
amesema jumla ya watahiniwa 34599
waliofanya mtihani wa kidato cha nne
mwaka jana kutoka tanzania bara waliokuwa na sifa za kuchaguliwa kujiunga na
kudato cha tano na vyuo vya ufundi ni 34482
wakiwemo wavulana 23976
na wasichana 10506.
Aidha akitaja vigezo vilivyotumika kuwachagua
wanafunzi hao kujiunga na kidato cha tano amesema kuuwa mwanafunzi alitakiwa
kujaza form maalum SELFORM
na kuchagua shule anayotaraja kwenda pamoja na kukidhi ufaulu wa masomo ambayo
aliyachagua
QIN-----------------------
Katika
hatua nyingine MULUGO amesema kuwa serikali imebadili mfumo wa muda
wa kujiunga kidato cha tano ambapo sasa watakuwa wakijiunga mwezi julai tofaui
na zamani huku akiwataka MPENZI MSOMAJI TUNAHANGAIKA KUPATA MAJINA YA WOTE WALIOCHAGULIWA HAPA ILI HADI KUFIKIA JIONI UWE UMEYAPATA
No comments:
Post a Comment