Watu wanaosadikiwa n majambazi leo jijini dar es salaam wamevamia benk ya HABIBU AFRICAN BENK ILIYOPO KARIAKOO JIJNI DAR ES SALAAM na kufanikiwa kupora zaidi ya bilion moja ya kitanzania huku waakiondoka kimya kimya bila tatizo lolote
Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo mbele ya waandishi wa habari jijini dar kamishna wa kamda maalum ya dar es salaam SULEMAN KOVA amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa tatu aubuhi ambapo majambazi hao waliingia kama wateja na kisha kuanza kuwaweka wafanyakazi wa benki hiyo chini ya ulinzi na kisha kupora fedha zote katika benk hiyo
Amesema kuwa baada ya polisi kufika katika eneo hilo wamegundua kuna mazingira ya uzembe wa uongozi wa benki hiyo ikiwemo mlinzi aliyekuwa akilinda alikuwa hana silaha yoyote hata rungu ya kujihami kitu ambacho amesema kuwa ni makosa makubwa sana,aidha amesema kuwa benki hiyo haikuwa na ulinzi wa uhakkika ikiwemo kamera za cctv ambazo amesema hazikuwepo.
Aidha amesema kuwa jeshi la polisi linamshikilia meneja wa benki hiyo DANIEL MATEMBA pamoja na mlinzi ENDRU PETER kutokana na kuonekana kuwa wamepanga njama za tukio hilo kutokana na wao kutokuhangaika kuwazuia wezi hao ambapo amesema kuwa jeshi linawahoji kujua kama wanahusika ama la.
Aidha katika tukio jingine usiku wa kuamkia leo poisi imekamata watu wanne kwa tuhuma za kumchoma dereva tax kisu kifuani hadi kufa maeneo ya OBAMA ROAD jjini dar es salaam
KAMISHNA KOVA AMMETANGAZA HALI HATARI HUKU AKITOA MILLION 100 KWA YEYOTE ATAKEYELETA TAAIFA ZA WAHALIFU HAO
No comments:
Post a Comment