Friday, September 20, 2013

JUKWAA LA KATIBA LATEMA CHECHE,LASEMA MCHAKATO WA KATIBA UNA HATARI YA KUKWAMA,WAKANA KUUNGANA NA VYAMA VYA SIASA

            Jukwaa la katiba tanzania limesema kuwa halina imani na mchakato wa kutafuta katiba mpya tanzania unavyokwenda huku likisema kuwa mchakato huo unavyokwenda unaweza kufeli muda wowote kutokana na mambo mengi yanayoonekana katika mchakato huo

         Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dar es salaam mwenyekiti waa jukwaa hilo bw DEUS KIBAMBA amesema kuwa ukimya uliotanda katika utayarishaji wa mswada kuanzia hatua ya ofisi ya mwanasheria mkuu hadi kusomwa kwa mara ya kwanza bungeni mwezi june umewashangaza sana.

          Amesema kutokana na mambo mengi yanayoweza kuvuruga mchakato huo ikiwemo fujo zilizotokea bungeni amesema kuwa wanamsihi raisi JAKAYA KIKWETE kitosaini mswada uliopitishwa bungeni na badala yake mswada huo urudishwe mara moja bungeni kujadiliwa upya.
MWENYEKITI WA JUKWAA LA KATIBA TANZANIA BW DEUS KIBAMBA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

WAANDISHI WA HABARI WALIOJITOKEZA KUMSIKILIZA KIBAMBA AKIZUNGUMZA

Aidha katika hatua nyingine bw KIBAMBA amesema kuwa jukwaa la katiba halijaungana na vyama vya siasa kama ilivyoripotiwa na baadhi ya watu bali kilichofanyika ni vyama hivyo kulitembelea jukwaa la katiba na kukubaliana baadhi ya hoja kuzisimamia kwa pamoja.

No comments: