KATIBU WA BARAZA LA HABARI TANZANIA MH KAJUBI MUKAJANGA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM |
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam katibu wa baraza hilo bw KAJUBI MUKAJANGA amesema kuwa ukaguzi huo umefanyika baada ya kugundua kuwa kuna baadhi ya wamiliki wa vyuo wamekuwa wakitoa elimu ambayo haistahili pamoja na kupokea malalamiko mengi kutoka kwa waandishi wa habari kuwa wamekuwa wakipokea wanafunzi ambao hawajui kitu
Amesema kuwa vyuo viwili tuu ndio vimekidhi vigezo vya kuendelea kutoa elimu kwa kutumia mtaala wa nacte ambavyo amevitaja kuwa ni A3INSTITUTE OF PROFESSIONAL STUDIES cha jijini dar es salaam,pamoja na ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLLEGE kilichopo arusha.
Amesema kuwa vyuo vingine ambavyo havijakidhi vigezo hivyo vimepewa muda hadi mwezo wa 12 kutimizaa masharti huku akuvutaja kuwa ni DSJ,TSJ,ROYAL COLEGE,INSTITUTE OF SOCIAL MEDIA,PAMOJA NA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI ZANZIBAR
Aidha baraza hilo limetoa onyo kali kwa watua ambao wanaanzisha vyuo vya uandishi wa habari kwa lengo la kujipatia fedha na kushindwa kuvisimamia akisema kuwa hatua kali juu yao zitachukuliwa.
No comments:
Post a Comment