KATIBU MKUU WA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI BW PR SIFUN MCHOME AKIIZUNGUMZA NA WANAHABARI |
Jedwali Na 1
MUUNDO WA ALAMA NA UFAULU
ALAMA
|
UWIGO WA ALAMA
|
IDADI YA ALAMA
|
TAFSIRI
|
A
|
75 -
100
|
26
|
Ufauli
Uliojipambanua
|
B+
|
60 -
74
|
15
|
Ufaulu
bora sana
|
B
|
50-
59
|
10
|
Ufaulu
mzuri sana
|
C
|
40 -
49
|
10
|
Ufaulu
mzuri
|
D
|
30 -
39
|
10
|
Ufaulu
Hafifu
|
E
|
20 -
29
|
10
|
Ufaulu
hafifu sana
|
F
|
0 -
19
|
20
|
Ufaulu
usioridhisha
|
Kwa aina hii ya muundo wa
alama, na kwa kuwa muundo wa GPA utaanza kuandaliwa na wadau kuelimishwa kabla
haujaanza kutumika, katika kipindi hiki mpaka wakati huo, muundo wa madaraja
utakuwa kama inavyooneshwa kwenye jedwali la 2 hapa chini.
Jedwali Na 2
MUUNDO WA MADARAJA
MUUNDO WA ZAMANI
|
MUUNDO MPYA
|
MAELEZO
|
||
POINTI
|
DARAJA
|
POINTI
|
DARAJA
|
|
7-17
|
1
|
7-17
|
I
|
Kundi
la ufaulu uliojipambanua na bora sana
|
18-21
|
II
|
18-24
|
II
|
Kundi
la ufaulu mzuri sana
|
22-25
|
III
|
25-31
|
III
|
Kundi
la ufaulu mzuri na wa wastani
|
26-33
|
IV
|
32-47
|
IV
|
Kundi ufaulu hafifu
|
34-35
|
0
|
48-49
|
V
|
Kundi la ufaulu usioridhisha
|
Wataalamu wa mifumo ya mitihani watalifanyia kazi zaidi jedwali hili la
madaraja ili liweze kutumika kwa ufanisi katika kipindi hiki cha mpito.
Kwa mantiki hii, Daraja Sifuri linafutwa na
kuwekwa daraja litakalojulikana kama Daraja la Tano na ambalo litakuwa ndilo la
mwisho kabisa katika ufaulu.
HITIMISHO
Mabadiliko haya yamefanyika
ili kuendelea kuimarisha mfumo wetu wa elimu na kuweka wazi taratibu mbalimbali
kwa ajili ya mitihani na masuala mengine. Yako mambo mengi mengine ambayo
hayana budi kuendelea kuimarishwa ikiwemo mfumo wa mitaala, walimu, mazingira
ya kujifunzia na kufundishia pamoja na vitabu na vifaa vingine muhimu katika
elimu. Masuala haya yanaendelea kuangaliwa kupitia mikakati mbalimbali ikiwemo
mpango wa Matokeo Makubwa Sasa ama Big
Results Now (BRN).
Ushirikiano wa wadau wote ili kuleta tija kwenye elimu
ni muhimu sana na hivyo wizara itaendelea kuwashirikisha wadau wote kwa kadri
itakavyohitajika na wadau pia wanaombwa wasiache kuishirikisha wizara pale
watakapokuwa na jambo lolote ambalo linahitaji ushirikiano ili kwa pamoja
tuweze kupata mafanikio katika sekta ya elimu.
Imetolewa,
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
No comments:
Post a Comment