Saturday, October 12, 2013

samahani msomaji picha zinatisha sana..MAAJABU YA DUNIA MTU MMOJA AKUTWA NA KONTENA NZIMA LA MAFUVU YA BINADAMU,DUNIA INAKWISHA,SAMAHANI KWA PICHA ZINATISHA SANA


1615141312111087654321


17
         Wengi walioipata hii taarifa wanashangaa imekuaje ni viungo tu vya binadamu vimepatikana kwenye kontena zima vikiwa vinaingizwa Kenya? vinakwenda wapi? kazi yake ni nini?

               Taarifa iliyoripotiwa na Citizen TV Kenya inasema Shehena hii iliyokamatwa baada ya kupitishwa kwenye bandari ya Mombasa inasemekana imesafirishwa na Mwanasiasa maarufu ambae kabla ya kukamatwa alisema ilikua na bidhaa za nyumbani ambapo ilipofika kwenye kituo cha ukaguzi wa mashehena cha Changamwe ilipatikana na vikaragosi vya mafuvu na mifupa ya binadamu ndipo amri ikatoka kontena likamatwe.

             Baadhi ya mifupa ya binadamu iliyopatikana ni pamoja na mafuvu, miguu na mikono pamoja bidhaa za nyumba ambapo vyote kwa pamoja vilikua vinasafirishwa ambapo Afisa wa maswala ya Uhusiano mwema wa KRA Fatuma Yusuf alithibitisha kwamba hii shehena iliingia kutoka China siku ya pili ya October 2013 kabla ya kugundulika ilikua na vikaragosi vya kutisha ikiwemo mifupa ya binadamu
 
               Mpaka sasa uchunguzi wa shehena hili unaendelea lakini baadhi ya wakazi wa Mombasa wameonyesha wasiwasi wao na kusema kuna haja ya Serikali kutoa ripoti ya ibada za kishetani ambayo inasemekana kubuniwa na Rais Mstaafu Daniel Arap Moi miaka kadhaa iliyopita .
 

No comments: