Thursday, November 28, 2013

BAADA YA KAPUYA KUDAIWA KUTOROKA NCHINI KUKWEPA POLISI,SASA ATEGWA UWANJA WA NDEGE

Na Karoli Vinsent

   BAADA ya kufanikiwa kuukwepa mtego wa polisi na kufanikiwa kutimkia nje ya nchi kukwepa mkono wa sheria dhidi ya tuhuma za kutishia kumuua binti anayedaiwa kumbaka na kumuambukiza Virusi vya ukimwi, Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), huenda akatiwa mbaroni katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere siku atakayorejea nchini, Habari24 limedokezwa.
ENDELEA ZAID HAPO CHINI--


   Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, zilisema kuwa kumekuwa na shinikizo kutoka ndani na nje ya jeshi hilo kutaka waziri huyo wa zamani ahojiwe kuhusiana na tuhuma zinazomkabili za kutishia kumuua binti anayedaiwa kumbaka na kumuambukiza virusi vya ukimwi.

         Hatua ya polisi kutaka kumnasa Kapuya akiwa uwanja wa ndege, inadaiwa kuchangiwa na taarifa ya Blogs hii wiki iliyopita kwamba baadhi ya vigogo wa jeshi hilo walishiriki kufanikisha safari ya mbunge huyo nje ya nchi huku wakijua fika anatakiwa na polisi.

 Vyanzo vya habari vimeeleza kuwa polisi wamekuwa wakifuatilia kwa karibu siku ya kurejea kwake ili akamatwe na kuhojiwa kuhusiana na tuhuma zinazomkabili.

          Kwa mujibu wa habari hizo ambazo Habari24 imezipata, makundi ya kijamii yanayotetea haki za binadamu ambayo yamekuwa yakitoa msaada kwa binti huyo, nayo yamekuwa yakifuatilia kwa karibu kurejea kwa mbunge huyo.

        Wakati mkakati wa kumnasa Profesa Kapuya ukisukwa, habari zaidi zinasema uchunguzi dhidi ya vielelezo vilivyowasilishwa na binti anayedaiwa kutishiwa kuuawa na mbunge huyo, umeanza.

         Polisi kupitia vielelezo hivyo wamefuatilia ushahidi wa sauti ya Kapuya  iliyorekodiwa na binti huyo wakati alipokuwa akiwasiliana  naye kwa simu na kulinganisha na sauti halisi ya mbunge huyo ili kubaini kama zinafanana.

           Pia makachero hao wameanza kufuatilia namba ya simu inayodaiwa kutumika kumtisha binti huyo na wakati mwingine kutumika kurusha pesa kwa njia ya mtandao, zinazodaiwa kutoka kwa Profesa Kapuya kwenda kwa binti huyo.

         Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema kwa kifupi kuwa polisi inaendelea na uchunguzi na kumsaka Profesa Kapuya kuhusiana na tuhuma zinazomkabili.

         Hivi karibuni, Blogs hii  iliripoti jinsi vigogo wa polisi wanavyonyosheana kidole kwa kuhusika kumsadia Profesa Kapuya kusafiri nje ya nchi huku wakijua fika anatafutwa.
Hata hivyo, kuna utata na kauli zinazopingana kuhusu mbunge huyo.

       Taarifa nyingine zinasema mbunge huyo anadaiwa kusafiri kwenda nchini Sweden kwa masuala ya kikazi, na kwamba atakuwepo huko kwa muda usiopungua mwezi mmoja.
Chanzo kingine kimedokeza kuwa mbunge huyo alidai ametumwa kazi na kigogo mmoja serikalini na atakuwepo nchini humo miezi miwili hadi mitatu.

      Hata hivyo, haijajulikana kazi anayokwenda kuifanya Kapuya ingawa kuna taarifa kwamba safari hiyo imelenga kutuliza upepo mbaya wa kuandamwa na tuhuma za ubakaji na kumuambukiza virusi vya ukimwi pamoja kutishia kuua ambazo zipo polisi hivi sasa.

        Tayari Profesa Kapuya alishafunguliwa jalada namba OB/RB/21124/13 katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

         Blogs hii imekuwa likiandika namba ya simu ya Prof. Kapuya ambayo huwa anaitumia kutuma ujumbe wa vitisho kwa binti huyo.

       Simu hiyo namba 0784993930 inayodaiwa kumilikiwa na Profesa Kapuya, mbali ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno ya kutishia kuua, pia ndiyo inayodaiwa kutumika kutuma pesa kwa njia ya mtandao kwenda kwa binti huyo.

         Wachambuzi wa masuala ya mambo pamoja na Wanaharakiti wamekuwa wakiishutumu serikali kwa kushindwa kumchukulia hatua profesa huyo na mpaka kupelekea kukimbia,licha mototo alifanyiwa vitendo hivyo kinyama kuthibitisha kufanyiwa unyama huo pamoja na ushahidi,

       Licha ya wanaharakati hao kuishutumu serikali ya kwa kushindwa kumchukulia hatua profesa Kapuya pia wamekitaka kitengo cha kupambana na kudhibiti madawa ya kulevya kuanza kumchukulia hatua profesa huyo kutokana na kujisifia kuwa watoto wake wanauza madawa ya Kulevya na hawataweza kuchuliwa hatua hii inajiririsha jinsi kiongozi huyo anavyovunja sheria makusudi huku mamlaka zikimtazama tu bila kumchukulia hatua

No comments: