Na Mohamded Mhina wa Jeshi la Polisi, Zanzibar
Mzee
mmoja mwenye umri wa miaka 55, mkazi wa Kijiji cha Kidutani Gando mkoa
wa Kaskazini Pemba ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye
umri wa miaka 12 na baadaye kujitosa bahari kukwepa mkono wa dola.
Mzee
huyo Muslih Mserembe, alikamatwa na wananchi waliokuwa wamekizingira
kibanda chake kilichojengwa kwa miti, kuezekwa kwa makuti na kukandikwa
kwa udongo wakati akimbaka binti huyo bila ya huruma. (Jina la binti
huyo linahifadhiwa kwa usalama).
Kamishna
wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa(Pichani), amesema kuwa tukio hilo
limetokea jana majira ya saa 12.00 alfajiri wakati binti huyo
akiwafuatilia wenzake kwenda shambani kuokota maembe na ndipo mzee huyo
alipomuona na kumuita
Amesema
baada ya binti huyo kumsogelea mzee huyo, alimwambia waingie ndani ya
nyumba yake akidai kuwa angempatia maembe badala ya kuwafuata wenzake na
ndipo alipombaka na binti kupiga kelele za kuomba msaada.
Kamishna
Mussa alisema baada ya kelele hizo wananchi walikwenda nyumbani kwa
mzee huyo na wakati wakiizingira nyumba yake, mzee huyo alitoka na
kutimua mbio na kwenda kujitosa baharini lakini wananchi nao walijitosa
humo na kumvua kama samaki.
Amesema
baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo, wananchi hao walimpeleka katika
kambi moja ya KMKM na ndipo Polisi walipofika na kumchukua kwa hatua
zaidi.
Kamishna
huyo wa Polisi Zanzibar amesema kuwa binti aliyebakwa alikimbizwa
katika Hospitali ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba kwa matibabu zaidi na
hali yake imeelezwa kuendelea vizuri.
Kamishna
Mussa ambaye amelaani vikali kitendo hicho, lakini amepongeza hatua za
wananchi za kumkamata mtuhumiwa bila ya kumzuru na kumfikisha kwenye
vyombo vya dola akiwa salama.
Mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kujibu shitaka lake.
No comments:
Post a Comment