Taswira ya picha eneo la tukio
Habari
iliyoifikia hivi punde toka jijini Arusha, inaeleza kuwa Ndege ya
abiria aina ya Boeing 787 ya shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopian
Airlines) mchana huu imeshindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutoka na hitilafu iliyokuwepo Uwanjani
hapo na kulazimika kutua kwa dharula kwenye Uwanja wa Mdogo wa
Arusha,hali iliyopelekea Ndege hiyo kusimama nje kabisa ya uwanja huo
huku abiria zaidi ya 200 wakiwa ndani ya ndege hiyo mpaka sasa bila ya
kushuka.
Wataalam
wa Ndege wapo eneo la tukio hivi sasa kutafakari namna watakavyoweza
kuwashusha abiria hao na kutafuta namna ya kuweka sawa mambo ili Ndege
hiyo iweze kuruka.
Globu ya Jamii inaendelea kufatilia kwa ukaribu tukio hilo,na tutaendelea kufahamishana kadri taarifa itakavyokuwa ikitufikia.
PICHA NA MDAU WETU KUTOKA ARUSHA
CHANZO: BLOG YA PAPARAZI
|
Wednesday, December 18, 2013
BREAKING NEWS:WATU 200 WALIOKUWA WAKISAFIRI KWA NDEGE YA ETHIOPIAN AIRLINE WANUSURIKA KUFA BAADA YA KUTUA DHARURA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA ARUSHA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment