Kiingilio
cha chini kwenye mechi ya Mtani Jembe kati ya Simba na Yanga
itakayochezwa Jumamosi (Desemba 21 mwaka huu) ni sh. 5,000. Kiingilio
hicho ni kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648.
Kwa
upande wa viti vya rangi ya bluu kiingilio ni sh. 7,000, viti vya rangi
ya chungwa itakuwa sh. 10,000, VIP C kiingilio ni sh. 15,000, VIP B
itakuwa sh. 20,000 wakati VIP A yenye viti 748 tu tiketi moja
itapatikana kwa sh. 40,000.
Tiketi
zitaanza kuuzwa siku moja katika vituo mbalimbali, mchezo huo
utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Vituo
ambavyo tiketi hizo zitauzwa keshokutwa (Ijumaa) ni Shule ya Sekondari
Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa
Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala,
Uwanja wa Uhuru, na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.
Mechi
hiyo itachezeshwa na Ramadhan Ibada (Kibo) kutoka Zanzibar, ambapo
atasaidiwa na Ferdinand Chacha wa Bukoba, na Simon Charles kutoka
Dodoma. Mwamuzi wa akiba ni Israel Nkongo wa Dar es Salaam wakati
mtathimini wa waamuzi ni Soud Abdi wa Arusha.
|
No comments:
Post a Comment