Na Karoli vinsent
KWA kile kinachotafsiriwa
Chama cha Mapinduzi CCM,kimeanza kuchoshwa maamuzi ya mwenyekiti wa Chama hicho
Rais Jakaya Kikwete Baada ya kupuuza maamuzi ya kamati Kuu (CC) ya CCM ya
kuwafukuza mawaziri mizigo,Mbunge mbunge wa Mwibala(CCM) Mh Kangi Lugola
ameibuka na kumvaa mwenyekiti wa chama hicho na kusema ndio
anayekiua chama hicho.
Mbunge Lugola,
aliyasema leo Wakati alipokuwa na Mahojiano na kituo Cha Runinga Cha Star Tv
katika kipindi cha tuongee asubuhi kinachoruka kila siku ,ambapo alisema
Chama hicho kinayumbishwa na Mwenyekiti wake kutokana na Kupuuzia mamuzi ya
Kamati kuu ya CCM.
ENDELEA--------
“Leo inasikitisha sana Rais anawarudisha Mawaziri mizigo
ambao walikuwa wametajwa na Kamati kuu kuwa hawafai kuenderea kuongoza kwenye
hizo wizara hizo,huku ni kukimaliza chama chetu na kuwapa hoja wapinzania hasa
hawa Chadema ambao wanaenderea na Ziara ya yao nchi nzima”alisema Lugola
Mbunge huyo alishangaa kitendo cha Katibu wa Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye Pamoja Katibu Mkuu, Abdulhaman Kinana Kuenderea
kukaa ofisini huku maamuzi yao yamepuuzwa na Kudharauliwa.
“Ningekuwa mimi kinana au Nape,mala baada ya katibu kiongozi
kutangaza Baraza jipya la Mawaziri siku ileile ningewaita waandishi wa Habari
na Mimi ningeachia Ngazi,Maana mtu unatoa mapendekezo yako unapuuzwa na
Kuzarauliwa,Maana mawaziri hawa hawawezi kuenderea kuongoza wizara hizi hawa
hawafai na sijui kwanini mwenyekiti anawarudisha?alihoji Lugola
Ikumbukwe kwamba chimbuko la mawaziri mizigo lilitokana na ziara ya Katibu Mkuu, Abdulhaman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi taifa, Nape Nnauye, katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, ambapo waliwataja baadhi ya mawaziri kuwa ni mizigo.
Katika mikutano tofauti ya hadhara, viongozi hao wa juu wa CCM walimtaka Rais Kikwete awatimue mawaziri mizigo kwa madai kuwa walishindwa kuendana na kasi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Wakiwa bado ziarani katika mikoa hiyo, Kinana alisema mawaziri mizigo watahojiwa na Kamati Kuu ya CCM na hata baada ya kuwahoji, CC iliyoketi mbele ya Rais Kikwete mjini Dodoma ilipendekeza watimuliwe.
Mawaziri waliotajwa kuwa mizigo ambao jana waliapishwa na kurejea kwenye nafasi zile zile ni pamoja na Waziri wa Kilimo na Chakula, Christopher Chiza, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe.
Lakini baada ya kuwaacha mawaziri mizigo, Rais Kikwete aliwatupa nje mawaziri watano, akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mazingira), Dk. Terezya Huvisa na nafasi yake kuchukuliwa na Dk. Binilith Satano Mahenge na Naibu wake anakuwaUmmy Ali Mwalimu.
Katika mabadiliko hayo, pia Rais Kikwete aliwatupia virago manaibu waziri wanne, ambao ni Gregory Teu, ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Philip Mulugo, ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Goodluck ole Medeye, ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Benedict ole Nangor
Baadhi ya makada maarufu wa chama hicho ambao waliomba
majina yao yahifadhiwe, waliliamwambia mwandishi wa mtandao huu kuwa kitendo
cha Rais Kikwete kutomtimua hata waziri mmoja kati ya wale waliopendekezwa na
chama chake baada ya kujiridhisha kwamba hawana uwezo kiutendaji, ni usaliti wa
hali ya juu na unakiweka chama hicho katika mazingira mabaya.
“Si tu kwamba amekiweka chama mahali pabaya, bali pia amewashushia hadhi mzee Kinana na Nape ambao wamerejesha imani ya wananchi kwa chama kwa kiwango kikubwa,” alisema kada huyo ambaye pia ni mmoja wa wenyeviti wa CCM wa moja ya mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu (CC) ya CCM, alisema hata baada ya Kinana na Nape kutaja majina ya mawaziri mizigo na kutaka waitwe kuhojiwa na Kamati Kuu, Rais Kikwete aliwataka viongozi hao wa chama kuongeza majina mengine ya mawaziri mizigo ili wahojiwe na kuchukuliwa hatua.
“Katika orodha ya Kinana na Nape, Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia, hawakuwemo. Hawa waliongezwa baadaye kwa agizo la Rais. Na bado kulikuwa na pendekezo hata la kutaka kumwita na kumhoji Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kwamba amezembea kupata fedha za msaada kutoka nje kwa ajili ya kuboresha reli na bandari.
“Rais kama mwenyekiti ameshiriki kikao cha kuwahoji na amepokea mapendekezo, leo amepuuzia mapendekezo ya chama. Wana CCM watawaangaliaje kina Kinana na Nape? Watawezaje kwenda tena kwenye ziara na kuikosoa serikali yao?” alihoji kada huyo.
Kiongozi mwingine wa CCM jijini Dar es Salaam, alisema kwa kawaida chama kinachoongoza serikali ndicho chenye nguvu na kinapotoa maoni dhidi ya serikali kiliyoiunda lakini yatekelezwe.
Kada huyo alikwenda mbali zaidi kwa kumlaumu Rais Kikwete kuwa hata kwenye mchakato wa Katiba kuna uwezekano mkubwa mazungumzo yake na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, kuhusu serikali tatu ni tofauti na msimamo anaouzungumza kwenye chama.
“Warioba na tume yake wamekuja na mapendekezo ya serikali tatu, wanapokutana na rais kujadili maoni hayo, bila shaka wanaimba lugha moja, anapokuja kwenye chama kinachoamini kwenye serikali mbili, anaimba wimbo huo huo. Mwisho wa siku msimamo wake uko wapi? Sitashangaa kuona chama kitaachwa kwenye mataa kama kilivyoachwa kwenye hili la wabunge mizigo,” alisema

No comments:
Post a Comment