Ligi kuu ya Vodacom sasa itarushwa
moja kwa moja kupitia Azam TV ili washabiki wa mpira wa miguu Tanzania waweze
kujionea mechi kali za ligi kuu muda wowote na mahali popote zitakapochezwa.
Ligi hizi zitaonyeshwa katikati na mwisho wa wiki.
Ratiba za mwisho wa wiki hii:
Jumamosi tarehe 25 Januari:
Ashanti United na
Young Africans zitacheza Uwanja wa Taifa (DSM)
Azam FC na Mtibwa
Sugar zitacheza Uwanja wa Azam Chamanzi (DSM)
Jumapili tarehe 26
Januari:
JKT Ruvu na Mgambo JKT
zitacheza Uwanja wa Azam Chamanzi (DSM)
Simba SC na Rhino
Ranger zitacheza Uwanja wa Taifa (DSM)
Ratiba za wiki ijayo:
Jumatano tarehe 29
Januari:
Azam FC na Rhino
Rangers JKT zitacheza Uwanja wa Azam Chamanzi (DSM)
Coastal Union na Young
Africans zitacheza Uwanja wa Mkwakwani (Tanga)
Alhamis Tarehe 30
Januari:
Ruvu Shooting na Mbeya
City zitacheza Uwanja wa Mabatini (PWANI)
Mechi zitaonyeshwa moja kwa moja
kuanzia saa kumi kamili jioni.
Katika habari nyingine mpya na za
kusisimua, mashabiki sasa watakuwa na uwezo wakuangalia dondoo za mechi zote
kupitia simu zao za mkononi, ikiwapa fursa ya kuangalia matukio yaliyopita na
kujua yatakoyojiri mechi zijazo.
“Baada ya kupata kibali cha
kuonyesha ligi kuu ya Vodacom, moja kati ya malengo makuu ni kuhakikisha kuwa
tunafikia kiwango cha juu cha kimataifa. Katika kufanikisha hili, tumewekeza
Zaidi kwenye teknolojia ya kisasa ya matangazo ya nje na mafunzo ya wafanyakazi
wetu. Na tumedhihirisha hilo kwamba tumejizatiti katika kutoa matangazo yenye
ubora wa hali juu tuliporusha Ligi ya kombe la Mapinduzi lililomalizika hivi
karibuni” Amesema Rhys Torrington, mkurugenzi mkuu wa Azam Media.
Azam Media Ltd waliingia mkataba wa
miaka mitatu (3) na TFF wa haki za kutangaza na kuonyesha mechi zote za ligi
kuu ya Vodacom wenye thamani ya Tshs 5,560,800,000.
AzamTV tayari inaonyesha chaneli
Zaidi ya 50, zinazojumuisha chaneli maarufu za kimataifa na za kitaifa na
chaneli tatu maalumu kutoka Azam. Chaneli hizo maalum ni:
· Azam
One – Burudani motomoto kwako na familia kutoka bara la Afrika, ambazo nyingi
ni kwa lugha ya Kiswahili.
· Azam
Two – Programu maalum mbalimbali zilizochaguliwa ulimwenguni.
· Sinema
Zetu – Chaneli maalumu inayoonyesha filamu za kitanzania masaa 24.
Kwa ujumla, chaneli hizi zinawapa
fursa wateja wetu kuweza kuangalia kiwango cha juu cha michezo mbalimbali,
filamu, vipindi vya watoto, tamthilia, maisha na burudani na mengineyo kwa bei
nafuu kabisa ya Tshs 12,500/= tu!
Kwa sasa Azam TV inapatakana
Tanzania tu, lakini kwa wiki chache zijazo itaanza kupatikana Uganda na Kenya,
kabla ya kuenea Afrika Mashariki kwa ujumla. Kwa ujumla AzamTV inakupa nafasi
yawewe na familia yako kupata burudani mbalimbali kwa bei rahisi na nafuu.
Azam Media itaendelea kuwekeza
kwenye utengenezaji wa programu mpya za ndani ya nchi kupitia kampuni tanzu ya
Uhai Productions kwa ushirikiano na watengeneza vipindi wa kitaifa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment