Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania inaingia raundi ya 16 wikiendi
hii kwa mechi nne ambapo kesho (Februari 1 mwaka huu) Simba itakuwa mwenyeji wa
Oljoro JKT katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
ENDELEA CHINI-------
Uwanja
wa Azam uliopo Mbagala siku hiyo kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Ashanti
United na Mgambo Shooting kutoka Handeni mkoani Tanga kwa viingilio vya sh.
3,000 kwa sh. 10,000.
Jumapili
(Februari 2 mwaka huu) ni Yanga vs Mbeya City (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,
saa 10 kamili jioni), na Azam vs Kagera Sugar (Uwanja wa Azam Complex, Chamazi
saa 10 kamili jioni).
Ligi
hiyo itaendelea Jumatano (Februari 5 mwaka huu) kwa mechi kati ya Tanzania
Prisons vs Coastal Union (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Mgambo Shooting vs Ruvu
Shooting (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers vs Oljoro JKT (Uwanja wa
Ali Hassan Mwinyi, Tabora), na JKT Ruvu vs Ashanti United (Uwanja wa Azam
Complex, Chamazi).
No comments:
Post a Comment