IGP Ernest
Jumbe Mangu alizaliwa mwaka 1959 mkoani Singida na alipata elimu ya Sekondari katika
Shule ya Tumaini mwaka 1981.
Alijiunga na
Jeshi la Polisi katika Chuo cha Polisi Moshi (CCP) Agosti 17 mwaka 1982
na kuhitimu Juni, mwaka 1983 ambapo alipata mafunzo ya awali ya Polisi.
ENDELEA NAYO HAPO------
Mwaka 1987
alipata mafunzo ya sheria kwa ngazi ya cheti katika Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Novemba mwaka 1992 alitunukiwa shahada ya kwanza ya sheria (LLB) katika
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Juni mwaka
2010, alitunukiwa shahada ya udhamili katika masuala ya usalama katika
Chuo Kikuu Cha Usalama cha Marekani.
Akiwa ndani ya
Jeshi la Polisi amepandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Koplo wa Polisi
(1988), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1992), Mkaguzi wa Polisi (1995), Mrakibu
Msaidizi wa Polisi (1997), Mrakibu wa Polisi (2002), Mrakibu Mwandamizi wa
Polisi (2004), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2006), Kamishna Msaidizi mwandamizi
wa Polisi (2010), Naibu Kamishna wa Polisi (2013) na Kamishna wa Polisi (2013).
Amewahi
kufanya kazi Dar es Salaam katika ngazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa
Upelelezi wa Wilaya (OCCID) na pia Naibu Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mwanza mwaka
1996 akimsaidia Aliyekua RCO wakati huo, Said Mwema. Pia amefanya kazi Dodoma.
Alipoteuliwa
kuwa IGP Saidi Mwema alifanya kazi kwa karibu na Mangu akiwa mmoja wa wasaidizi
wake muhimu makao mkuu ya Polisi kabla ya hupewa majukumu ya kiuongozi.
Vilevile
kamanda huyo aliwai kufanya kazi katika kitengo cha ionterpor yaani polisi wa
kimataifa
No comments:
Post a Comment