Na Karoli Vinsent
KATIBU mkuu wa
chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ameivaa Tume ya Taifa ya
uchaguzi Nchini NEC na kusema inawanyima vijana fursa katika chaguzi
mbalimbali .
ENDELEA HAPO -------
Hayo yalisemwa
leo na katibu wa chama hicho DK Wilbrodi Slaa katika semina iliyoandaliwa na
Tume ya uchaguzi nchini kwa ajili ya vyama vya kisiasa nchini.Slaa alisema
inashangaza kuona mpaka sasa Daftari la kudumu la wapiga kura alijawaandikisha
vijana wanaofikia Milioni 2 na nusu.
“Nidhahili kuwa serikali inawanyima Fursa vijana katika
kupiga kura.inashangaza sana Daftari hili la kudumu la wapigakura
alijafanyiwa marekebisho tangu 2007 hebu jiulizeni ni vijana wangapi
wamefikisha umri wa miaka 18 tangu kipindi hicho hadi leo ?”alihoji Dk slaa
Dk slaa alizidi
kufafanua na kusema Tume ya uchaguzi imeshindwa kufanya majukumu yake,na
kuendesha ofisi kwa mazoea kwa kushindwa kununua mitambo mipya.
“Kwanini serikali
inashindwa kununua mitambo mipya tena kwa ajili ya kuwasajili vijana wapya
katika daftari la wapiga kura,akati leo ukiangalia katika sensa ya watu na
makazi ya mwaka 2012 inasema kila mwaka vijana wanaofikisha umri wa miaka
18 ni zaid ya miloni 3.sasa hebu jiulizeni tangu mwaka 2007 mpka leo ni vijana
wangapi wamenyimwa fursa katika nchi yao iliwaweze kupiga kura”alisema Dk Slaa
Kwa upande,wake
mwenyekiti wa Chama cha Wananchi Cuf Profesa Ibrahimu Lipumba kwa upande wake
aliitupia lawama tume hiyo kwa kufanya kazi yake kizamani kutokana na mtandao
wa Tume hiyo kuonyesha wazi tume hiyo imeshindwa kufanya kazi zake kwa ufasa
“Ukienda kwenye mtandao wa Tume hii ya uchaguzi utapata
taharifa ya uboreshaji wa tume ya uchaguzi ulifanyika 2007,leo tunakuja hapa
tunaambiwa tume imefanya kazi kubwa kazi hipi hiyo? kama si kuwadanganya
wananchi”alisema Lipumba
No comments:
Post a Comment