TIKETI ZA ELEKTRONIKI ZIPO SOKONI
Mauzo ya tiketi za elektroniki kwa
mechi tatu kati ya nne za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zitakazochezwa keshokutwa
(Januari 27 mwaka huu) tayari yameanza, hivyo wanatakiwa kununua mapema.
ENDELEA-----------
Mechi hizo ni kati ya Coastal Union
na Yanga itakayofanyika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Kagera Sugar na
Mtibwa Sugar itakayochezwa Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na ile ya Azam dhidi
ya Rhino Rangers kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Kwa washabiki wa Dar es Salaam
watakaokwenda Tanga kushuhudia mechi kati ya Coastal Union na Yanga
wanashauriwa kuanza safari wakiwa na tiketi zao mikononi, hasa kwa wale
watakaonunua kupitia maduka ya Fahari Huduma.
Tiketi pia zinaweza kununuliwa kupitia
mtandao wa M-Pesa kwa kupiga namba *150*03*02#. Kwa wanaotumia CRDB simbanking
wanaingia kawaida kwa *150*03.
Vilevile tunawakumbusha washabiki kuwa
kwa viwanja ambavyo tayari vina mfumo wa tiketi za elektroniki hakuna tiketi
zitakazouzwa uwanjani, hivyo wanaokwenda kwenye mechi wanatakiwa kuwa na tiketi
zao mikononi.
YANGA YAINGIZA MIL 86/-, SIMBA MIL
53/-
Mechi
za Ligi Kuu ya Vodacom zilizohusisha timu za Simba na Yanga na kuchezwa Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam wikiendi zimeingiza jumla ya sh. 139,850,000.
Yanga iliyoibuka na ushindi wa mabao 2-1
dhidi ya Ashanti United pambano lake liliingiza sh. 86,035,000 kutokana na
watazamaji 14,261. Mechi ya Simba ambayo ilishinda bao 1-0 dhidi ya Rhino
Rangers kutoka Tabora iliingiza sh. 53,815,00 kwa watazamaji 9,629.
Mgawanyo
kwa mechi ya Yanga ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 13,123,983.05,
gharama za kuchapa tiketi sh. 2,910,300 wakati kila klabu ilipata sh.
20,650,211.50.
Uwanja sh. 10,500,107.54, gharama za
mechi sh. 6,300,064.53, Bodi ya Ligi sh. 6,300,064.53, Mfuko wa Maendeleo ya
Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,150,032.26 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar
es Salaam (DRFA) sh. 2,450,025.09.
Mechi ya Simba mgawo ulikuwa Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 8,209,067.80, gharama za kuchapa tiketi sh.
2,910,300 wakati kila klabu ilipata sh. 12,595,211.50.
Uwanja sh. 6,404,344.83, gharama za
mechi sh. 3,842,606.90, Bodi ya Ligi sh. 3,842,606.90, Mfuko wa Maendeleo ya
Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,921,303.45 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar
es Salaam (DRFA) sh. 1,494,347.13.
Vilevile tiketi zinapatikana kupitia
maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo katika maeneo mbalimbali nchini.
Watakaonunua kupitia maduka hayo watapata tiketi na kwenda moja kwa moja
uwanjani.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment