Monday, January 13, 2014

TIGO YAENDELEA KUFANYA KWELI,WATEJA WENGINE WAJINYAKULIA MILION MBILI KILA MMOJA LEO

MRATIBU WA PROMOTION HIYO BI MARY RUTTA AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM
          Kampuni ya tigo leo imekabidi zawadi ya shilingi million mbili kwa watanzania watatu kila mmoja ikiwa ni mwendelezo wa promotion inayoendeshwa na kampuni hiyo ya CHEZA KWA FURAHA UNAPOSHINDA KITITA NA TIGO PESA.

       Akizungumza na wanahabari leo jijini dar es salaam baada ya kukabidhi zawadi hizo mtaribu wa shindano hilo bi MARY RUTTA amesema kuwa jumla ya zawadi za fedha taslimu zenye thamani ya bilion 1.12 zitashindaniwa na watumiaji wa tigo pesa mpaka pale promotion hii itakapofika ukomo katikati ya mwezi wa pili.

        RUTTA amesema hadi sasa wateja 1,215 kutoka kila kona ya tanzania wamejishindia zawadi hizo huku akiongeza kuwa wanatarajia kuwa idadi kubwa sana itafaidika na zawadi hizo.

         Washindi hao waliofaidika na shindano hilo mara baada ya kupokea kitita chao wamesema kuwa wamefurahi sana kupata bahati hiyo na kuahidi kuwa watatumia fedha hizo kuboresha maisha yao.

NURU STANFORD AMBAYE NI MMOJA WA WASHINDI WA MILION MBILI AKIKABIDHIWA MFANO WA HUNDI MBELE YA WAANDISHI WA HABARI

MFANYA BIASHARA AMBAYE NAYE AMESHINDA BW NASSORO YUSUPH AKIPOKEA MFANO WA HUNDI.

No comments: