Dk.Kitila Mkumbo aliyetimuliwa uanachama Chadema.
KAMATI Kuu ya Chadema
iliyokutana Januari 3-4, 2014 katika Ukumbi wa Mbezi Garden, jijini Dar
es Salaam imeamua kuwavua uanachama Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba
kuanzia jana.Maamuzi hayo ni baada ya kunasa
mawasiliano mbalimbali ya Zitto Kabwe na washirika wake akiwemo
anayejulikana kwa jina la Chadema Mpya.
Akizungumza na wanahabari leo,
Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willbroad Slaa amesema malengo ya waraka
wa mabadiliko waliokutwa nao wahusika hayakuwa ya kisiasa tu bali
yalikuwa na lengo la kuimaliza chadema na kuwabomoa viongozi wa chama.
Ameongeza kuwa, chama
kinawatangazia wanachama wote na wapenzi wote kutokushiriki mikutano ama
shughuli zozote za kisiasa zitakazoandaliwa na Zitto Kabwe na washirika
wake kwa jina la Chadema.
Samson Mwigamba ambaye naye amevuliwa uanachama wa Chadema.
No comments:
Post a Comment