Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Sylvester Marsh ambaye amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) anasubiri vipimo vya mwisho ili aweze kuanza matibabu.
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limemtoa kocha huyo nyumbani kwake jijini Mwanza na kumleta Dar
es Salaam kwa lengo la kuhakikisha anapata matibabu zaidi na kwa uangalizi wa
karibu.
Tayari majibu ya kipimo cha kwanza
yameshapatikana, hivyo yanasubiriwa majibu ya kipimo kingine ili aweze kuanza
rasmi matibabu, lengo likiwa ni kubaini kitaalamu ugonjwa unaomsumbua.
No comments:
Post a Comment