MJUMBE WA KAMATI YA UONGOZI YA JUKWAA LA KATIBA NDUGU HEBRON MWAKAGENDA AKITOA TAMKO HILO LEO MBELE YA WAANDISHI WA HABARI |
TAARIFA KWA UMMA
JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tumeendelea
kufuatilia mchakato wa kuandikakatiba mpya ya Tanzania kwa umakini mkubwa tangu
mchakato huu ulipoanzishwarasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
tarehe 31 Disemba 2010.
Katika kufuatilia mchakato wa kuandika
katiba mpya JUKWAA LA KATIBATANZANIA tumekuwa na utaratibu wa kutoa tarifa kwa
Umma kuhusu uendeshajiwa zoezi hili ambalo ni la muhimu sana kwa watanzania
wote bila kujali itikadi, rangi,umri, jinsia, kazi wala elimu. Lengo la kutoa
taarifa kwa umma ni katika kukuza demokrasia na kuongeza ushiriki wa wananchi
kwenye mchakato wa kuandika
katiba mpya.
Mchakato wa katiba kwa sasa unaelekea
kwenye hatua ya bunge maalaum la katibaambalo Rais ameliitisha na linategemea
kuanza vikao vyake mnamo tareheJumanne 18/02/2014 mjini Dodoma. JUKWAA LA
KATIBA TANZANIA linapenda kutoa tarifa kwa Umma juu ya mambo yafuatayo;
ENDELEA KUSOMA TAMKO HILO------
1. RASIMU YA PILI YA
KATIBA
JUKWAA LA KATIBA
TANZANIA linapenda kuipongeza Tume ya Mabadiliko yaKatiba kwa kutoa rasimu ya
pili ya katiba yenye mwanzo mzuri kwa kuingiza baadhiya mawazo ya wananchi kama
yalivyokua yanatolewa wakati wa ukusanyaji maonina wakati wa kujadili rasimu ya
kwanza ya katiba kwenye mabaraza ya katiba.
Rasimu ya pili ya katiba
iliyokabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano tarehe 30/12/2013 ndiyo
itakayojadiliwa kwenye bunge maalum la katiba wakati wa vikao vyake Dodoma. Hii
imeonyesha jinsi Tume ilivyokuwa sikivu na
kuwapa wananchi kile
wanachoona kinawafaa katika Katiba mpya kwa kuzingatia maoni na michango
mbalimbali waliyoitoa kwa Tume.
2. SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA SURA 83
TOLEO LA MWAKA 2012
Lilikuwa ni wazo jema na zuri kwa Serikali
kuandika katiba katiba mpya kwa kuongozwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba,
2012 ili usimamizi uwe wa uwazi zaidi na madhubuti. Ingawa sheria hii
imeshafanyiwa marekebisho mara mbili, JUKWAA LA KATIBA TANZANIA bado
limeendelea kubaini upungufu katika sheria
hii hata kwa kipindi
hiki cha uteuzi wa wabunge 201 ambao sio wabunge wa kawaida wala sio wajumbe wa
baraza la wawakilishi. Sheria hii imempatia Rais wa Jamhuri wa Muungano mamlaka
ya kuteua wabunge 201 kutoka makundi kama walivyobainishwa kwenye sheria na
ilivyotangazwa kwenye gazeti la serikali la
tarehe 07/02/2014.
Kutokana na sheria hii kuminya demokrasia
ya wananchi kuchagua wajumbe wao moja kwa moja kwenye bunge maalumu la katiba,
iliyataka makundi haya kupendekeza idadi ya wajumbe 4-9 ili Rais aweze
kuchangua wale atakaoona wanafaa kuwa wajumbe wa bunge maalum la katiba. JUKWAA
LA KATIBA tulipaza sauti kupinga sheria hii, na tunaendelea kupaza sauti kuwa
sheria hii imedumaza demokrasia na kufifisha matarajio ya watanzania walio
wengi. Kutokana na ubovu
wa sheria hii, Rais
amapewa madaraka ambayo kidemokrasia yalipaswa yaachwe mikononi mwa wananchi
wenyewe.
Hivyo basi, JUKWAA LA KATIBA TANZANIA
limebaini baadhi ya upungufu kwenye baadhi ya makundi katika upatikanaji
wa wajumbe 201 waliotangazwa hivi karibuni; Kwanza, Katika kundi la taasisi
zisizokuwa za kiserikali (20), Kutokana na sheria hii kuwa kandamizi Rais
ameteua baadhi ya wajumbe katika kundi hili ambao JUKWAA KATIBA TANZANIA
linaamini kuwa hawakupaswa kuwepo kwenye kundi hili kwa kuwa kwa namna moja au
nyingine sio wadau katika sekta hii au kwa upande mwingine inaonekana
wazi hawawakilishi mawazo ya sekta hii kama ifuatavyo;
Watu watano (5) kati ya watu 20
hawajulikani kabisa kwenye sekta hii.
1. Ndugu Kingunge Ngombale Mwiru- huyu ni
kada mkongwe wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na waziri mstaafu wa serikali ya
Jamhuri ya Muungano. Kwa kifupi, ni wazi
kuwa mjumbe huyu hana rekodi zozote katika sekta ya taasisi zisizokuwa za kiserikali.
2. Ndugu Paul Kimiti- Huyu ni mwanasiasa
mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na waziri mstaafu wa serikali ya Jamhuri
wa Muungano wa Tanzania,
rekodi yake kwenye
sekta hii inatia shaka.
3. Ndugu Sixtus Raphael Mapunda- Huyu ni
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chama cha
Mapinduzi (UVCCM), huyu ni kiongozi wa chama cha siasa hivyo hakupaswa kabisa
kuteuliwa kwenye kundi hili.
4.
Ndugu Elizabeth Maro Minde- Huyu ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
wilaya ya Moshi hivyo uwepo wake kwenye kundi la taasisi zisizokuwa za
kiserikali unatia shaka.
5. Ndugu Fortunate Moses Kabeja-Huyu
taarifa zake hazijulikani kabisa kwenye sekta husika na hata tulipotumia
mtandao wa google kutafuta habari zake hazijulikani popote duniani.
Pili, katika kundi la
watu wenye malengo yanayofanana (20), Katika kundi hili, JUKWAA LA KATIBA
TANZANIA tuliongea na kutoa maoni kuwa kundi hili litatoa mwanya kupatikana
wajumbe ambao itakuwa vigumu kubaini uteuzi wao umezingatia vigezo
gani. Sheria kutosema malengo yanayofanana ni yapi hili lilikuwa tatizo
ambalo tumeendelea kulipigia kelele wakati wote. Upungufu huu umeonekana kwa
wajumbe sita (6) kwenye uteuzi wa wajumbe kwenye kundi hili
ambapo baadhi ya
uteuzi unatia shaka.
1. Ndugu Paulo
Christian Makonda- Huyu ni katibu wa Uhamasishaji
chipukizi ya Chama
cha Mapinduzi (CCM)
2. Ndugu Julius
Mtatiro- Huyu ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha
Wananchi (CUF)
3. Ndugu Jesca
Msambatavangu – Huyu ni mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) mkoa
wa Iringa
4. Ndugu Abdallah
Majura Bulembo- Huyu ni mwenyekiti wa Jumuiya ya
wazazi taifa Chama
cha mapinduzi (CCM) na mjumbe wa kamati kuu
5. Ndugu Dr. Zainab
Amir Gama- Huyu ni mbunge mstaafu wa Chama cha
mapinduzi (CCM)
6. Ndugu Hassan
Mohamed Wakasuvi- Huyu ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa
Tabora. Kwa kifupi, uteuzi huu umeendeleza dhana ya kwamba mchakato huu hasa
bunge
maalumu la katiba
litakuwa limeshamili wajumbe ambao ni wanasiasa kuliko makundi mengine. Na pia ni vigumu kuelewa
wajumbe hawa wana malengo gani yanayofanana
hadi kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa wajumbe wa bunge maalum la katiba. Majina ya wajumbe toka Zanzibar
katika makundi yote mawili tuliyoyafanyia
uchambuzi tunaendelea
kutafuta taarifa zake na tutazitoa pindi zoezi ya uchambuzi litakapokamilika.
3. MUUNDO WA BUNGE MAALUM LA KATIBA
Kulingana na sheria
ya Mabadiliko ya Katiba Sheria hii inatamka aina tatu za
Wajumbe wa Bunge la
Katiba kama ifuatavyo:-
(i) Wabunge wote wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(ii) Wajumbe wa
Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na
(iii) Wajumbe 201 kwa
mujibu wa Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko
ya Katiba ambayo
inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika.
Makundi hayo ni kama
ifuatavyo;
4
a. Taasisi zisizokuwa
za Kiserikali (20)
b. Taasisi za Kidini
(20)
c. Vyama vyote vya
Siasa vyenye Usajili wa Kudumu (42)
d. Taasisi za Elimu
(20)
e. Watu wenye Ulemavu
(20);
f. Vyama vya
Wafanyakazi (19);
g. Vyama
vinavyowakilisha Wafugaji (10);
h. Vyama
vinavyowakilisha wavuvi (10);
i. Vyama vya Wakulima
(20); na
j. Vikundi vya Watu
wenye Malengo yanayofanana (20).
Ingawa sheria hii
iliwapatia wabunge wote wa bunge la Jamhuri ya Muungano na
wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi kuingia kwenye bunge maalum la katiba
halikuwa wazo baya
sana, ila JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tulipendekeza na
tunaendelea
kusisitiza kuwa ilipaswa wajumbe hawa wachaguliwe na wananchi upya
au wawe theluthi moja
(1/3) ya idadi ya wajumbe wote wa bunge maalum la katiba.
Na makundi
yaliyoainishwa kwenye sheria ya mabadiiliko ya katiba Kifungu 22 (1c)
walipaswa kuwa
theluthi (2/3) ya idadi ya wajumbe wote wa bunge maalum la katiba.
Kitendo cha
waheshimiwa wabunge na Wawakilishi kuingia kwa idadi yao (438) dhidi
ya wajumbe wasio
wabunge wala wawakilishi (201) hakina uwiano na hii ndiyo
sababu kuu tunaamini
kabisa majadiliano kwenye bunge maalum la katiba
yatatawaliwa na
maslahi ya kivyama na kisiasa.
Pia hata katika hawa
wajumbe wengine (201) bado vyama vya siasa vimepewa
wajumbe (42) katika
(201) na bado hata kwenye makundi mengine tumeona namna
Mheshimiwa Rais
alivyoteua wajumbe ambao bila kificho wanaingia kwenye kundi la
wanasiasa. JUKWAA LA
KATIBA TANZANIA tunaendelea kusisitiza kuwa bunge
maalum la katiba
litatawaliwa na maslahi ya kisiasa hasa kwa kuzingatia
Mheshimiwa Rais hivi
karibuni amekutatana na vyama vya siasa ili kupata msimamo
wa vyama kuelekea
bunge maalum la katiba. Hii inatia shaka na kuzidi kutoa picha
kuwa wajumbe
waliowengi watajinasibisha kwenye bunge maalum la katiba kwa
kufuatana na itikadi
zao za vyama.
4.
MAPENDEKEZO YALIYOPITA
Kama tuliyosema hapo
awali wakati wa hatua mbalimbali kwenye mchakato huu wa
kuandika katiba,
JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tumekuwa tukitoa mapendekezo
na kuendelea
kusisitiza masuala muhimu ambayo yalipaswa ama yanapaswa
kuendelea kufuatwa
katika kukamilisha mchakato wa kuandika katiba mpya.
A) Tulipendekeza toka
awali kuwa Mheshimiwa Rais asiteue wajumbe wa Tume
ya mabadiliko ya
katiba Tanzania pendekezo ambalo lilipuuzwa na kutupwa
kapuni. Bado ni imani
yetu kuwa pendekezo hili lilipaswa kufuatwa na
kutekelezwa ili
kukuza demokrasia shirikishi katika kuandika katiba mpya
5
kwani katiba sio ya
chama, mtu wala taasisi yoyote, katiba ni ya wananchi
wote.
B) Tulipendekeza pia
haikuwa demokrasia sheria kumpatia Mheshimiwa Rais
mamlaka ya kuteua
wajumbe (201) kwenye bunge maalum la katiba kwa
kuwa katika kuwateua
wajumbe hawa atakuwa amekandamiza uhuru wa
wananchi walio wengi
ambao kama wangelipewa nafasi ya kuchangua
wawakilishi wao labda
ingelikuwa tofauti na alivyoteua Rais. Tunaendelea
kusisitiza kuwa
haikuwa sawa kwa Mheshimiwa Rais kuteua wajumbe hawa,
Rais aendelee kuteua
viongozi watakaomsaidia kutekeleza majukumu yake
na sio kuteua wabunge
wa bunge maalum la katiba kama ilivyofanyika hivi
karibuni.
C) Tulipendekeza kuwa
haikuwa sahihi kutumia kamati za maendeleo ya kata
(WDC) wakati
upatikanaji wa mabaraza ya katiba ya wilaya ili kujadili Rasimu
ya kwanza ya katiba
kwa kamati hizi zinaongozwa na madiwani ambao wengi
ni wa chama kimoja ya
CCM ambao waliendesha mijadala kwa misingi ya
vyama vyao. Kwenye
mabaraza haya, viongozi wa siasa walitumika sana
kuhakikisha mawazo ya
vyama vyao yanapenya na kuingia kwenye Rasimu
kwa kuandaa wachangiaji
ambao tayari walikuwa wameshapewa maneno ya
kuongea au kuchangia
wakati wa mikutano.
D) Tulipendekeza
uwepo waTume ya mabadiliko ya katiba wakati wa majadiliano
kwenye bunge maalum
la katiba, pendekezo hili lilitupwa. Hivyo basi, Tume
ya mabadiliko ya
katiba imefutwa kabla ya kumaliza jukumu lake la msingi,
tunazidi kusisitiza
kuwa kitendo cha kuifuta Tume ni kinyume na utaratibu wa
kuandika katiba na
kutokuwepo kwa Tume hii kunatia shaka kwamba
inawezekana baadhi ya
watu, vikundi au vyama vya siasa wakatumia fursa hii
kubadilisha maudhui
yote au kwa sehemu kubwa ndani ya Rasimu na kuleta
mambo mapya yenye
tija kwa watu au kikundi cha watu wachache.
5.
MAPENDEKEZO YA SASA
A.
Bunge la Maalum la katiba liwe huru na lionyeshwe moja kwa
moja
Bunge Maalum la
Katiba litaanza vikao vyake mnamo Jumanne tarehe 18/02/2014
mjini Dodoma kwa
takribani siku 70 hadi 90. Wajumbe wa bunge hili tayari
wameshajulikana,
hivyo tunawataka katika kujadili Rasimu ya katiba ili kupata katiba
inayopendekezwa
majadiliano ni muhimu yakajengeka kwenye misingi ya uhuru wa
kutoa maoni na
kuchangia hoja. Pasiwepo na vitisho vya aina yoyote ile wakati wa
majadilianao na bunge
hili ni vyema likaonyeshwa moja kwa moja na vyombo vya
habari vyote nchini
ili wananchi wapate kusikia na kuona mwenendo wake ili wakati
6
wa kura ya maoni
waweze kufanya maamuzi ambayo watakuwa wanafahamu kwa
nini wameamua
kuchukua maamuzi hayo.
Kwa upande mwingine
wajumbe hawa ni sharti waepukane na malumbano ya
namna yoyote ambayo
hayana maslahi kwa taifa, waweke kando ushabiki wa
kivyama, udini,
ukanda na namna yoyote ile ya ushabiki usiokuwa na tija kwa taifa
letu ili waweze
kujadili rasimu ya katiba kwa maendeleo ya taifa kwa miaka mingi
ijayo kama
alivyowasihi Rais wa Jamhuri Mheshindiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
B.
Hoja kuu kwenye bunge maalumu la katiba iwe rasimu ya pili ya
katiba
Kumekuwepo na kauli
tofauti kuhusu maudhui yaliyomo kwenye rasimu ya pili ya
katiba. Kwa mfano
kauli aliyoitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwamba bunge maalum
la katiba linayo mamlaka ya kubadilisha rasimu kwa namna
yoyote ile wakati wa
vikao vyake. Kauli hii inatia shaka kwa kuwa kama bunge
maalum la katiba
likifanya mabadiliko makubwa ya kimaudhui inamaanisha kazi
kubwa na nzuri
iliyofanywa na Tume ya mabadiliko ya katiba itakuwa haina maana
tena na itakuwa
imetumia fedha za umma bila faida yoyote. Hivyo, tunapendekeza
kuwa hoja kuu kwenye
bunge maalum la katiba iwe ni kujadili rasimu na sio kufanya
marekebisho kwenye
rasimu na kama marekebisho yanafanyika yasiondoe maudhui
ya kifungu husika. Na
endapo kutakuwa na hoja inayokosa muafaka basi kifungu
hicho kiachwe kama
kilivyo kwenye rasimu.
C.
Kuimarisha uendeshaji wa kura ya maoni kwa kuwa na Tume huru ya
uchaguzi
na kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura
JUKWAA LA KATIBA
TANZANIA linaona kwamba ili kuimarisha demokrasia katika
upigaji kura ya maoni
unatarajiwa kufanyika mara baada ya bunge maalum la katiba
basi ni muhimu
kuimarisha uendeshaji wa kura hiyo kwa kuwa na Tume huru ya
uchaguzi na kuboresha
daftari la kudumu la wapiga kura na kuandikisha wapiga
kura wapya. Kwa kuwa
Zanzibar wameshaboresha daftari na kuandikisha wapiga
kura wapya, kwa
upande wa Tanzania bara bado hawajaanza kufanya lolote ingawa
Tume ya Taifa ya
Uchaguzi imetangaza nia ya kuboresha daftari la kudumu la
wapiga kura. Hivyo,
tunapendekeza zoezi hili lifanyike mara moja ili wananchi
waweze kutimiza haki
yao ya kidemokrasia ya kupiga kura.
D.
Elimu ya uraia
JUKWAA LA KATIBA
TANZANIA linasisitiza kwamba elimu ya uraia ni muhimu kwa
ajili ya wananchi
kupata uelewa juu ya katiba wanayotaka kuipigia kura ili waweze
kupiga kura wakiwa
wanajua wanapigia kura kitu gani (informed consent). Kifungu
cha 38(2)
kinasema...... Tume italazimika, na vyama vya siasa na vyama vya kijamii
vinaweza kutoa elimu
ya uraia na uhamasishaji juu ya Katiba inayopendekezwa kwa
muda usiozidi siku
thelathini kuanzia siku ya kuchapishwa katika Gazeti la Serikali.
7
Muda wa kutoa elimu
ya uraia kwa siku thelathini hautoshi hata kidogo,
tunapendekeza
uongezwe na kuwa miezi mitatu.
E.
Matokeo Ya Kura Ya Maoni
Katika kifungu cha
41(5) cha sheria ya Kura ya Maoni ya Mwaka 2013 kinaeleza
kwamba “Pale ambapo
wingi wa kura halali zilizopigwa kwenye kura ya maoni
zitakuwa ni “HAPANA”
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka
1977, itaendelea
kutumika”. Dhana hii kwamba nchi inaweza kuendelea kutumia
katiba 1977 baada ya
mchakato mrefu na wa gharama kubwa, na kuwapa ufahamu
wananchi juu ya
upungufu mkubwa wa katiba hii, haifai na ni hatari. Aidha JUKWAA
LA KATIBA TANZANIA linapendekeza
kwamba ni muhimu kutambua maeneo
yaliyosababisha
katiba inayopendekezwa kupigiwa kura ya hapana na kuyaweka
wazi ili wananchi
wayajadili na kufikia muafaka kabla ya marudio ya kupiga kura
mara ya pili.
JUKWAA LA KATIBA
TANZANIA pia linapendekeza kuwa Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania
ya mwaka 1977, ifanyiwe marekebisho makubwa katika
maeneo yote
yaliyoainishwa kuwa na kasoro wakati wa mchakato wa katiba mpya
na kama yamepatiwa
muafaka yaingizwe kama utaratibu wa mpito wa kukamilisha
utengenezaji wa
katiba mpya.
Kwa sababu ya
kuharakisha katiba hii hasa kuhusu suala zima la uchaguzi wa
mwaka 2014/2015.
Sheria za uchaguzi zifanyiwe marekebisho na uchaguzi wa
mwaka 2015 ufanyike
na viongozi watakaoingia madarakani ndio waendelee
kusimamia mchakato wa
kuandika katiba mapya kuliko hii kasi tunayoenda nayo
ambapo bado kuna
mambo mengi yenye kukinzana na maswali yasiyo na majibu
kuhusiana na mchakato
huu na katiba ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977
na Katiba ya
Zanzibar.
6.
HITIMISHO
Tunahitimisha kwa
kusema kuwa tangu mchakato wa kaundika katiba mpya
ulipoanza mambo mengi
yameshafanyika ikiwa ni pamoja na kutunga sheria ya
mabadiliko ya katiba,
kuunda Tume ya Mabadiliko ya katiba, kukusanya maoni kwa
watu binafsi,
mashirika na kutoa rasimu ya katiba, kuendeshwa kwa mabaraza ya
katiba kwa ajili ya
kuipitia rasimu ya katiba na kutoa maoni kwa Tume ya Mabadiliko
ya Katiba, Tume
Kuwasilisha rasimu ya pili ya katiba, Rais kuteua wajumbe 201 wa
bunge la katiba na
sasa tunasubiria bunge maalum kuanza vikao. Hata hivyo ili
mchakato huu wa
kuandika Katiba mpya uweze kukamilika kwa ufasaha na kutoa
katiba yenye maslahi
kwa wananchi walio wengi, ni muhimu:
Bunge maalum la
Katiba liendeshwe kwa uhuru na lionyeshwe moja kwa
moja kwa wananchi
Tuwe na Tume huru
ya uchaguzi
8
Daftari la wapiga
kura liboreshwe kabla ya kura ya maoni kufanyika
Tume ya mabadiliko
ya katiba ni vyema ikarudishwa ili iweze kutoa
ufafanuzi wakati wa
majadiliano ya bunge maalum la katiba ili kuepusha
uchakachuaji wa
maudhui ndani ya rasimu ya katiba
Majadiliano yalenge
masilahi ya taifa na sio masilahi mengine yoyote
Pamoja tujenge taifa,
Imetolewa na;
Deus Kibamba
Mwenyekiti
No comments:
Post a Comment