Tuesday, February 11, 2014

EXCLUSIVE----BAADA YA TAMKO LA WAZIRI NYALANDU JANA,MBUNGE MSIGWA AMVAA WAZI WAZI



NA KAROL VICENT
      
        SIKU moja kupita Baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu kukanusha taarifa iliyoandikwa na Gazeti la “Dailymail”la nchini uingereza.ambapo taarifa hiyo ilikishutumu Chama cha Mapinduzi CCM kuhusika na vitendo vya ujangili nchini,Mbunge wa Iringa Mjini Piter Msigwa amevaa Waziri Nyarandu na kusema aache kudanganya Umma.
ENDELEA HAPO---------

         
          Haya,yalisemwa Leo wakati wa Mahojiano kati ya Mwandishi wa Mtandao huu na Mbunge huyo,ambapo alisema Waziri huyo anaficha mambo na kuficha ukweli ulioandikwa kwenye makala hiyo.

       “Nyalandu ameshindwa kujibu hoja iliyoandikwa na Gazeti hilo wao wamesema Serikali hii imeshindwa kudhibiti vitendo vya ujangili yeye Nyalando anasema Serikali imekamata Meno ya Tembo hiyo ni tofauti kabisa,na yako maswali mengi ameyaacha wazi kwenye makala hiyo hajayajibu na mimi kwa upande wangu naona Makala ya Gazeti hilo iko sahihi”alisema Msigwa.

       Piter Msigwa,ambaye pia ni Waziri kivuli wa Wizara hiyo ya Maliasili na Utalii alisema ni kweli serikali imeshindwa kudhibiti vitendo vya ujangili kwa kuwafumbia macho makada wa chama Chama cha mapinduzi CCM ambao wanahusika kwenye vitendo vya Ujangili.

      “Ni kweli Makada wa CCM wanahusika na vitendo vya ujangili,nashangaa Nyalandu anakataa nini wakati ushahidi uko wazi kwenye mikutano ya kudhibiti vitendo vya Ujangili Duniani vilimtaja mtu anayeitwa Shen ambaye ni kada waCCM kuwa anahusika na vitendo hivyo,leo serikali  haijamchukuliwa hatua”

     “Ripoti ya tokomeza ujangili iliwataja Baadhi ya wabunge wanahusika na vitendo vya ujangili na Serikali imeshindwa kuchuka hatua yeyote kwa wabunge hao,mimi mwenyewe nilisema kuhusu kiongozi wa Chama hicho anayomiliki  Meli za kusafilishia Pembe za ndovu,leo unasema vipi Serikali ya CCM haihusiki na vitendo vya ujangili”alisema Msigwa
        
     Gazeti la “Dailymail” katika Toleo lake la tarehe 6 mwezi huu.katika moja ya Makala yake liliishutumu serikali ya Tanzania kuhusika na Vitendo vya ujangili na pia Makala hiyo pia ilisema Pesa zinazopatikana kutokana na Vitendo vya Ujangili zinatumika katika kukijenga chama cha Mapinduzi CCM.
         
      Ikumbukwe,Ripoti mbalimbali Duniani Zinaishutumu Serikali ya Tanzania kwa kushindwa kuchukua hatua kwa Vigogo wanahusika na Biashara hizo za ujangili huku ripoti hiyo ikiungwa mkono na Mbunge wa Iringa Mjini CHADEMA Piter Msingwa ambapo alisema ni kweli vigogo wanahusika katika biashara ya Ujangili na kumtaja Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Bara ABDURAHMAN KINANA kumiliki Meli zinazopakia Pembe za Ndovu.
        


No comments: