Na Karoli Vinsent
SIKU chache Baada Rais Jakaya Kikwete kutangaza
majina ya wajumbe wa Bunge la Katiba,Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA
kimepinga uteuzi huo na kusema uwezekano wa kupata katiba mpya upo shakani
kutokana na kuwepo na wabunge wa katiba wasiokuwa na Sifa katika bunge hilo.
Hayo,yalisemwa Leo wakati wa mahojiano kati ya
Mwandishi wa Mtandao huu na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo
CHADEMA Tundu Lissu kuhusu msimamo wa chama hicho kuhusu Uteuzi huo ,ambapo
alisema uteuzi huo umejaa ubabaishaji mkubwa.
“Ikulu kujaza watu wao kwenye bunge la katiba,
tumeona CCM wamekuwa na wajumbe wengi kuliko vyama vingine vya kisiasa na Taasisi zingine,na sisi Chadema tulisema
tangu mwanzo endapo tukimwachia Rais ateuwe wajumbe wa katiba ni kupelekea
kupata katiba ya kibabaishaji”
ENDELEA HAPA--------
“ Hao walioteuliwa kila anayezungumza anasema asante Rais kwa kuniteua,hii ni
dalili tosha hao wajumbe ni watu wa Rais,na bunge limejaa watu wa Rais,na kwa
mpango huo hilo sio bunge la katiba mpya”alisema Lissu
Tundu Lissu ambaye ni Mbunge wa Singinda Mashariki
CHADEMA na Vilevile ni miongoni mwa
Wajumbe watakao kuwepo kwenye Bunge hilo la Katiba linalotalajiwa kuanza
Jumatatu ijayo,alisema atapambana katika bunge hilo la katiba na kuhakikisha
katiba inayopatikana iwe ya wananchi na sio ya wanasiasa.
“Tutapambana mpaka mwisho tuhakikishe katiba
inayopatikana iwe ya Wananchi na sio ya
wanasiasana kama ikishindikana tutajitoa katika bunge hilo na Tutawashirikisha
wananchi”alisema Lissu
Kuhusu Posho kuwa kubwa kwa wajumbe wa Bunge la
Katiba mpya
Tundu Lissu alisema hao wanaandika hivyo watakuwa
wanapotosha Umma,
“Malipo ya wabunge yanaamuliwa na Rais na Sheria
inasema hivyo,na Rais anafanya hivyo kwa kutumia walaka na inatakiwa itolewe
walaka kwenda kwa wabunge wa Katiba na hao wanaoandika hivyo wameona huo
walaka?hata mimi sijaona huo walaka wala sijapata”.
Ikumbukwe Gazeti la Tanzania Daima Toleo la Februari
10 mwaka huu lilsema kila mbunge wa Bunge la Katiba atapata milioni 49 kwa siku
70 yaani kila siku mbunge wa Katiba anapata laki saba kwa siku.taharifa hiyo
imepingwa na viongozi na kusema sio ya kweli.
No comments:
Post a Comment