WAKILI EMELDA URIO AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI MUDA MCHACHE ULIOPITA HAPA JIJINI DAR ES SALAAM
Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini tanzania leo kimeitaka
serikali kuwachukulia hatua kali za kinidhamu mkuu wa mkoa wa
manyara,mkuu wa wilaya ya kiteto pamoja na mkurugunzi wa wilaya ya
kiteto baada ya kugundua kuwa wao ndio chanzo kikubwa cha mgogoro wa
wakulima na wafugaji uliotokea mapema mwaka huu na kugharimu maisha ya
watu.
Akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam wakati akitoa tamko la
kituo hiko kuhusu mgogoro huo wakili EMELDA URIO amesema kuwa kituo hiko
kimegundua kuwa viongozi hao ndio chanzo kikubwa cha mgogoro huo baada
ya kuruhusu ukusanyaji wa fedha usio wa halali kutoka kwa wafugaji ili
kulipia gharama za dalali wa kuwaondoa wakulima katika eneo lenye
mgogoro jambo ambalo amesema kuwa lilizua taharuki kubwa na baadae
mapigano makubwa sana Aidha amezitaja sababu nyingine
zilizochangia mgogoro huo kuwa ni mfumo mbovu wa matumizi ya ardhi ya
kijiji kwani wale ambao wanaonekana ni wavamizi walipata ardhi maeneo
hayo kutoka kwa viongozi wa kijiji kwa kutoa kiasi fulani cha fedha.
Katika hatua nyingine kituo cha sheria na haki za binadamu kimelitaka
jeshi la polisi kuhakikisha kinafwatilia kwa makini mgogoro huo na
kuhakikisha kuwa linawachukulia hatua kali za kisheria wale wote
wanaotajwa kuhusika katika mgogoro huo.
|
No comments:
Post a Comment