NA KAROL VICENT
SHIRIKA la maendeleo ya Petrori Nchini ( TPDC)
Limekanusha Taarifa zilizotolewa na vyombo mbalimbali vya Habari, juu ya utafiti wa Mafuta na Gesi asilia
unaoendelea katika maeneo ya Kilosa_kilombero,Tanga na Maeneo ya Kilimanjaro
kuwa mafuta yamegundulika.
SOMA HAPA----------------
Hayo,yalisemwa leo Jijini Dar Es Salaam na
Mkurugenzi Mtendaji shirika hilo wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari, Yona
Killagane alisema taarifa hizo sio za
kweli kuhusu Upatikanaji wa Gesi.
“Tunapenda kuwafahamisha wananchi kuwa
Taarifa hizo sio Sahihi ,tunaomba wananchi
wajue kuwa ili kuwa na uhakika kuwa eneo Fulani ilnamafuta au gesi ni
lazima kuchimba kisima/visima vya
utafiti katika eneo,maeneo husika na kuona kuwa gesi au mafuta vyakitoka yenyewe kisima au visima
hivyo”
“Mpaka sasa hakuna hata kisima kimoja
kilichochimbwa katika maeneo tajwa hapo juu bali kilichofanyika mpaka sasa ni
utafiti wa awali uliohusisha uchukuaji wa takwimu za mitetemo na kufanyia
uchambuzi”alisema Killagane
Vilevile,Killagane alisema utafiti huo
umebaini maeneo hayo yana kina
(Thickness) cha kutosha cha Miamba tabaka ambayo utafiti wa mafuta na
gesi unaweza kufanyika .
Katika, hatua nyingine Mkurugenzi huyo
akasema Mamlaka iliyopewa uwezo wa kutoa taarifa za ugunduzi wa rasilimali za
mafuta na gesi asilia ziko chini ya
waziri wa Nishati na Madini na wala sio chombo kingine chochote ,
No comments:
Post a Comment