Thursday, February 13, 2014

HABARI ILIYOTIKISA MJI LEO NI HII---OKWI RUKSA YANGA

SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limemuidhinisha mshambuliaji Mganda, Emmanuel Arnold Okwi kuchezea klabu ya Yanga ya Dar es Salaam. Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Celestine Mwesigwa ameiambia HABARI24 BLOG  muda huu kwamba, FIFA imewaandikia barua ikiwaambia Okwi ni halali kuchezea Yanga SC. “Suala la Okwi limekwisha, ila siwezi kuzungumza zaidi kwa sasa naingia kwenye kikao, tutatuma taarifa kwa vyombo vya habari baadaye,”alisema Mwesigwa.  

           

No comments: