PRF ISSA SHIVJI AKIWA SEMINA HIYO INAYOFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM |
Na
Exaud Mtei
PROFESA Issa Shivji amesema Rasimu ya pili ya
Katiba ilitakiwa ijadiliwe kwanza na
wananchi katika mihadhara au mikutano ndipo mapendezo yao yangepelekwa bungeni
ili wajumbe wayapitishe huku wakielewa wananchi wanachokitaka.
ENDELEA NAYO----------------------
Pia amesema wajumbe wa Bunge la Katiba
kutoka katika asasi mbalimbali walitakiwa wachaguliwe na wananchi badala ya
ilivyofanyika sasa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete.
Profesa Shivji ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Kwanza wa kigoda cha Mwalimu Nyerere aliyasema hayo Dar es Salaam leo wakati akitoa mada kwenye mkutano wa mafunzo
kwa wajumbe wapya wa Bunge maalum la Katiba.
“Kabla ya Rasimu hii kujadiliwa na wajumbe
wa Bunge maalum la Katiba ilitakiwa wananchi nchi nzima waijadili kwanza na kutoa
maoni yao.
“Maoni hayo ndiyo yangewapa ufahamu
wajumbe wa bunge hilo kuwa Tanzania wanataka Katiba ya namna gani,”alisema
Prof. Shivji.
Akizungumzia kuhusu namna watakavyofanya
kazi hiyo alisema Rasimu siyo msaafu ambao hauwezi kubadilishwa chochote na
kwamba wanaweza kuingiza mapendekezo mapya iwapo kuna haja ya kufanya hivyo.
“Msije mkaingia pale mkavunja nchi yetu,
Sawa Rasimu tunayo tume imekusanya maoni lakini hayawezi kutengeneza
Katiba,”alisema.
Wakati huo huo baadhi ya washiriki wa
mkutano huo kutoka taasisi za kiraia wameonesha mpaka sasa hawaelewi watakwenda
kuzungumza nini au kama wananchi kwa sasa wakiwahoji hawana majibu ya msingi ya
kuwapa.
Dk
Zainabu Gama wakati akichangia hoja kwenye mkutano huo alimwomba Prof.
Shivji wawafafanulie zaidi wajumbe hao kuwa nini watakwenda kusema nini pia
ikiwezekana awatumie mada alizokuwa
akiwafundishia hata kama ni kupitia mndao ili ziwajengee uwezo.
No comments:
Post a Comment