Na Karoli Vinsent
SIKU chache
kupita Baada ya Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa kumshutumu Rais Jakaya
Kikwete kuwa serikali yake imeshindwa kuzuia ujangili hapa nchini, MBUNGE wa
Kilindi (CCM), Beatrice Shelukindo Amemvaa mbunge msigwa nakusema anadanganya
Umma.
Pia,Shelukindo amesema Serikali ya Jakaya Kikwete imefanya kazi kubwa ya
kupambana na ujangili unaoendelea hapa nchini,
Hayo,yamesemwa Leo na Mbunge huyo jijini Dar Es
Salaam,Wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari ndipo mbunge huyo alisema
Anashanga Kauli aliyoitoa Mbunge Msigwa juu ya Rais kikwete kuhusu Ujangili
unaofanyika hapa nchini.
ENDELEA HAPA---------------
“Leo Mbunge msigwa anamshambulia Rais kuwa Serikali ya CCM
ndio inayofanya Ujangili,nataka niwambie wananchi kauli ya mbunge msigwa sio ya
kweli kwani serikali ya Rais kikwete imefanya kazi kubwa sana ya kupambana na
vitendo vichafu vya ujangili”
“Leo ukiangali sensa kuhusu kufa kwa
tembo imepungua kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Rais kikwete
leo utasemaje Serikali ya kikwete haifanyi jitihada za kutokomeza Vitendo vya
ujangili”alisema Shelukindo
Hayo,yalitokana
Habari iliyoandikwa kwenye Gazeti la Dailmail la Nchini uingereza toleo la
tarehe 6 mwezi huu, ambalo liliishutumu Serikali ya CCM kuwa inahusika na
vitendo vya ujangili vinavyoenderea hapa nchini na kukishutumu chama hicho
kinapata pesa kutokana na vitendo vya ujangili na kukiendereza Chama hicho,
Mwandishi wa Gazeti hilo pia likamshutumu Rais kikwete
kuwa anashindwa kuwachukulia hatua vinara wa vitendo vya ujangili,kwasababu ni
marafiki zake,baada ya kauli hiyo ndipo Waziri wa Maliasili na utalii
akakanusha taarifa hiyo na kusema sio za kweli.
Ndipo,mbunge
wa Iringa mjini Piter msigwa CHADEMA akaibuka na kusema Makala
iliyoandikwa na Gazeti hilo la kuwa kuwachulia hatua makada ya wa chama
cha mapinduzi ambao wanahusika na vitendo vya ujangili hapa nchini.
Ikumbukwe,Mbunge
wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, alimtuhumu Katibu Mkuu wa CCM kuwa ni
mmoja wa watuhumiwa kwa ujangili na kwamba serikali haimchukulii hatua, hivyo
kuwaasa Watanzania wamweke mbali na tembo.
Alisema afadhali apige kelele ili tembo wasichukuliwe, twiga wasisafirishwe, apige kelele watu wapate maji, kuliko kukaa kimya aonekane ana nidhamu twiga na tembo wauawe au wasafirishwa
Alisema afadhali apige kelele ili tembo wasichukuliwe, twiga wasisafirishwe, apige kelele watu wapate maji, kuliko kukaa kimya aonekane ana nidhamu twiga na tembo wauawe au wasafirishwa
No comments:
Post a Comment