MECHI YA TWIGA STARS, ZAMBIA
‘LIVE’ ZNBC
Kikosi
cha Twiga Stars kinashuka Uwanja wa Nkoloma, Lusaka nchini Zambia leo kuwavaa
wenyeji Zambia (Shepolopolo) katika mechi ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa
Wanawake (AWC) itakayooneshwa moja moja ‘live’ na televisheni ya Shirika la
Taifa la Utangazaji la Zambia (ZNBC).
Mechi
hiyo itaanza saa 9 kamili mchana kwa saa za Zambia ambapo Tanzania itakuwa saa
10 kamili jioni huku Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage akiwa tayari
ametangaza ‘silaha’ zake kwa mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza.
Watakaoanza
kupeperusha bendera ya Tanzania katika mechi hiyo ambayo kiingilio ni bure kwa
majukwaa yote isipokuwa lile kuu ni; Fatuma Omari 1, Fatuma Bashiru 17, Donisia
Daniel 2, Fatuma Issa 5, Evelyn Sekikubo 15, Sophia Mwasikili 16, Vumilia
Maarifa 10, Mwapewa Mtumwa 9, Asha Rashid 14, Etoe Mlenzi 13 na Shelida
Boniface 7.
Wachezaji
wa akiba ni Maimuna Said 18, Fatuma Hassan 12, Zena Khamis 6, Esther Chabruma
8, Amina Ally 4, Therese Yona 11 na Happiness Hezron 3.
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment