Na Karoli Vinsent
WAZIRI wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Samweli Sitta ametangaza msimamo wake kuelekea
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kusema ,kamwe awezi kumnadi jukwaani Waziri mkuu
aliyejiuzulu,Edward Lowassa endapo atapitishwa na CCM kuwa mgombea wa urais.
endelea----------
Msimamo huu wa Sitta umekuja kipindi ambacho hali ya kisiasa
ndani ya CCM ikiwa imefika katika hatua ya kutisha kutokana na Vita hiyo ya
urais.
Katika kuonyesha hali si swali ndani ya CCM Sitta alisema
“Nitakuwa mwendawazimu kumnadi Lowassa jukwaani wakati muda wote msimamo wangu
dhidi yake unajulikana”Sita alitoa msimamo wake wakati alipokuwa anazungumza na
chazo chetu cha habari,
Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki kupitia CCM
alisema kama chama cha CCM kinataka kuvuka Salama Uchaguzi Mkuu 2015 ni Vema ni
vema kikajitathimini na kusimamia misingi iliyoachwa wazi na Baba wa
Taifa,Mwalimu Nyerere.
“Haiwezekani kishindwe kuchukua hatua.mtu anamwaga pesa
kanisani ,msikitini na kwengine halafu anaangaliwa tu”alihoji Sitta
Kwa mujibu wa Sitta kitendo cha Lowassa kutumia pesa
nyingi za harambee ni ishara tosha kwamba ameanza kampeni kabla ya wakati
na taratibu za chama
“Hadi sasa hvi amrfanya harambeeza sh7bilioni.hizi pesa nyingi
hanazitoa wapi lakini pia,watu wajiulize kwa nini anatumia fedha hizi”alizidi
kuhoji Sitta
UCHUNGUZI ZAIDI
Lakini,Duru za uchunguzi wa mtandao huu umebaini
Lowassa alipaswa kukutana na kamati ya maadili ya chama hicho mnamo tarehe 16.
Hata hivyo Duru hizo zinasema Lowassa hakutokea ofisi ndogo
za chama hizo zilizopo Lumumba jijini Dar ws Salaam lakini alikutana na Katibu
mkuu wa chama hicho Abdulrahaman Kinana katika chakula cha usiku badala ya
kumuita ofisini ili akutane na kamati hiyo.
“Jambo la ajabu la ajabu.Kinana badala ya kumuita
Lowassa ofisini ili ahojiwe kwanini ameanza kampeni mapema yeye alimuita katika
chakula cha jioni kufanya nae mazungumzo kwa kumbembeleza”kilisema chanzo hicho
Kwa mujibu wa Duru hizo zinasema katika kikao hicho cha
kinana na Lowassa inasemekana Lowassa alikuwa anamuomba katibu mkuu huyo apewe
nafasi ya mwisho ya kufanya harambee
KIKWETE AKEMEA
Akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa
Sokoine, Mbeya jana, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alisema
kutoa fedha kunaharibu taswira ya chama hicho na kukiweka katika hatari ya
kupoteza ushindi katika chaguzi zinazokuja.
“Agizo la CCM la miaka mingi iliyopita ni kwamba kila ngazi
kuwa na shughuli za kuwaingizia mapato sambamba na kuwa na mfuko wa uchaguzi.
Agizo hili bado halijatekelezwa na ndiyo linakiathiri chama,” alisema Rais
Kikwete.
Alisema hali hiyo imekiathiri CCM: “Hivi sasa viongozi
wanachukua fedha chafu kutoka kwa watu wenye sifa mbaya na nia chafu. Hata
wanaotoa rushwa hupokewa kishujaa.”
Alisisitiza wanaotoa fedha chafu kwa ajili ya kuimarisha
chama lazima wahojiwe akisema wema huo wameutoa wapi ilhali walikuwapo siku
zote. Alisema taswira ya chama hicho ikiwa nzuri, kitaungwa mkono na ikiwa
mbaya kitachukiwa na watu.
Aliwataka viongozi na wanachama wa CCM kulipa uzito
unaostahili suala la uadilifu na kwamba bila kufanya hivyo chama kinaweza kuwa
imara na kutekeleza majukumu yake lakini kisiungwe mkono na wananchi.
“Tusipoungwa mkono na wananchi tunaweza kupoteza ushindi.
Ndiyo maana chama kikaunda Kamati ya Usalama na Maadili kufanya kazi ya
kuwabana watu wanaokiuka maadili, naomba kamati hizo zifanye kazi yake
ipasavyo,” alisema.
Alisema kamati hizo zisipokuwa makini zitaathiri hadhi na
kukubalika kwa CCM katika jamii.
“Vitendo hivi vibaya lazima tuvikatae na tuvipige vita kwa
nguvu zetu zote. Tusiwaache watu wachache wanaotaka uongozi wa gharama yoyote
waharibu sifa nzuri ya CCM.”
Alisema watu hao wakiachwa itajengeka dhana potofu kwamba
uongozi ndani ya CCM ni wa kununua.
WANAOLUMBANA NA LOWASSA
Malumbano kuhusu ‘safari’ ya Lowassa yalianza kwa baadhi ya
wenyeviti wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Geita, Joseph Kasheku
`Msukuma’ kukana kauli ya Mwenyekiti wa CCM wa Singida, Mgana Msindai kuwa
wenyeviti wote wa CCM wa mikoa walikuwa wanamuunga mkono Lowassa. Hata hivyo,
Msindai alikanusha suala hilo.
Makamu Mwenyekiti wa zamani wa CCM, John Malecela na Mkuu wa
Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda pia
walimtuhumu Lowassa kwamba anakivuruga chama hicho kwa kuanza kampeni mapema za
urais.
Hata hivyo, kauli zao zilipingwa vikali na makada wengine wa
chama hicho akiwamo Mgeja, Mwenyekiti wa zamani wa CCM wa Dar es Salaam, John
Guninita na viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM wa Morogoro.
No comments:
Post a Comment